Kituo cha Polisi cha Mugumu chavamiwa!

Taarifa zilizotufikia punde zinasema kuwa wananchi wenye hasira wakiwa na silaha za jadi, wamevamia kituo cha polisi mjini Mugumu wakishinikiza kuwahukumu watuhumiwa wa mauaji!kweli hawa makurya hawana imani na polisi. Mh Vuai ameligusia hili kupitia taarifa ya habari ya ITV. Je wananchi kujichukulia sheria mikononi ni matokeo ya wananchi kutokuwa na imani na CCM

attachment.php


Source: Mdau -Mugumu
Haa haa haa, Aise sina mbavu, kweli Tz imebadilika, nikiangalia hii picha jamaaa alivyoshika panga, ninajiuliza matokeo yake nini? Sasa serikali na polisi wafikirie hali hii ikitokea Tz nzima polisi watafanya nini kwa hawa raia.
Kila kukicha mnatutangazia chukua tahadhari ina maana serikali haichukui tahadhari. Serikali mnakiburi sana sasa hicho kiburi kunasiku kitatoka chenyewe, mwangalieni mwezenu Gadaffi anavyonyolewa wakati alikuwa anajiona kama mungu mtu. Yaani imelala utafikiri imeenda likizo.
 
Basi kuna wanasihasa fulani watanunua hiyo kesi wanapenda kweli kuseek attation kwa gharama yoyote kaaazi kweli kweli

Mi nadhani tuangalie haki na kweli, na wala siyo swala la siasa. Kama kunahaja ya kununua siasa katika kutetea wananchi wasio na utetezi wowote naona siasa hizo ni bora kuliko siasa za kunyamanza kimya kwa kuogopa attention ya watu.

Watanzania tufike mahala siasa na utendaji wa serikali tuvitofautishe, nadhani matatizo yanayojitokeza hivi sasa yanachangiwa na viongozi wa serikali ambao hawawezi kutofautisha utendaji wa serikali na wa kisiasa.
 
Basi kuna wanasihasa fulani watanunua hiyo kesi wanapenda kweli kuseek attation kwa gharama yoyote kaaazi kweli kweli

wanasihasa ndo nini?attation ndo nini? hivi si muwe mnaandikia tu kiswahili?? shukle za kata hizi zimeleta mambo sana khaaaa..halafu manalaumu oooh mitihani ya NECTA migumu mtafaulu vipi kama hiki ndo kiingereza chenu...
 
wanasihasa ndo nini?attation ndo nini? hivi si muwe mnaandikia tu kiswahili?? shukle za kata hizi zimeleta mambo sana khaaaa..halafu manalaumu oooh mitihani ya NECTA migumu mtafaulu vipi kama hiki ndo kiingereza chenu...


Kigogo!????
 
Wananchi hawana imani na Polisi ndio maana wameamua kwenda kuvamia kituo ili wawamalize hao wauaji. Maana kuna uwezekanao kuwa hao watu watarudi mtaani na kuanza kuchukua hatua kwa kila aliyeoonekana kuwafuatila.
 
Kuna mjadala unaendelea sasa Magic Fm radio wanasema Chadema waombe radhi kwa wananchi kwani wamekua wakilea vitendo kama hivi na kushabikia wananchi kujichukulia hatua mkononi!
 
wanasihasa ndo nini?attation ndo nini? hivi si muwe mnaandikia tu kiswahili?? shukle za kata hizi zimeleta mambo sana khaaaa..halafu manalaumu oooh mitihani ya NECTA migumu mtafaulu vipi kama hiki ndo kiingereza chenu...

Chadema hapo mate yanawatoka wanatamani angekuwepo mwakilishi wao ili waonekane wameongoza wananchi kuvunja sheria
 
Chadema toeni tamko kuunga mkono uvamizi huo na itisheni maandamano kwa nini polisi haitaki kuwapa raia watuhumiwa hao waonje nguvu ya umma!
 
Hii haihusiani na kutokuwa na imani na CCM. Ninavyofikiri mimi ni kwamba POLISI JAMII ya afande Mwema ndo ilivyoeleweka kwa watanzania.
 
Taarifa nilizonazo ni kwamba sababu za wananchi hao kutoka kijiji cha ITUNUNU umbali kama km 5-6 toka Mugumu mjini walifikia hatua hiyo baada ya kuona jeshi la polisi linaendelea kuhujumu jitihada zao za kukabiliana na uhalifu kijijini kwao na wilayani kwa ujumla. Kumekuwa na tabia ya polisi kuwaachia wahalifu pasipo kuwafikisha mahakamani ili wakakabiliane na tuhuma zinazowahusu, mara nyingi polisi wamegeuka kuwa ndio mahakimu na kumalizia kesi zote kituo cha polisi mugumu wakati matukio ya wizi, majeruhi na mauaji yakiendelea kila mara.

Katika tukio la jana kulitokea wizi kijijini ITUNUNU na katika tukio hilo watu wawili wakauawawa na hao wezi, na kama kawaida polisi walitaarifiwa na kwakuwa kuna watu waliokuwa wanahisiwa kwamba ndio wezi wakakamatwa. Kwa upande wa pili wananchi hao walijitokeza kwa wingi kufuatilia ng'ombe waliokuwa wameibiwa na kufanikiwa kuwakamata.Sasa wakati wanarudi nyumbani ndo wakapata taarifa kwamba wezi na wauaji wamekamatwa wako kituo cha polisi mugumu, ndipo wakaamua kupita hapo ili kuja kinachojiri na kutokana na kuchoshwa na vitendo vya uhalifu vinavyojirudia rudia kila mara na pasipo polisi kuchukua hatua zinazostahili ndipo baadhi yao wakataka wakabidhiwe watuhumiwa hao wa wizi na mauaji ili wawashughulikie wenyewe kwa kuwa polisi imeshindwa kufanya kazi yake ipasavyo.
Polisi kuona hivyo, ghafla tu bila hata kutoa tahadhari wakaanza kupiga risasi za moto bila mpangilio hali ikiyopelekea watu wengi kujeruhiwa na kuna taarifa ambazo hazijathibitishwa rasmi kwamba kuna watu watatu wamefariki katika mtafaruku huo. Kibaya zaidi polisi walianza kuzunguka mji mzima na kupiga watu hovyo hata wasiojua kinachoendelea ambao hawakuwepo eneo la kituo cha polisi. Watu walikuwa kwenye shughuli zao, wakavamiwa huko na polisi na kuanza kupigwa; kuanzia sokoni, stendi hadi mitaani kote watu walikuwa wanapigwa tu hovyohovyo, hii hali ni ngumu kuieleza lakini kwa hali iliyopo mugumu, wananchi hawana imani kabisa na jeshi la polisi.

Kwa jinsi hali ilivyo, jeshi la polisi linatakiwa kujipanga upya, watafute mbinu mpya za kukabiliana na uhalifu na zaidi sana watafute weledi wa kushughulikia malalamiko ya wananchi, lakini kwa utaratibu huu wa sasa wa polisi kujigeuza mahakama, na kibaya zaidi kuchukua fedha toka kwa wahalifu na kushindwa kuwafikisha mahakamani kwa kisigizio cha kukosekana kwa ushahidi, hili ni jambo ambalo lazima litazamwe upya na kwa umakini wa hali ya juu, na katika hili IGP Mwema ana kazi kubwa sana ya kubadili mtazamo na utendaji wa polisi.

Kwa mtazamo wangu kwa kuangalia matukio mbalimbali yanayotokea yakihusiana na jeshi la polisi kuwaua wananchi, kuwajeruhi na kuwapiga, ni dhahiri kuwa wananchi wamepoteza na wanaendelea kupoteza imani na jeshi la polisi, kuanzia tarime, arusha, mbarali, iringa, tabora na kila kona ya nchi hii polisi wanalalamikiwa, na katika hili JESHI LA POLISI NI LAZIMA WAJIVUE GAMBA!!
 
Ugomvi wa Polisi na raia unazidi kushamiri sana these days.... Kuna nini nyuma ya hii kitu???
 
Jamani kwa hili kweli wananchi walichokifanya si cha busara.Mimi nilikuwa safarini wilayani Serengeti nilifika eneo la tukio kituoni kulikuwa na askari wachache pia gari la polisi halikuwepo kituoni walikuwa kwenye msafara wa NW wa TAMISEMI Agrrey Mwanli.Ilibidi gari la polisi likatishe safari kwenye msafara wa NW lirudi kituoni kuja kuongeza nguvu kuwasambaratisha hao wananchi waliokuwa wamekivamia kituo. Hakika kwa jinsi wananchi walivyokuwa na jazba gari la polisi lingechelewa kwa dk kama kumi uharibifu mkubwa ungetokea
 
Back
Top Bottom