Kitu gani huwezi tembea bila kuwa nacho mfukoni, kwenye mavazi uliyovaa?

Hayo mengine tunayoyajadili hapa ni bhlah blah tu, ila la huyo mkaanga chapati aliyekueleza:....'kijana handsome namna hiyo unavuta sigara, si uache tu?'..

Alikupatia ushauri mwepesi lakini umebeba ujumbe mzito sana na alitumia jicho la tatu kuona future yako ilivyo hatarini.

Nimezika wazazi wangu wawili wavuta sigara kwa maradhi yenye kufanana yaliyopelekea vifo vyao.

Wakati ninawauguza nilipambana na maswali ya madaktari yenye kufanana pia:..'hivi huyu mzee huwa anavuta sigara?'...

Upo kijana unavuta unasisimka unaona raha, lakini maradhi yatokanayo na moshi wa tumbaku hayawekwi bayana ninadhani kwa sababu za kibiashara!

Tatizo jingine litokanalo na sigara ni uteja wa uraibu upatikanao katika tumbaku, maana hata ninavyokushauri hivi sasa ukashituka na kuamua kuacha utapata tabu sana kujinasua.

Ni suala la uamzi mgumu sana kuacha, nnakushauri amua sasa.
 
Smartphone yangu nipo nayo 24/7 mpaka bafuni naingia nayo. Hata nikilala nikistuka usiku cha kwanza lazma niishike ndio niamke sikumbuki ni lini ilishawahi kua mbali na mimi kwa umbali wa walau mita mbili sikumbuki kabisa.
 
Piga ua kutembea bila Mashine/Gegedio? Aisee.... Ni ngumu kwangu. Piga ua lazima niwe na ukuni kwenye suruali au kaptula napotoka.
sijaelewa hata umetaja vitu gani mkuu,unaweza kuvunja vunja hiyzo kauli into simple kauli?
 
Pesa kwanzia buku kuendelea earphones na sunglasses
haijawahi kukutokea siku huna hata 1000, huwa hutoki? na hizi hela mnazosema hamuwezi kutoka bila kuwa nazo huwa ni mnakua na hard paper au mnakua nazo soft money nikimaanisha hela zinakua kwenye simu? kwa mfano ledada hutoki bila buku na kuendelea hii buku inakua kwenye simu au kwenye pochi?
 
Mimi hivi vifuatavyo huwa siviachi :

1. Mswaki wa mti (Ile midogo midogo).
2. Tester
3. Pakiti ya Viwembe
4. Kalamu

Ahsanteni.
kwa matumizi gani mkuu hasa hii no.3 pakti za wembe huwa unaenda fanyia nini?
 
Back
Top Bottom