Hivi Askofu Gwajima haoni hali ya mazingira ya kituo cha Kawe hasa kipindi hiki cha mvua?

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,566
Salaam Ndugu zangu,

Kijana wenu mfukunyuzi mtembezi sipendi kuacha kutia neno kila napoona jambo halijakaa sawa. Leo nikiwa kwenye harakati zangu nimepita maeneo ya kituo cha Kawe na kuona mambo ya ajabu kabisa katika kituo kikuu cha Mabasi cha eneo hilo.

Wakuu nafahamu kuwa mazingira ya vituo vingi nchini yana hali mbaya sana lakini nasikitishwa sana na Mbunge wa Kawe bwana Askofu Gwajima kutofanya jitihada zozote kuweka mazingira sawa katika mazingira ya kituo hicho. Miaka mitatu kituo hakijawahi kuboreshwa.

Kwa ufupi ni kwamba kituo cha Kawe kina madimbwi makubwa ya maji, uchafu uliokithiri sambamba na biashara ya chakula.

Sasa ndugu Askofu Gwajima najua kutupeleka Birmingham haiwezekani lakini hata kuweka vifusi vya mawe vizuri ili kuweka sawa stendi hii umeshindwa? Au ndo unasubiri uchaguzi ukaribie ili umwage vifusi uwaombe watu kura. Updates: Yanayojili Safari ya wanakawe kuelekea mji wa Birmingham Marekani

Tafadhali wewe na viongozi wengine wanaohusika tuboresheeni miundombinu pamoja na kuweka sawa sehemu za kuweka taka.


Siongei bila ushahidi tazameni wenyewe picha na video zifuatazo:



1684309888990.png

1684309935850.png

1684309972077.png


Note:
Hapo sio dampo ni Kawe Stendi. Haya nileteeni Gwajima tuone.
 
anadubiri hilo bwawa lijae, atalitumia kufanya usaili wa kwenda kusoma ubaharia marekani🤣
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom