Jamani wala tusishangae sana, hizi dini ambazo tumeziamini na kuzishikilia zimeletwa na wao, sisi tukawa watekelezaji tu. Huyu shetani ni wao, hayo matendo tuliyoambiwa ni mabaya ni wao walituaminisha hivyo. Sasa leo ukienda huko Ulaya hakuna mtu anakwenda kusali, makanisa mengi yamekua makumbusho, wao wanaendekeza hayo mambo ya kishetani ambayo walitukataza ndio wanayafuata na kuyaabudu kweli kweli. Niseme tu ukweli nchi ambazo bado zinamjali na kuamini Mungu yupo ni Africa peke yake. hao waliotuletea dini kwa kweli no one cares. Bora hata hao wachina ambao toka wameujua ulimwengu wao hawajua kanisa wala msikiti. Sasa na sisi tujiandae it is the matter of time, hawa hawa watakuja tena kuwa Mungu hayupo na tuliwadanya hivyo kuoana wanaume kwa wanaume, wanawake kwa wananke ni sawa, yatafika tu muda si mrefu