Kituo Cha Police Kilwaroad Chazingirwa Na Maji

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
55,881
29,255
Habarini Za Saizi Ndugu Wapendwa,,poleni Kwa Wote Ambao Mmepatwa Na Shurub Ya Mvua Leo Jijini Dar Es Salaam,,hakika Ni Siku Ambayo Haitasahaulika Kwa Mshangao Wa Watu,,yaliotokea,,,,leo Hii Kwa Masikitiko Makubwa Nikiwa Naendesha Gari Niliona Watu Wamekizingira Kituo Cha Police Cha Kilwa Nikahisi Usalama Umeshapotea Na Labda Wazee Wa Kazi Wameshahitimisha Sikuukuu Zao,,la Hasha Niliposhuka Nilikukuta Kituo Kizima Parking Za Nyuma Zimezingirwa Na Maji Huklu Wakuu Wakiwasiliana Na Radiocall Ndani Na Kuamua Walio Ndani Wabaki Ndani Walio Nje Wakapumzike,,hakika Ilinishtua Kuona Kituo Kikubwa Kama Kile Makandarasi Wanajenga Kama Wanavyojenga Vyoo Vya Mchambawima,,leo Hii Kila Mtu Amekuwa Akisikitika Kwa Matatizo Ya Foleni Yaliotokea Hakuna Hivi Sasa Kuna Watu Waliokuwa Barabarani Tangu Saa Kumi Na Mpaka Sasa Hawajafika Makwao,,je Wewe Waziri Chenge Unaona Matataizo Ya Ten Perc?????????si Mpaka Mungu Aje Anaweza Kuwaonyesha Kabla Ajaja Yeye Dhambi Mliokuwa Mkiwatendea Watanzania Na Jinsi Wanavyohangaika,hakika Hata Kama Si Wewe Basi Mjomba Mkeo Shangazi Yako Jirani Lazima Amepata Shuruba Ya Leo.........
Yetu Macho
Ahsanten
 
Mkuu Pdidy,
Mvua ya jana hapa Dar ilikua siyo ya kawaida, ilikua katika intensity ambayo inatokea mara chache sana.
Mwl. JKN Airport ilikua haitamaniki.
Kwa kifupi si jambo la mkandarasi au jambo la kulaumu watu hawa au wale... ni kwamba uwezo wetu hauturuhusu kujenga miundombinu ya kuweza kuhimili hali kama ile.
 
Mkuu Pdidy,
Mvua ya jana hapa Dar ilikua siyo ya kawaida, ilikua katika intensity ambayo inatokea mara chache sana.
Mwl. JKN Airport ilikua haitamaniki.
Kwa kifupi si jambo la mkandarasi au jambo la kulaumu watu hawa au wale... ni kwamba uwezo wetu hauturuhusu kujenga miundombinu ya kuweza kuhimili hali kama ile.

Hatuwezi kuhimili kujenga Mifereji ya chini kwa chini ya maji machafu lakini tunaweza kustahimili wezi wa Mabilioni ya dola!
Fedha pekee yake haileti maendeleo.
Ndiyo maana Saudi Arabia wenyefedha nyingi kuliko Dubai bado wanajikanyaga wakati Dubai inapiga hatua kubwa katika kila uwanja.
Matatizo tuliyo nayo hayatuumizi vichwa ndiyo maana hatujengi hoja za kuyatatua.
 
Kwanza naomba niwape pole wahanga (nikiwemo mimi mwenyewe na familia - maji yalijaa mpaka vyumbani,si utani). Lakini kusema kwamba eti mvua hizi sio za kumlaumu kandarasi (contractor) ni sawa lakini lawama lazima tuwape wahandisi (consultants)... Jamani, kama barabara tunazifanyia design ya drainage yake kwa kuangalia 25 year rains/flood records sasa haka kamvua ka mwanzo ka masika tunakaita eti ni janga na tunashindwa kuendesha magari (na hata kulala for cases like mine) halafu tunasema eti hatulaumu mtu ni NATURE, je yakitokea ya Msumbiji tutasemaje, "MWISHO WA DUNIA"?

Tukumbuke kwamba hata zikinyesha vuli zilizoshiba kidogo kuna maeneo kama (Muhimbili Primary, Al Haramain, Bibi Titi/Morogoro jct, Mandela road nk) ambapo maji lazima yajae.....

Bottom line is "Tunatakiwa kuangalia upya na kwa ufasaha mipango/miradi yetu ya kimaendeleo (ujenzi wa barabara, majengo nk) kama inavyotakiwa na sio kuacha vipengele flani kisa "Dubai hawafanyi hivyo"!!! Tumeshasahau kwamba Tanzania ni Tropical Country ambapo kuna what they call "Flash Rains" ambazo zinaweza zisiwe predictable.......

Hivyo kwa swala zima la mafuriko hapa Jijini, Mererani na sehemu nyingine kadha wa kadhaa hapa nchini sio chochote zaidi ya "UZEMBE na KUTOKUONA MBALI na KUDHARAU BASIC ENGINEERING PRINCIPLES - the more the area is developed, the lesser the natural percollation/infiltration resulting in posible massive/catastrophic surface runoff......

Naomba kuwakilisha.........
 
Tukio hili ni lakweli kwa sababu na mimi nililishuhudia,kituo kilikua kimezingirwa na maji,lakini nashindwa kujua Chenge ameingiaje hapa kwa sababu kituo cha kilwa road kilikuwepo miaka dahari iliyopita.Jamani muoneeni huruma chenge kwa mambo ambayo hajahusika kwani mzigo alionao ni hatari.
 
a.9784 upo sawa kwa hilo lakini tujikumbush yafuatayo:
1. Zamani kulikuwa na kamfereji uchwara kule nyuma ya Kilwa road polisi maeneo ya Keko Machungwa, siku hizi hebu pita uangalie kuna nini?
2. Ujenzi holela nao pia umechangia sababu imepunguza/kuziba zile njia za maji (same is applicable kule TMJ hospital na maeneo ya mikoroshoni)
3. Ujenzi wa barabara ya Kilwa (mpya by KAJIMA). Hapa kidogo pagumu sababu ukikumbuka kale kabarabara ketu ka zamani kalikuwa kidogo chini hivyo maji yalikuwa yanatiririka kuelekea maeneo ya karibu na kituo bila kudhuru kituo chetu.....

Sasa ukiweka yote hayo hapo ndipo pale niliposema ni kosa letu sisi Wahandisi (please note sio MoW - Chenge) kwa kuacha kufanya tathmini za muda mrefu katika swala zima la drainage. Hata hivyo, siwezi kusema kwamba MoW wamesamehewa kabisa kwa sababu kama Mhandisi atafanya matumbo lazima pale kwa Chenge kutakuwa na watalamu ambao wataangalia na kuhoji mapungufu hayo, so indirectly MoW wamo ndani.

Je kuhusu la uwanja wa Taifa nalo lina ubishi?? Tumeweka nyasi mpya lakini wanja lipo chini ukizingatia obstruction ya maji ambayo yalikuwa yanajaa pale kwenye wanja jipya... Tumelijenga jipya sasa maji haya tuyapeleke wapi?? Au itakuwa ni mvua inyeshe then tungoje maji yakauke kisha tutandaze soka??

Kubwa zaidi ni pale JNIA - Wanja letu la ndege - Duh, meni sana manake kule napo ni haya haya, pita ile njia ya nyuma ya uwanja (kunaitwa kipunguni ee?) wakati zinanyesha uone maji yanavyojaa... Sasa zamani kule nyuma ya uwanja kama unaelekea relini (kutokea Temeke) kulikuwa na matindiga (kiswahili yanaitwaje haya manake wengine wa bara jamani) ambapo siku hizi kuna nyumba kila pembe...

Hivyo ndugu yangu hata kama majengo/barabara zilikuwepo toka mwaka 47, siku hizi mengi yametokea na hivyo kuondoa ile natural dissipation ya rain water na hivyo kupelekea kuwa na mafuriko (rather mabwawa) wakati wa flash rains katika maeneo mengi ya Tanzania.

Naomba kuwakilisha............
 
Back
Top Bottom