Jinsi Tony Robbins alivyoweza kutengeneza zaidi ya Dola Milioni 600 bila kuwa na cheti chochote

Seif Mselem

JF-Expert Member
Oct 16, 2023
257
441
Kama Umekuwa ukijiuliza ni Jinsi gani watu Wanaweza kutengeneza PESA Nyingi bila hata ya Kuwa na Cheti Kimoja basi.

Makala hii ya Leo ni DHAHABU Kwako kwasababu itaenda kukuonesha Utofauti Uliopo kati ya Mtu mwenye Cheti na asiye na cheti ila kabla Sijakwambia naomba Kwanza nikupe hii Story Fupi ya huyu Mtu anaitwa “Tony Robbins”

Kama Hufahamu tu Tony Robbins ni Mwandishi wa Kimarekani, Coach na Motivational Speaker aliyeweza Kuwasadia zaidi ya watu Millioni 50 kutoka kwenye Changamoto mbalimbali za Maisha yao ikiwemo:

Uvutaji sigara
Unywaji wa Pombe
Utumiaji wa Madawa ya Kulevya n.k

Vile Vile ni mtu Pekee anayeweza kutengeneza zaidi ya US Dolla 80 Millioni kila mwaka Kupitia Seminars, Podcast na Kuuza Vitabu vyake. "Amewezaje Sasa Kutengeneza Pesa nyingi Kiasi Hicho?"

(Unaweza Kujiuliza)!

Okay Vizuri, Ili uweze Kunielewa Vizuri ngoja Nikurudishe nyuma Kidogo miaka ya 80’s wakati Tony anaanza Kujifunza Career yake alianza kwa Kujifunza kitu Kimoja kinaitwa “Neuro-Linguistic Programming (NLP)”

Kwa Ufupi Tu NLP ni inahusu kujifunza Jinsi gani Mawazo ya mtu yana Athiri Tabia zake. Yaani unajifunza ni Jinsi gani Ubongo una tafsiri Signals Inazopokea na Jinsi gani tafsiri ya hizo Taarifa kwenye Ubongo ina affect kile Mtu anachokuwa anakifanya kwenye Maisha halisi.

Na Ubongo unafanya hivyo kwa Kutumia “Linguistic Language” kwahiyo Tony alienda Kujifunza huu Ujuzi na

Alikuwa amejiunga Kusoma hiyo Course kwa Miezi 6 tu… na baada ya Siku chache akatokea Kulipenda hilo Somo la NLP.

Kwasababu alilipenda Haikuchukua muda akawa Amejifunza na Kuelewa vitu vingi kwa Muda mfupi na hapo hapo Tony akataka Kuanza kuwasaidia watu.

Siku moja Usiku alipokuwa Akienda kuwasaidia Watu mtaani, trainer wake Akamwambia “You can’t go help people Because you’re NOT Certified yet”. Yaani kwa Lugha yetu ya Kibongo ni kwamba, “Huwezi kwenda Kuwasaidia watu Kwasababu bado huna Cheti”

Tony akamjibu kwa Mshangao…

“Certified? I know how to help People. Let’s go help!”

Akiwa ana Maanisha kwamba “Cheti? Najua jinsi ya Kusaidia watu. Twende Tukawasaidie”

Jamaa akatoka zake kwa Kujiamini nje ya Hostel alizokuwa anaishi kisha akaingaia Mtaani kwenye Migahawa ya Karibu. Akaanza Kusaidia watu. Unajua Nini Kilitokea baada ya Hapo?

Hahahaaaa. Yeah, uko Sahihi. Alifukuzwa kujifunza hiyo Program kwasababu… Alikuwa anawafundisha watu huku akiwa hana Cheti!

Unajua nini Kilitokea? Tony aliondoka pale Bila cheti na akaenda Kufundisha kile alichokuwa anakijua kitawapa watu Matokeo na hadi hapa Ninapoandika tayari ameshawasaidia zaidi ya Watu Millioni 50 kupitia Neuro-Linguistic Programming (NLP)!

Na Baadhi ya watu wakubwa Aliyoweza kuwasaidia ni Pamoja na Leonardo DiCaprio, Mother Teresa, Nelson Mandela, Bill Clinton, Serena Williams Opray Winfrey n.k

Na Ameweza kufanya yote hayo Bila ya kuwa na CHETI Chochote Juu ya kile anachofundisha!

Sasa Mselem, Kwanini Unanambia yote Haya?

Yeah Bora Umeuliza…

Ukweli ni kwamba…

Watu wengi kwenye Maisha wamekuwa wakiaminishwa kwamba Huwezi kufanya kitu chchote kile bila kuwa na Chet

Na ndio maana Rundo la watu kila Siku wana songamana Vyuoni kwenda kutafuta vyeti. Sio kwamba hawajui kufanya vitu ila ni kwasababu ameaminishwa ili uweze kufanya kazi flani basi Lazima uwe na Cheti.

Haiko hivyo wala Haifananii na Hivyo kitu pekee unachotakiwa kuwa nacho ni UJUZI wa Kufanya unachotaka Kukifanya ili uwasaidie watu.

Ujuzi ukiutumia kuwasaidia watu, Utakupa kitu kinaitwa RESULTS!

Au matokeo na matokeo ndio CHETI Chako (Your Results are Your Certification)

Kama umeweza Kutengeneza mwili wako kwa Kufanya Seti flani ya Mazoezi… Unadhani unahitaji Cheti kutoka Gym X ili Umsadie mtu mwingine apate Matokeo kama yako? Jibu ni HAPANA kwahiyo kwenye haya Maisha uhitaji kuwa na Cheti ili uweze kusaidia watu unahitaji kuwa na “PROVEN Way” ya Kupata matokeo ambayo Mtu mwingine akiitumia pia atapata kile ulichokipata Wewe.

As long as kile Unachompa mtu mwingine Akitumie kinafanya Kazi…Mzee wewe tayari ni “EXPERT”. Wewe Jiulize…

Watu wangapi hapa BONGO wanawasaidia watu na Kupata matokeo wanayotaka Ikiwa hawana hata Vyeti vya Kile wanachofundisha?

Wako wengi Mno…

Brother Joel Nanauka anafundisha watu Vitu vingi na hana Cheti chochote kwenye hivyo Vitu

Chris Mauki anafundisha watu kuhusu Mahusiano na hana Cheti Chochote kwenye Mahusiano

Kwahiyo mzee uhitaji kuwa na Cheti ili Usaidie watu. Otherwise uwe unataka kuwa Daktari au Mwanasheria

Ila kama kweli Unataka kuwa Mjasiriamali basi. Be REALLY GOOD at What you do and FOCUS on Getting People Results!

Mengine mwachie Mwalimu wa Mathee. Uwe na Asubuhi Njema. Gracias…

By the way. Nilitaka Kusahau kama una Maoni au Mawazo juu ya Hili Somo La Leo Basi Nafasi ya Comments iko wazi. Karibu tu Discuss.

Seif Mselem
 
Uwezo unakuwezesha kung'amua maarifa na kuyatumia Ila cheti ni uthibitisho kuwa umepitia mafunzo kikamilifu na kufaulu pasipo kujali ufaulu wala "uwezo binafsi"

Hivyo bhasi, katika story ya Tony tunaona

1. Aligundua umuhimu wa elimu ndio maana akaenda kupitia mafunzo rasmi

2. Alikuwa hana ustahimilivu na uvumilivu

3. Alikuwa na ari, uwezo binafsi mkubwa maana mtu ambaye ana uwezo mdogo ni ngumu kujua kuwa "hiki kitu kinatosha"

Mwisho wa siku, angevumilia na kupata cheti bado angeweza kufanikisha yote aliyoyafanikisha maana cheti sio kikwazo cha mtu kufanikiwa

Hata huyo Chris Mauki bado ni mkufunzi wa chuo

Joel nnanauka nae ni msomaji mzuri wa vitabu ambavyo vimeandikwa na experts wa fields anazopenda kuziongelea.. Mara nyingi anatafsiri tu

Mwisho wa siku cheti ni uthibitisho sio pass ya kuwa na exceptional ability lakini kikubwa zaidi ni kuitafuta ELIMU, iwe nje au ndani ya mfumo
 
Huyo Chris Mauni bado ni mkufunzi wa chuo

Joel nnanauka nae ni msomaji mzuri wa vitabu ambavyo vimeandikwa na experts wa fields anazopenda kuziongelea.. Mara nyingi anatafsiri tu

Mwisho wa siku cheti ni uthibitisho sio pass ya kuwa na exceptional ability lakini kikubwa zaidi ni kuitafuta ELIMU, iwe nje au ndani ya mfumo
Njia au codes za watu kupata utajri huwa mara zote ni siri,wanachokueleza wao jinsi walivyo chomoka ni kukuzuga tu ili uone kuwa ni njia rahisi,lakini ukweli sio rahisi hivyo watu wanavyowaza...
 
Uwezo unakuwezesha kung'amua maarifa na kuyatumia Ila cheti ni uthibitisho kuwa umepitia mafunzo kikamilifu na kufaulu pasipo kujali ufaulu wala "uwezo binafsi"

Hivyo bhasi, katika story ya Tony tunaona

1. Aligundua umuhimu wa elimu ndio maana akaenda kupitia mafunzo rasmi

2. Alikuwa hana ustahimilivu na uvumilivu

3. Alikuwa na ari, uwezo binafsi mkubwa maana mtu ambaye ana uwezo mdogo ni ngumu kujua kuwa "hiki kitu kinatosha"

Mwisho wa siku, angevumilia na kupata cheti bado angeweza kufanikisha yote aliyoyafanikisha maana cheti sio kikwazo cha mtu kufanikiwa

Hata huyo Chris Mauki bado ni mkufunzi wa chuo

Joel nnanauka nae ni msomaji mzuri wa vitabu ambavyo vimeandikwa na experts wa fields anazopenda kuziongelea.. Mara nyingi anatafsiri tu

Mwisho wa siku cheti ni uthibitisho sio pass ya kuwa na exceptional ability lakini kikubwa zaidi ni kuitafuta ELIMU, iwe nje au ndani ya mfumo
Uko Sahihi Brother, Kitu cha Muhimu ni MAARIFA Pekee.

Sema Nikuulize Swali?..

Cheti cha Nini kama Mtu unaweza Kufanya Kitu kwa Ufasaha na Kupata Matokeo?..
 
Njia au codes za watu kupata utajri huwa mara zote ni siri,wanachokueleza wao jinsi walivyo chomoka ni kukuzuga tu ili uone kuwa ni njia rahisi,lakini ukweli sio rahisi hivyo watu wanavywaza...
 
Uko Sahihi Brother, Kitu cha Muhimu ni MAARIFA Pekee.

Sema Nikuulize Swali?..

Cheti cha Nini kama Mtu unaweza Kufanya Kitu kwa Ufasaha na Kupata Matokeo?..

Hakina umuhimu sana Ila ukipitia mafunzo rasmi lazma utafundishwa vitu vingi zaidi ikiwemo pia ethics.
Pia cheti ni uthibitisho kuwa umepitia mafunzo kikamilifu na hivyo kutumika kama moja ya qualification

Imagine dunia ya bila cheti, watu wangetumia kipimo kipi kujua kuwa mtu flani kaiva kwenye profession flani
 
Uwezo unakuwezesha kung'amua maarifa na kuyatumia Ila cheti ni uthibitisho kuwa umepitia mafunzo kikamilifu na kufaulu pasipo kujali ufaulu wala "uwezo binafsi"

Hivyo bhasi, katika story ya Tony tunaona

1. Aligundua umuhimu wa elimu ndio maana akaenda kupitia mafunzo rasmi

2. Alikuwa hana ustahimilivu na uvumilivu

3. Alikuwa na ari, uwezo binafsi mkubwa maana mtu ambaye ana uwezo mdogo ni ngumu kujua kuwa "hiki kitu kinatosha"

Mwisho wa siku, angevumilia na kupata cheti bado angeweza kufanikisha yote aliyoyafanikisha maana cheti sio kikwazo cha mtu kufanikiwa

Hata huyo Chris Mauki bado ni mkufunzi wa chuo

Joel nnanauka nae ni msomaji mzuri wa vitabu ambavyo vimeandikwa na experts wa fields anazopenda kuziongelea.. Mara nyingi anatafsiri tu

Mwisho wa siku cheti ni uthibitisho sio pass ya kuwa na exceptional ability lakini kikubwa zaidi ni kuitafuta ELIMU, iwe nje au ndani ya mfumo
Raha ya kusoma na kupata cheti ndio hii confidence and facts
 
Hakina umuhimu sana Ila ukipitia mafunzo rasmi lazma utafundishwa vitu vingi zaidi ikiwemo pia ethics.
Pia cheti ni uthibitisho kuwa umepitia mafunzo kikamilifu na hivyo kutumika kama moja ya qualification

Imagine dunia ya bila cheti, watu wangetumia kipimo kipi kujua kuwa mtu flani kaiva kwenye profession flani
Nakuuliza Swali La Mwisho...

Kwanini wengi Tunashindwa Kuvifanya kwa Vitendo Vitu Tulivyosoma Chuo?..
 
Simple, elimu yetu imeegemea kwenye kutoa maarifa na sio ujuzi,

Mbaya zaidi implementation yoyote hutegemea skill set hasa zile soft skills ambazo hatufundishwi darasani

Pia kwa experience yangu binafsi. Bachelor degree ipo too general ilhali kwenye field kinachohitajika ni specific expertise

Mfano mtu anasoma Business Administration, atajifunza accounts, marketing, procurement, public administration etc

Sasa imagine mtu kama huyu atatoa wapi muda wa kufocus kwenye specific field na hii ndio sababu, wengi wetu huwa tunajitafuta tukishaingia makazini ili kupata area of expertise
 
Ila Si Anapewa CHETI Kuthibitisha Anajua Alichokisome?..

(Kwa Maneno yako Sasa)!
 
Hatubishani, tunaelekezana...

Unajua waigizaji wa nchi kama Korea au USA, wengi wana vyeti vya uigizaji Ila wanaotoboa na kuwa mega stars ni wachache sana na hapo ndipo experience, exceptional talent, passion na bahati huja.

Kwa hiyo kupewa cheti si sawa na kupewa grammy awards, moja kinathibitisha umepitia mafunzo na umefikia standard inayohitajika na kingine kinakutuza kwa "outstanding peformance"

Sikatai kuwa elimu yetu ina gaps Ila haimaanishi ni useless au haimuandai mtu kuwa mtu fulani. Kwa sisi tuliosomea st kayumba tunalielewa zaidi, kuna nafasi yako katika kila kitu unachokifanya hivyo, ni jukumu lako kuitumia elimu kufanikisha unachotaka na sio kuitegemea elimu kukupatia kila unachokiwaza
 
Anyway... Nimekupata Kaka.

By the way... Nimefurahi Unajua Vitu vingi na I Hope Hujajifunza Shule vyote.
 
Kufanya chochote waweza tajirika

UNatakiwa. Kujiuliza swali moja tu je wateja wapo na Nina uwezo.wa kuwapata?
Ujasiliamali huanziii kujiuliza kuwa mtaji ninao? Mtaji waweza kopa nk baada ya kupata majibu ya maswali hayo mawili kwanza
 
Back
Top Bottom