Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 40,334
- 72,798
"Sijui sisi nani ametuloga" ni kauli ya Mheshimiwa Rais juzi. Jee anazungumzia kina nani? anamaanisha wapitisha sheria na kuandaa mikataba hiyo yaani Serikali ya ccm, CCM yenyewe na yeye kama mmoja wao. Ni kweli nani kawaloga CCM? nani aliwaloga mawaziri (JPM inclusive)? nani aliwaloga wabunge wa NDIYO ambao ndio wengi?
Kama sasa hivi anatenda yale yaliyo sababisha Kina Zitto wafungiwe bungeni miezi kadhaa, Mnyika kutolewa na askari bungeni, Kina Lissu na wengine kuzomewa hadi kutukanwa na wabunge wa CCM, basi ni kuwa anakubaliana nao kuwa waliona wizi huo mapema lakini kwa sababu upande huu aliokuwepo muheshimiwa Rais wakati huo walikuwa "WAMELOGWA" basi hawakuona na yeye sasa hivi anashindwa kutamka wazi tuu kuwa CCM IMEHARIBU NCHI.
Sasa nani kawaloga? au ule Unga unga Chenge alioonekana akimwaga Bungeni usiku ndio ulozi wenyewe?
CCM iache kelele,inyamaze kimya maana tunakoelekea JPM atakuja sema wazi kuwa yenyewe ndio chanzo cha shida yote hii.