CCM nao wameshindwa uchaguzi 2020, mshindi Dkt. Magufuli tu

IslamTZ

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
309
182
CCM nayo imepoteza katika uchaguzi huu, mshindi JPM tu

Abu Kauthar

Uchaguzi wa 2020 Tanzania umepita. Inasemekana Watanzania wameamua kukirejesha chama tawala, CCM kwa kishindo. Kishindo kilikuwa ni kikubwa mno. Kishindi cha bomu lililoteketeza sio tu vyama vya upinzani, bali hata mmea uliobeba ua zuri liitwalo demokrasia ambalo ndio hubeba tunda tunalolijua kama ‘vyama vingi’.

Huenda kishindo cha bomu hili la ushindi litaitekeleza hadi CCM yenyewe wakabakia wasanifu wa bomu lenyewe. Ni suala la muda tu tutajua.

Kuna wanaoshangilia. Hawa ni wanachama, wafuasi na wapenzi wa CCM. Wapo wanaouguza majeraha ya maumivu ya kushindwa, ya moyoni na baadhi hata katika miili yao. Hawa ni wafuasi wa vyama vya upinzani ambao vyama vyao vimepata kipigo cha mbwa mwitu.

Lakini lipo kundi la tatu la wale ambao wameweza kujitoa kifikra katika boksi dogo la ‘chama’ anachokishabikia iwe ni CCM au upinzani na kuzingatia zaidi maslahi ya taifa. Hawa wanasikisikishwa na wanaumia kutokana na yaliyotokea. Mi ni mmoja kati yao.

Mimi ni muumini wa demokrasia. Naamini demokrasia sio siasa au nadharia timilifu lakini ni njia pekee yenye nafasi kubwa ya kufanikiwa katika jamii yenye watu mchanganyiko kama ya Tanzania kuweza kujenga na kuhakikisha ustawi wa nchi kiutulivu, mshikamano, maendeleo ya vitu na watu nk.

Lakini demokrasia niliyoiamini imekejeliwa; imetusiwa, imebakwa katika namna ambayo sikuwahi kudhani ingeweza kutokea Tanzania. Si kupitiliza mipaka viongozi wa vyama vya upinzani walipougeuza jina uchaguzi huu na kuuita ‘uchafuzi’. Ulikuwa ni uchafuzi dhahiri kwa kigezo chochote kile.

Nikiwa muumini wa demokrasia nikiangalia mtiririko wa matukio kuanzia 2015 pale awamu ya tano, naona wazi wazi kuwa huenda yajayo katika mustakbali wa nchi yetu yasiwe ya kufurahisha.

Tunachokiona ni kuwa, nchi inazidi kuponyoka kutoka mikononi mwa wananchi na kuingia katika udhibiti wa wachache ambao huamua hatima ya kila mtu kutokana na wanavyojisikia moyoni.

Ni ujinga kudhani kuwa Chama Tawala kinapata nguvu zaidi kwa hujuma iliyofanyika dhidi ya demokrasia na dhidi ya upinzani. Si kweli. Anayezidi kupata nguvu na kujilimbikizia mamlaka, madaraka ya kuamua chochote ni mtu mmoja tu: John Pombe Magufuli, aliyetangwa na tume ya uchaguzi kuwa mshindi wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Spika wa Bunge katika hafla ya kuzinduliwa bunge amesema wao, wabunge wa CCM, wamedhaminiwa na rais kuja kwao bungeni. Na ni wazi kuwa, kwa kuwa wao ni wengi, basi kimsingi bunge la sasa linadaiwa fadhila na Rais Magufuli. Tunaona kila uchao viongozi wa mahakama nao wakitoa kauli zinazoashiria kudhalilika kwa mhimili huo mbele ya Magufuli.

Kiujumla, ni Rais John Pombe Magufuli pekee anayeweza kuamua kwa kadri anavyojisikia moyoni, sio tu aina gani ya maendeleo yaletwe, yaende wapi, nani akose, kwa kiasi gani, na nani apate. Na hii inatishia ustawi wa nchi yetu kwa sababu yeye sio malaika; na hata katika ubinadamu wake twaona mapungufu mengi ikiwemo kukosa utu, upendeleo, ukatili na kadhalika.

Mungu ibariki Tanzania
 
"Muheshimiwa Rais Nikushukuru sana
Maana wewe ndio umetudhamini wabunge kuwepo hapa"
Jobu ndugae.

wabunge wa CCM, wamedhaminiwa na rais kuja kwao bungeni. Na ni wazi kuwa, kwa kuwa wao ni wengi, basi kimsingi bunge la sasa linadaiwa fadhila na Rais Magufuli.

MTU MMOJA JIWE ANAZIDI KUHARIBU NCHI NA WAPUMBAVU TUNAMCHEKEA.
 
Na leo kasema kituo cha uwekezaji anakihamishia ofisni kwakwe,kwa hali hii wawekezaji watakuja kweli
 
Kama kawaida, wa kujitoa ufahamu watapita hapa na kuchafua hali. Na kauli ni zile zile, "wapinzani wamekataliwa na wananchi, wananchi wameona na kukubali kazi ya JPM..nk".
 
Back
Top Bottom