Kituko kingine cha Chiku Ghalawa, Mkuu wa Mkoa Tanga!

Watawala wameanzisha wilaya na mikoa mipya ili mahawara,watoto wao,marafiki na makada wa CCM wapate nafasi ya kugangaa njaa. Hivi mahitaji muhimu ya wananchi ni kuwa na watawala karibu ama huduma za msingi,maji,zahanati,barabara,shule na nishati ya umeme??
 
Katika hali isiyo ya kawaida mkuu mkoa wa Tanga Bi Chiku amewaamuru watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga kuhamia Wilayani kwa lazima huku kukiwa hakuna nyumba za kuishi.

Katika kuitikia amri hiyo mbayuwayu hao wengine wamehamia wodini na familia zao mfano manesi na wauguzi.

Kutokana amri hiyo baadhi ya watumishi wamekimbilia mahakamani kuweka zuio la mahakama mpaka kieleweke.

RC huyuhuyu alimsababisha mkuu wilaya ya Mkinga Mh. Rashid kuacha kwa kumwambia 'Chukua ofisi yako, siwezi kuingiliwa kwenye utendaji'.

Kama wafanyakazi watamshinda mahakamani, nadhani aliyemteua kwa vigezo maalumu itabidi ampige chini kutokana na kushindwa kufanya maamuzi mazuri ya kiuongozi.
Kwani wenyeji wa hiyo Wilaya wanaishi wapi?
 
Back
Top Bottom