Red Giant
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 15,658
- 20,889
Tanzania imebarikiwa kila kitu kinachofaa kwa kilimo cha umwagiliaji. Tuna ardhi ya kutosha kabisa. Nchi yetu ina eneo kubwa la kilomita za mraba 900,000+ . Wanasema tuna eneo la hekari milioni kama 30 zinazofaa kwa umwagiliaji lakini eneo linalomwagiliwa halifiki hata 1m.
Maji, Tanzania ni moja ya nchi yenye maji kwa wingi duniani(surface fresh water). Ziwa Tanganyika lina kama asilimia 16 ya surface fresh water yote duniani. Tanzania inamiliki 45% ya ziwa hilo. Ziwa nyasa lina karibu asilimia 6 ya maji yote safi yaliyopo juu duniani. Haya ni maji mengi sana. Hapo bado hatujazungumzia maziwa yenye maji machache kama Victoria, Rukwa na mito mingi ambayo huishia baharini. Pengine kuna changamoto kutoa maji kwenye maziwa ya bonde la ufa lakini ni ishu inayowezekana.
Kwanini basi hili suala haliendelezwi Tanzania? Ni ajira ngapi zinaweza tengenezwa ukijenga irrigation scheme ya ekari 1m?
Siku moja nilitembelea irrigation scheme ya Kapunga mbeya, ni kubwa nilishangaa sana na ile ni Hekta sijui ni ekari kama 7,000 hivi. Wakati wa kilimo watu wanajaa vibaya mno eneo lile, ajira za kutosha. Nasikia hii ilijengwa na wajapan, serikali yetu hii sidhani kama imewahi kujenga Irrigation scheme.
Nyie wadau mnasemaje, kwanini nchi kilimo cha umwagiliaji hakiendelezwi na hali kinaonyesha kuwa ni kitu chenye faida sana? Au ndiyo ile in abundance of water the fool is thirsty!!?