Kiukweli dunia ni ya wachache

Kiukweli dunia ni ya wachache

Level ya umaskin wa ukoo wenu ni ipi ebu nipe picha

Kuna shida pahali huo umaskini sio wako ni wa ukoo wako, maadam ukiona unatoa bila kupokea jua kuna pahala pana shida, Haezekan ukoo wa watu 30+ wote maskini level ya chini haezekani
Sure kuna maagano itakua yapo kwenye ukoo wao...hata akipewa kazi TRA ni bado atasota tu..ukane ukoo wako kiroho alafu tafuta mishe ya kufanya
 
Hayo makundi ya kigaidi Yana njaa ya ubongo na Sio njaa ya tumbo,hao mfadhili wao mkuu ni kiranja wa mashoga watakuwaje na njaa
 
kutokuyasikia ww sio sababu yasitokee, Rudi kwenu Jua ilikuwaje kwa maana ukijua shida ndo utajua jinsi ya kuomba usije ukaomba kilokole tu.

Itabidi uingie kwenye maombi ya siku saba Nasfi yako ikishuhudi ufunge utafunga, First born ni shidah Muombe Yesu kwa dam yake ya samani ufanyike lango upya ili ufanyike baraka ww na kwajili ukoo wa kwako.

Una miaka mingap?
Usimshauri tena mtu kuhusu mafanikio. Wewe mwenyewe unahitaji kushauriwa
 
1. Napambana na sifanikiwi
Ila kuna wachache hata hawatoi jasho wanakula na wanasaza.

2. Nkaona huenda shda ni elimu, nikasoma bado si msaada....mwaka wa 9 sasa mtaani, wenye ramani wanahitimu leo kesho wapo kwenye mfumo.

3.Nikashika jembe, piga mpini haswa mpaka viganja vinafanana na unyayo. Still ardhi sio yangu.

4. Nikaamua weka vyeti kabatini, ingia msituni nkachoma mkaa,, Maliasili wakanikalia koo na kunichomoa tonge lililo kooni tayar ..mzigo ukawa mali yao na faini nkalipa.

Naelewa sasa chimboko la BOKOHARAM, ISIS, ALSHABAAB, NI NJAA..
Pole sana kinacho kusumbua unatafuta utajiri,utajiri hautafutwi bali uja wenyewe
 
Mkuu, if you can make room for two, naomba ni tag along na mimi.

Elimu yangu ni bachelor's degree in management of social development. Nipo Kigamboni na umri wangu ni miaka 24.
Social skills zip unazo?
 
Social skills zip unazo?

•Social welfare advocacy
•Anti-gender based violation campaigns
•Conflict mediation

Hizo zote nimezifanya practically kwenye NGO niliyokuwa nikijitolea couple of months ago.
 
Pole sana kinacho kusumbua unatafuta utajiri,utajiri hautafutwi bali uja wenyewe
Sitafuti utajiri kaka..najua una hatua na ngazi zake... Nikipata hata kibarua cha elfu 8 kwa siku..kitanikidhi...ili mradi iwe ni kaz endelevu angalau kwa miaka3.. ntakuwa nimesave mtaji..nipe connection
 
Ni kubwa kaka.. ni ya wazazi (wa kiume) waliowekeza ulevi.. nilipambana kwa pesa ya kujikimu (boom) nikawajengea pa kuishi angalau pasipovuja... Nikajisahau mwenyewe.... Nikapambana kuwabadili wawe wachapa kaz za shamba,, angalau kwa sasa wanajiinua kidogo... ni wakulima wa kahawa..mfumo wa mauzo pia kikwazo kwa mwenye kipato kidogo.. hali tete..ila sijawa mvivu,,, nikasaka ajira private schools.. mwaka jana nikapata ajali pindi tunaenda kusimamia mitihani darasa la 7...kila njia ikajifunga kuanzia hapo
Hapo kwenye kuwajengea ndio kosa la umasikini wako lilipoanzia. Yaan fedha ambayo ilikuwa msingi wako Sasa wewe unauridisha nyuma. Jaman wazazi hebu pigeni kaatua kidogo ili watoto nao waje wapate urahisi wa Maisha. Umasikini mwingine unasababishwa na wazazi kwa kiasi kikubwa. Miaka 50,60 kweli hata kama ulikuwa unanunua tofali moja kila wiki c mtu ingekuwa hata na vivyumba viwili vizuri vya kulala na badae hata watoto wanakuja kufanya upanuzi. Najua wengi watasema Maisha ya wazee yalikuwa magumu, sio utani wengi wanapata lakini pombe kwa wingi.
 
Ni kweli kiongozi..basi majuto ni mjukuu
 
Hili swala la umaskini wa ukoo huwa linanikatisha sana tamaa ya kupambana coz wanamaanisha hata tupambane vp atuwez kutoboa et sababu koo zetu ni maskini huwa nachukia sana hii kitu
 
Back
Top Bottom