Kituko Makongo Juu, waweka msiba kumbe hajafariki

KITEKSORO

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2012
Posts
346
Reaction score
425
Jambo la ajabu limetendeka Makongo juu, mgonjwa kapelekwa hospitali Mwananyamala juzi akalazwa. Walioenda kumjulia hali jana asubuhi wakarudi wanalia kwamba mtu wetu kafariki. Taarifa zikasambaa ukawekwa msiba, maturubai, watu kibao tumelala msibani. Rambirambi zimechangwa.

Ajabu asubuhi hii aliyeenda hospitali kukamilisha taratibu za huko kaleta taarifa kuwa mgonjwa alikuwa hajafa, ila alihamishwa kitanda! Hivi ndo kila mtu kabaki mdomo wazi. Ndo tunaondoa maturubai na kurudisha makochi ndani.

My take: Tuwe makini, kabla ya kusambaza taarifa mtu kafa, tucomfirm kabisa na daktari na ikibidi ushuhudie mwili kabisa. Usumbufu mkubwa watu wamepata na itaathiri sana maisha katika familia ya mgonjwa.

Mungu aendelee kumponya. Amen.
 

na nyinyi mnaopokea taarifa kuhakiki ni jukumu lenu
 
Kuna utaratibu wa kimila wa kutangaza kifo.
Mwaka jana nilienda kijijini kwetu nikabahatika kukutana na msiba wa classmate wangu wa primary. Miongoni mwa watu watano wa mwazo kupokea taarifa za kifo chake Mimi nilikuwa mmoja wapo. Lakini kifo chake kilitangazwa baada ya saa mzima Mara baada ya kuita wazee wazoefu wa kimila na kuthibitisha kuwa kweli amefariki (kwakuwa hakufia hospital). Nilijifunza kitu. Hata mama Mzazi wa marehemu hakujua kama mwanae amefariki hadi confirmation ilipofanyika.
 
du poleni sana mkuu bila shaka waliotoa taarifa ni wanawake maana akili za wanawake wanazijua wao tu.
Itakuwa waliuliza huyu mgonjwa wetu yuko wapi?
Mgonjwa wa alilala kitanda cha pili yake aliwajibu..Huyu mbona atunae hapa!Wao kwa akili zao, wakakurupuka hadi nyumbani na vilio njia nzima....
Hii ilimtokea Baba wa jirani yangu na alitangaza msiba alikuwa mkewe,,,,
Ilituchukua mwaka mzima kuitafuta Aman kwenye Familia.....
 
Mkuu kukutana na msiba ni bahati ee!
Maana unasema ulibahatika kukutana na msiba wa classmate wako!
 
Hahaha...
Wazee wa ubwabwa kama kawaida bajeti ya leo ya maakuli ilikua juu ya wafiwa.
Sijui itakuaje leo!!!
Mmmmmmmm
Wacha nichekee bafuni[emoji87] [emoji87] [emoji87] [emoji87] [emoji87]
 
Kwa kweli tuwe makini hata mtaani kwetu hii ishu ulitokea waliokwenda kwa mgonjwa hawakumkuta pale kitandani wakarudi na vilio kumbe mgonjwa alikuwa ameenda kusafishwa kidonda
 
Watu wana stress na dawa

Sizonjemadawa
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…