Kituo cha uzalishaji wa umeme unaotokana na joto la ardhini kikikamilika kitazalisha Megawati 70

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,817
11,993
e2fd361b-08c0-4320-9c61-fc98d789e005.jpeg

7c23fbd8-e7c0-4086-b726-0182958ab2bc.jpeg
Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Jaffar Haniu amefanya ziara na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Kituo cha uzalishaji wa umeme unaotokana na Umeme wa Joto ardhi kilichopo Kijiji cha Mbeye, Kata ya Isongole.

Katika ziara hiyo Haniu ameagiza Mkandarasi anayetekeleza mradi huu kufanya kazi kwa bidii ili kusaidia upatikanaji wa nishati hiyo kwa wakati.

Aidha, ameagiza kuendelea kuajiri vijana wanaopatikana katika mazingira yanayozunguka mradi huu ili kupanua wigo wa ajira kwa Watanzania.

Kituo hiki kilichopo ndani ya Msitu wa Ziwa Ngosi kinatarajia kuzalisha kiasi cha Megawati 70 mara kitakapokamilika.
cf8ffb17-36c7-4933-a85f-1c92b4b8da9b.jpeg
Umeme huu unaozalishwa kwa kutumia mvuke uliopo chini ya ardhi unatarajia kuleta manufaa lukuki ikiwemo kuingizwa katika grid ya Taifa na hivyo kupanua upatikanaji wa umeme nchini, Pamoja na kupatikana joto asilia litakalotumika kukaushia mazao kama chai, pareto, Kakao, kahawa na mengine mengi.

Mkuu wa Wilaya ameeleza kuwa mradi huu unaenda kuondoa adha ya ukataji miti ovyo kwa ajili ya upatikanaji wa nishati hasa katika viwanda vya ukaushaji wa mali mbichi.
 
Umeme utatoka Rufiji halafu watasema ni wa Ardhi joto. Zanzibar nao wameanzisha mradi wao , utatoka Rufiji halafu waseme ni wao, Abduli nae kawahi Uganda..
 
Back
Top Bottom