Kituko kingine cha Chiku Ghalawa, Mkuu wa Mkoa Tanga!

Kituko kingine cha Chiku Ghalawa, Mkuu wa Mkoa Tanga!

matongo manawa

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2011
Posts
336
Reaction score
79
Katika hali isiyo ya kawaida mkuu mkoa wa Tanga Bi Chiku amewaamuru watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga kuhamia Wilayani kwa lazima huku kukiwa hakuna nyumba za kuishi.

Katika kuitikia amri hiyo mbayuwayu hao wengine wamehamia wodini na familia zao mfano manesi na wauguzi.

Kutokana amri hiyo baadhi ya watumishi wamekimbilia mahakamani kuweka zuio la mahakama mpaka kieleweke.

RC huyuhuyu alimsababisha mkuu wilaya ya Mkinga Mh. Rashid kuacha kwa kumwambia 'Chukua ofisi yako, siwezi kuingiliwa kwenye utendaji'.

Kama wafanyakazi watamshinda mahakamani, nadhani aliyemteua kwa vigezo maalumu itabidi ampige chini kutokana na kushindwa kufanya maamuzi mazuri ya kiuongozi.
 
Lisu akiwaambia hadi majaji hawajui kusoma hukumu mnashagaa,enyi ccm mlaaniwe na kizazi chenu na siku mkiondoka madarakani msirejee tena milele na woote semeni amen !
 
jk ,lazima azingatie vigezo vya msingi ktk kumpa m2 urc! na sio kuangalia jinsia ,bora ma rc wot waw wanaume weny busara
 
Rais Kikwete tafadhali mwekee gavana huyu Chiku. Utawapelekaje watu waishi mahali hakuna nyumba.
 
Tatizo ni nafasi hizo anawapa makada wa chama,wengi wao wakiwa hawana uwezo.
 
She is not the first to do that...nchi hii ina historia ya mambo ya kijinga kama hayo....operesheni vijiji vya ujamaa ni mfano hai.
 
Anawachukulia watumishi umma kama watwana nyumbani kwake,ubabe bila busara
Kwanini asimshawishi aliyemteua kwa vigezo vinavyotia kichefuchefu ajenge nyumba
za watumishi?

Ndomana ktk katiba mpya tunataka vyeo hivi vya kuangalia shepu viondolewe.Vyeo hivi
ni janga kwa Taifa imefikia huyu RC anaita watanzania wanaoingia Tanga kwa shughuli za
kiuchumi kuwa ni wahamiaji haramu.
 
Tatizo la kuteua mtu kushika wadhifa mkubwa katika utumishi wa umma bila kuzingatia uwezo na sifa stahiki, ila kwa kuangalia jinsia yake!
 
She is not the first to do that...nchi hii ina historia ya mambo ya kijinga kama hayo....operesheni vijiji vya ujamaa ni mfano hai.

of course wa kwanza kufanya alikuwa ni Mtume Nyerere na operesheni yake ya vijiji vya ujamaa.
 
Lisu akiwaambia hadi majaji hawajui kusoma hukumu mnashagaa,enyi ccm mlaaniwe na kizazi chenu na siku mkiondoka madarakani msirejee tena milele na woote semeni amen !

Mkuu wengine wameoa ni ukweni huko Chchm hiyo laana duh!
 
kwakweli huyu RC anakosea mbona Saidi Kalembo pamoja na kuwa mkorofi hakutoa agizo hilo!
 
Mimi kwanza nna allergy ( mzio ) na hawa watu Mkuu wa Mkoa & Mkuu wa Wilaya.....sipatani nao tu

Ndio maana huyu Mama RC alipokuja ofisini kwetu sikumsalimia na aliponisalimia " Hujambo " nliitikia kwa kichwa !
 
Ni mtendaji mzuri sana utakaaje mjini tanga Wakati kituo Chako cha kazi ni mkinga
 
kwa hili nampongeza huyu mama, uzembe namna hii upo sana tz, bwana mifugo anakaa mijini, wabunge hawakai sehemu zao za ubunge, kule mkinga sio kweli kama hakuna nyumba za kuishi, wakapangishe za watu binafsi waishi na wafanye kazi karibu na office zao
 
kwa hili nampongeza huyu mama, uzembe namna hii upo sana tz, bwana mifugo anakaa mijini, wabunge hawakai sehemu zao za ubunge, kule mkinga sio kweli kama hakuna nyumba za kuishi, wakapangishe za watu binafsi waishi na wafanye kazi karibu na office zao
Mkuu tufikirie kidogo,hiyo jiografia yamkinga
ni ngumu ofisi ziko porini nyumba za wenyeji wachache walio karibu ni za makuti,ofisi za halimashauri hazijakamilika kujengwa inasemekana zinaweza kamilika baada ya miaka minne kandarasi walipewa wachina na pesa imekata.
Mkuu wa mkoa amewaamuru watumishi wakae na wafanyie kazi madarasani,kioja
ni kwamba madarasa hayo hayana hata umeme,maswali ya kujiuliza:-

1.watafanyaje kazi bila computa?
2.Kulikuwa na haja gani ya kuanzisha wilaya mpya wakati serikali haina uwezo?
3.Ni nani mwenye jukumu la kuandaa makazi ya watumishi?

Nyongeza:kutokana na makao makuu yalipo ni rahisi kufika Tanga mjini kuliko kufika
Mkinga.Max weber aliwahi kuandika:-
"Bureaucrat some times are stupid,they send a set of television in place where
there is no electricity"

Ndiyo vioja vya watawala wetu,wao wanakaimu mikoa mfano RC Lindi alikuwa anakaimu
Dar,RC Tanga alikuwa anakaimu Moshi na inawezekana wao hawjui hata kutumia
Komputa,lkn hawa watumishi kazi zao zinategemea sana mitandao.

Ni aibu kuwa na watawala wa aina hii.
 
Back
Top Bottom