Kituo cha kupoza Umeme cha Mpomvu kuipa Geita umeme wa Megawati 90

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,815
11,992
Uwepo wa kituo cha kupokea, kupoza na kusafirisha umeme mkubwa wa kilovoti 220/33 kutoka Bulyanuhlu hadi Mpomvu Geita sasa utaifanya Geita kupata umeme wa Megawati 90 wakati mahitaji yao kwa sasa ni Megawati 18.
geita 1.JPG
Kukamilika kwa kituo hiki kunaifanya Geita pia kuanza kupata umeme wa kutosha kwa shughuli za kiuchumi na za kijamii.

Hayo yamebainika baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kufanya uzinduzi wa kituo hicho Jumamosi, 15 Oktoba, 2022.

Hapo awali Mkoa wa Geita wenye wilaya tano ulikuwa ukipata umeme mdogo kutokea Shinyanga wa Megawati 4. Kutokana na ukuaji wa uchumi, umeme huo ulikuwa ni kikwazo kwa shughuli za kiuchumi hususani katika sekta ya madini.
geita 5.JPG
Pamoja na kuondoa tatizo la umeme mdogo ambapo awali maeneo ya Mkoa wa Geita ikiwemo Chato na Sengerema yalikuwa yakipata changamoto hiyo na kushindwa kufanya shughuli zake za kiuchumi kwa ufanisi, TANESCO ilikuwa inashindwa kuwapatia umeme wachimbaji wakubwa na wadogo wa madini kama vile Geita Gold Mines (GGM), Geita Gold Refinery na StamiGold.

Kwa sasa TANESCO inaweza kuwapelekea umeme wateja wakubwa na wadogo na tayari Shirika limesaini mkataba na Mgodi mkubwa wa Geita Gold Mines (GGM) na kukamilisha njia itakayopeleka umeme kwenye mgodi huu mkubwa.
GEITA 6.JPG

Rais Samia Suluhu Hassan akisikiliza maelezo kuhusu Kituo cha kupokea, kupooza na kusambaza umeme cha Mpomvu Geita tarehe 15 Oktoba, 2022.


Hatua hiyo itaongeza mapato kwa Shirika kwa kiasi cha shilingi bilioni 6 kwa mwezi na kupunguza gharama za uendeshaji kwa GGM kwa shilingi bilioni 4 kwa mwaka.

Migodi midogo itakayonufaika ni pamoja na maeneo ya Nyarugusu, Rwamgasa, Nyakangwe, Msasa, Iparamasa, Katente, Nyakafuru, Shenda na Mwamakiliga.

Vilevile, Rais Samia amezindua mradi wa kituo cha kupoza umeme cha Mpovu Geita ambapo mradi huo wenye sehemu tatu ambazo ni Njia ya kusafirishia umeme kutoka Bulyanhulu mpaka Geita yenye uwezo wa kilovoti 220 za umeme. Mitambo umba za kupoza umeme zenye uwezo wa kupitisha megawati 90 na Usambazaji umeme katika Wilaya ya Geita.
geita3.JPG

Rais Samia Hassan akikata utepe kuzindua Kituo cha kupokea, kupooza na kusambaza umeme cha Mpomvu Geita tarehe 15 Oktoba, 2022.


Katika hatua nyingine, Rais Samia amewasihi wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa kuwaambia: “Niwaombe wafanyakazi msivunjike moyo, najua huenda kinachopatikana ni tofauti na matokeo ya kazi mnayoifanya, lakini huko mbele mambo yakikaa sawa tutagawana kitakachopatikana.”

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Maharage Chande amesema uzinduzi wa kituo hiki cha Mpomvu utaondoa changamoto iliyokuwepo ya umeme mdogo pamoja na kushindwa kuwapelekea umeme wa uhakika wachimbaji wakubwa na wadogo wa madini.

Gharama zilizotumika kutekeleza Mradi huo ni jumla ya Dola Milioni 23 (zaidi ya Tsh. Bilioni 50.63) ambapo Serikali ya wa Tanzania imetoa Dola Milioni 3, BADEA na OFID (The Opec Fund for International Developement) Dola Milioni 10 kila mmoja.
GEITA7.JPG
 
Back
Top Bottom