Kiukweli Huwa "SICHEKESHWI" na Vichekesho Vya "MKALI WENU (TVE)"


Pengine ni stress tu za maisha zinanifanya nishindwe ku enjoy vichekesho vya huyu jamaa kwa maana kila kichekesho chake nnachotazama hua sicheki ama kufurahi kabisa naona kama ni vitu vile vile tu vilivyokosa ubunifu,

Au pengine ni sanaa ya bongo hasa hasa kwenye fani hii ya comedy ndio kusema imekosa ubunifu kabisa siku hizi,kwa maana vitu ambavyo wanatuletea tufurahi naona kama ni vitu vya kawaida mno kiasi kwamba labda mtoto mdogo ambae akili bado haijapevuka ndo anaweza vunjika mbavu kwa kucheka,

Ama pengine ndo kusema akili zetu sisi watazamaji ndo zimevurugwa labda ni kutokana na mambo yanayoendelea kwenye nchi hii na ndio kusema hata tukitazama vichekesho siku hizi akili zetu zinakua zishachoshwa na siasa na changamoto nyingine za nchi hii??

Kiukweli nashindwa kupata majibu,Na hii sio kwa msanii huyu tu ni karibia wasanii wote wa sanaa ya uchekeshaji naona hawana ubunifu kabisa sikuhizi.

Sijui kwenu nyie wadau??


Jaribu Kutazama CHURCHILL SHOW ya Kenya Ni nzuri.Kuna watu Kama MCA TRICKY,PROF HAMMO nk utafurahi Sana.
 
Jaribu Kutazama CHURCHILL SHOW ya Kenya Ni nzuri.Kuna watu Kama MCA TRICKY,PROF HAMMO nk utafurahi Sana.
Exactly sema trick sanaaaaa, wako vizuri bila kumsahau MC Jessey, na Njoroge, yule Jamaa aneigiza movie na ujambazi lazima uvunjike mbavu kwa kucheka
 
Exactly sema trick sanaaaaa, wako vizuri bila kumsahau MC Jessey, na Njoroge, yule Jamaa aneigiza movie na ujambazi lazima uvunjike mbavu kwa kucheka

Haswaa.Mimi ninawakubali Sana.Wanachekesha Sana.
MCA TRICKY
Prof HAMMO
Mammito
Consumator
Njoroge
na wengineo. wako vizuri
 
Kwa bongo ukimtoa majuto, serious funny wanafuata. Halaf joti kwa mbaaaliiiii.. Ila mkali wenu huyo aendelee kubaki kuwa mkali wenu tu
 
Dah! Yawezekana ni kweli lakini kiukweli ubunifu skuizi umeshuka sana mkuu, Yani hata Joti wa skuizi sio joti yule kipindi kile cha ze komedi,sijui tatizo liko wap.
Sio wewe tu. Tena mimi niseme ''wachekeshaji'' wa Tanzania wanaoweza kunifanya nicheke sikui kama wapo. (kwa sasa). Sana sana najikuta nakasirika badala ya kucheka! Kuna watu kama marehemu Mzee Jongo ndio alikuwa comedian wa ukweli kabisa. Hata Mzee Jangala yuko vizuri. Hao mnaosema sijui kina Joti and co kwangu mimi naona ni wakasirishaji na si wachekeshaji.
 
inaelekea wewe una stress tuu....
Lakini mimi huwa namkubali Mangaje na yule mwinjilisti
 
Nimekuja kugundua kucheka ni maamuzi.
Especially inapofika wakati mtu anafanya jambo maalumu ili kukuchekesha .

Ukiamua jambo hilo unaweza kuliamulia maamuzi ya kucheka am usicheke.


Mfano:

Same same Video hapo kwnye uzi , itazame then k
usicheka , kisha Irudie na fanya maamuzi ya kucheka ., utajikuta unacheka pia .

So kucheka ni maamuzi ya mchekeshwaji.
 
Back
Top Bottom