Kiuhalisia Magufuli anaiumbua CCM ila anashindwa kutamka wazi

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,707
71,018
"Sijui sisi nani ametuloga" ni kauli ya Mheshimiwa Rais juzi. Jee anazungumzia kina nani? anamaanisha wapitisha sheria na kuandaa mikataba hiyo yaani Serikali ya ccm, CCM yenyewe na yeye kama mmoja wao. Ni kweli nani kawaloga CCM? nani aliwaloga mawaziri (JPM inclusive)? nani aliwaloga wabunge wa NDIYO ambao ndio wengi?

Kama sasa hivi anatenda yale yaliyo sababisha Kina Zitto wafungiwe bungeni miezi kadhaa, Mnyika kutolewa na askari bungeni, Kina Lissu na wengine kuzomewa hadi kutukanwa na wabunge wa CCM, basi ni kuwa anakubaliana nao kuwa waliona wizi huo mapema lakini kwa sababu upande huu aliokuwepo muheshimiwa Rais wakati huo walikuwa "WAMELOGWA" basi hawakuona na yeye sasa hivi anashindwa kutamka wazi tuu kuwa CCM IMEHARIBU NCHI.

Sasa nani kawaloga? au ule Unga unga Chenge alioonekana akimwaga Bungeni usiku ndio ulozi wenyewe?

CCM iache kelele,inyamaze kimya maana tunakoelekea JPM atakuja sema wazi kuwa yenyewe ndio chanzo cha shida yote hii.
 
CCM toka enzi za Nyerere haijawahi kuacha kuwashughulikia wabadhirifu ndani na nje ya CCM.
FB_IMG_1497359565714.jpg
 
CCM toka enzi za Nyerere haijawahi kuacha kuwashughulikia wabadhirifu ndani na nje ya CCM.
For 20 years tunaibiwa madini jee walishughulikiwa namna gani? acha porojo. NANI KATULOGA? Jibu swali la JPM
 
Bora tuliorogwa! kuliko ofisi ya ufipa ambayo haiendani na ruzuku, swali linakuja jee? Tungewapa dhamana si wangetuuza utumwani.
 
"Sijui sisi nani ametuloga" ni kauli ya Mheshimiwa Rais juzi. Jee anazungumzia kina nani? anamaanisha wapitisha sheria na kuandaa mikataba hiyo yaani Serikali ya ccm, CCM yenyewe na yeye kama mmoja wao. Ni kweli nani kawaloga CCM? nani aliwaloga mawaziri (JPM inclusive)? nani aliwaloga wabunge wa NDIYO ambao ndio wengi?

Kama sasa hivi anatenda yale yaliyo sababisha Kina Zitto wafungiwe bungeni miezi kadhaa, Mnyika kutolewa na askari bungeni, Kina Lissu na wengine kuzomewa hadi kutukanwa na wabunge wa CCM, basi ni kuwa anakubaliana nao kuwa waliona wizi huo mapema lakini kwa sababu upande huu aliokuwepo muheshimiwa Rais wakati huo walikuwa "WAMELOGWA" basi hawakuona na yeye sasa hivi anashindwa kutamka wazi tuu kuwa CCM IMEHARIBU NCHI.

Sasa nani kawaloga? au ule Unga unga Chenge alioonekana akimwaga Bungeni usiku ndio ulozi wenyewe?

CCM iache kelele,inyamaze kimya maana tunakoelekea JPM atakuja sema wazi kuwa yenyewe ndio chanzo cha shida yote hii.
na alietuloga ameshakufa, sa sijui twende kwa nani akatuague, sijui Gwajimaaa!!!!!!!!
 
Je kwa mkristo kutubu ni dhambi?
 
Bora tuliorogwa! kuliko ofisi ya ufipa ambayo haiendani na ruzuku, swali linakuja jee? Tungewapa dhamana si wangetuuza utumwani.
Matumizi ya ruzuku ni kujenga ofisi kubwa? Jengo lao la Ufipa wameona linawatosha kwa kazi za kiofisi shida iko wapi?
Ni sawa na baba mwenye kipato, kuna mwingine ataona ni vema kipato hicho akitumie kununua suti na magari ya kutembelea na mwingine atumie kusomeshea watoto. Chadema wanatumia fedha zao kujengea ufahamu wa demokrasi wa raia.
 
Sio dhambi, ila lazima ukiri kwa kinywa chako makosa yako.
CCM walikosea na sasa wanatubu na wanajirekebisha. Kosa lipo wapi mbona kila kukicha wewe na marafiki zako akina Salary Slip et. al. mnakazana na maandiko. Tuanze kufikiria kwenda mbele baadala ya kuhangaika na historia na mihemuko ya CDM na CCM tumewachoka sasa
 
Yaani ccm kwa kulisababishia hasara taifa miaka 50 bado wanaona haitoshi wanakuja na ngonjera nyingine naona wanaanza mikakati ya kulisababishia taifa hasara tena
 
ccm wanafiki sana, walimpa uwaziri muhongo wapinzani wakahoji kwa nini mwizi kupewa hii nafasi, mkuu akamwambia "wewe chapa kazi" hawakutosheka, wakamchagua chenge kama mwenyekiti wa bunge wapinzani wakalalamika, kwani nini hawa wezi, wakazomewa..leo ccm wanasema mikataba ipelekwe bungeni halafu ikaguliwe upya chini ya mwenyekiti mtuhumiwa chenge, mwizi mwingine Dalali Kafumu, Ngeleja,. halafu eti wanatoa zuio wasisafiri nje ya bunge bali waendelee kuwa bunge kufanya kazi za wananchi wakati wezi wa kuku wanafia magereza.. CCM haijawahi kumuweka mwananchi mahali salama.
 
Nawapenda sana saana CCM maana wana CONFIDENCE ya ajabu sana yaani Watu wana uwezo wa Kupinga kwa viapo mambo ambayo waliyasapoti kwa makusudi kabisa na kwa makofi na kwa vilio, kama yule mbunge aliyelia ili bunge lisionyeshwe LIVE
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom