Kitu gani hutokea hadi pesa kupanda au kushuka thamani?

Mohamedy cadinaly

JF-Expert Member
Apr 24, 2012
2,449
2,238
Habari wanajamvi kama kichwa cha habari kinavyoonyesha ningependa kwa yoyote ufahamu wa hili jambo ktk nukta zifuatazo

1. ni kwa vipi pesa ya nchi inaweza kushuka thamani ama kupanda thamani.

2. Ni vitu gani hupekea pesa kushuka thamani

3.Na pindi pale pesa inaposhuka thamani je kuna uwezekano Wa kupanda tena thamani? Na kama inawezekana ni njia gani zinaweza kutumika kuipandisha thamani tena

Naomba kuwasilisha
 
Kushuka kwa thamani ya shilingi kunaweza kukawa kwa (i)shilingi ya ndani yenyewe hasa kutokana na inflation yaani bidhaa kupanda thamani,lakini pia nchi kuamua kushusha thamani ya shilingi yake yenyewe (ii) kushuka kwa thamani ya Shilingi kwakulingalisha na dolar.
(1)Kushuka kwa thamani kwa sh ndani ya nchi.
Bidhaa zinapopanda thamani tafsiri yake ni kwamba tutahitaji pesa nyingi kununua vitu kidogo,hapo tunasema pesa baina thamani kiuchumi huita inflation.
Chanzo cha inflation kinaweza kua ni kushuka kwa uzalishaji aidha mashambani ama viwandani.
Kwa upande wa viwandani chukua mfano wa sukari juzi sukari ilipanda baada sana yakuadimika kutokana na viwanda kufungwa. Na kwa upande wa mashambani tizama bei ya vyakula pindi kutokeapo ukame bei ya vyaka hupanda sana.
Lakini pia sera mbovu zakiuchumi hasa BOT wanapo print pesa nyingi na kuziingiza kwenye mzunguko pia husababisha thamani ya sh kushuka.
Nchi kuamua kushusha thamani ya shilingi yake yenyewe mfano mzuri ni china mara kadhaa huamua kushusha thamani ya shilingi yake.Ifahamike kwamba kwa nchi zenye viwanda na uzalishaji mkubwa kushuka kwa thamani ya shilingi wakati mwingine ni faida kwao kwani huchochea uuzwaji wa bidhaa nje ya nchi huku ikidhoofisha uingizwaji wa bidhaa ndani ya nchi.
(2)Kushuka kwa thamani ya shilingi kulinganisha na Dolar.
Kama tujuavyo dola huhitajika kwaajili ya manunuzi nje ya nchi.Kama hifadhi ya dolar zilizopo ndani ya nchi ni chache kuliko mahitaji yake yaani kutosheleza mahitaji ya manunuzi yanayo hitajika nje lazima tsh itashuka thamani against dolar.
Ilishawahi tokea Dola ziliadimika kiasi chakuvuruga safari za watu.Wengine hulazimika hata kuongeza kidau wenyewe ili tu waweze kwenda na ratiba zao.
Lakini pia pia Dolar yenyewe kuimarika thamani yake mfano mzuri ni sasa ambapo tunaona nchi nyingi shilingi zao zimeshuka thamani ukilinganisha na Dolar kutokana na dolar yenyewe thamani yake kuimarika.
 
Asante Mkuu kidogo ameanza kunipa mwanga
 
Fedha Ni bidhaa ambayo kiujumla hutumika katikati ya miamala mingine, (kwa maana kwamba unatafuta fedha ili kuhifadhi nguvu yako ya kimanunuzi, manunuzi tunayafanya pale matamanio yetu yanapoizidi thamani fedha tunayomiliki, kwa mfano:- unamiliki tsh 20,000/=, sokoni Kuna kiatu kinauzwa tsh 20,000/=, matamanio ya kiatu yanapoizidi thamani fedha ndipo unapoamua kutoa fedha iliyopoteza thamani ili upate kiatu. Na thamani ya fedha ipo kwenye upatikanaji wake!, fedha inapokuwa nyingi kwenye mzunguko thamani yake hushuka Na ndipo hapo fedha nyingi hutumika kununua mahitaji kidogo, Na fedha inapopungua kwenye mzunguko thamani yake hupanda Na hapo fedha kidogo hutumika kununua bidhaa nyingi. Kitu kinachotumika kuthibiti thamani ya fedha kwenye mzunguko Ni sera za kifedha za benki kuu (monetary policy)(kwa mfano:-RIBA), Na sera za kibajeti(fiscal policy), riba inapopanda wafanyabiashara wanapunguza kukopa Na kuwekeza, pia serikali inapoongeza makusanyo yakodi hivyo fedha kwenye mzunguko/kupunguza matumizi, riba ikishuka wafanyabiasha hukopa zaidi na/au serikali ikipunguza kodi kodi/kuongeza manunuzi fedha huongezeka kwenye mzunguko hivyo thamani yake hushuka!. Hii Ni kwa mzunguko wa ndani.
Kwa mzunguko wa nj'e fedha huuzwa dhidi ya fedha ya nchi nyingine kutegemeana Na mahitaji. Tunapomiliki (kwa mfano US dollar) nyingi baada ya kuuza bidhaa zetu nj'e mahitaji yetu kwa US dollar hupungua hivyo thamani ya fedha yetu hupanda dhidi ya US dollar , lakini tunaponunua bidhaa nyingi kutoka nj'e mahitaji yetu kwa US dollar huongezeka hivyo thamani yake hupanda dhidi ya fedha yetu, Na kinyume chake Ni hivyohivyo!. Wenye ujuzi zaidi wataongezea/kosoa nipopungua/kosea!, Nawasilisha.
 
Mkuu hapa umemaliza kila kitu hakuna hata haja ya mm kuongea tena
 
Asante mkuu kwa maelezo mazur nazidi kupata mwanga
 
Kuna kipind nliwah kuwaza kama pesa ziachapishwa kwnn serikali ic chape nyingi itugawie wananchi tusahau umasikini
 
Jaman Mungu akubariki Sana, kwa jinsi ulivyoelezea utafikiri umelipwa, Yan kila mtu ameshangazwa kwa jinsi ulivyojituma hapa, Mama yako anajivunia kupata mtoto Kama wewe, hata Kula Leo sili kabisa kwasabu yako wewe
 
Kuna kipind nliwah kuwaza kama pesa ziachapishwa kwnn serikali ic chape nyingi itugawie wananchi tusahau umasikini
Serikali ikichapisha fedha nyingi thamani yake hushuka hivyo utatumia lundo kubwa kununua bidhaa chache!, rejea Congo ya Mobutu, Mugabe Na Somaliland (tofauti Na Somalia), pia umaskini hauondokani kwa wewe kumiliki fedha nyingi bali Ni kupata huduma zote za kiuchumi/kijamii Kama vile elimu bora, afya, ajira, maji Safi Na Salama nk. Kwa gharama naafuu!.
 
Kushuka kwa thamani ya shilingi kunaweza kukawa kwa (i)shilingi ya ndani yenyewe hasa kutokana na inflation yaani bidhaa kupanda thamani,lakini pia nchi kuamua kushusha thamani ya shilingi yake yenyewe (ii) kushuka kwa thamani ya Shilingi kwakulingalisha na dolar.
(1)Kushuka kwa thamani kwa sh ndani ya nchi.
Bidhaa zinapopanda thamani tafsiri yake ni kwamba tutahitaji pesa nyingi kununua vitu kidogo,hapo tunasema pesa baina thamani kiuchumi huita inflation.
Chanzo cha inflation kinaweza kua ni kushuka kwa uzalishaji aidha mashambani ama viwandani.
Kwa upande wa viwandani chukua mfano wa sukari juzi sukari ilipanda baada sana yakuadimika kutokana na viwanda kufungwa. Na kwa upande wa mashambani tizama bei ya vyakula pindi kutokeapo ukame bei ya vyaka hupanda sana.
Lakini pia sera mbovu zakiuchumi hasa BOT wanapo print pesa nyingi na kuziingiza kwenye mzunguko pia husababisha thamani ya sh kushuka.
Nchi kuamua kushusha thamani ya shilingi yake yenyewe mfano mzuri ni china mara kadhaa huamua kushusha thamani ya shilingi yake.Ifahamike kwamba kwa nchi zenye viwanda na uzalishaji mkubwa kushuka kwa thamani ya shilingi wakati mwingine ni faida kwao kwani huchochea uuzwaji wa bidhaa nje ya nchi huku ikidhoofisha uingizwaji wa bidhaa ndani ya nchi.
(2)Kushuka kwa thamani ya shilingi kulinganisha na Dolar.
Kama tujuavyo dola huhitajika kwaajili ya manunuzi nje ya nchi.Kama hifadhi ya dolar zilizopo ndani ya nchi ni chache kuliko mahitaji yake yaani kutosheleza mahitaji ya manunuzi yanayo hitajika nje lazima tsh itashuka thamani against dolar.
Ilishawahi tokea Dola ziliadimika kiasi chakuvuruga safari za watu.Wengine hulazimika hata kuongeza kidau wenyewe ili tu waweze kwenda na ratiba zao.
Lakini pia pia Dolar yenyewe kuimarika thamani yake mfano mzuri ni sasa ambapo tunaona nchi nyingi shilingi zao zimeshuka thamani ukilinganisha na Dolar kutokana na dolar yenyewe thamani yake kuimarika.

Fedha Ni bidhaa ambayo kiujumla hutumika katikati ya miamala mingine, (kwa maana kwamba unatafuta fedha ili kuhifadhi nguvu yako ya kimanunuzi, manunuzi tunayafanya pale matamanio yetu yanapoizidi thamani fedha tunayomiliki, kwa mfano:- unamiliki tsh 20,000/=, sokoni Kuna kiatu kinauzwa tsh 20,000/=, matamanio ya kiatu yanapoizidi thamani fedha ndipo unapoamua kutoa fedha iliyopoteza thamani ili upate kiatu. Na thamani ya fedha ipo kwenye upatikanaji wake!, fedha inapokuwa nyingi kwenye mzunguko thamani yake hushuka Na ndipo hapo fedha nyingi hutumika kununua mahitaji kidogo, Na fedha inapopungua kwenye mzunguko thamani yake hupanda Na hapo fedha kidogo hutumika kununua bidhaa nyingi. Kitu kinachotumika kuthibiti thamani ya fedha kwenye mzunguko Ni sera za kifedha za benki kuu (monetary policy)(kwa mfano:-RIBA), Na sera za kibajeti(fiscal policy), riba inapopanda wafanyabiashara wanapunguza kukopa Na kuwekeza, pia serikali inapoongeza makusanyo yakodi hivyo fedha kwenye mzunguko/kupunguza matumizi, riba ikishuka wafanyabiasha hukopa zaidi na/au serikali ikipunguza kodi kodi/kuongeza manunuzi fedha huongezeka kwenye mzunguko hivyo thamani yake hushuka!. Hii Ni kwa mzunguko wa ndani.
Kwa mzunguko wa nj'e fedha huuzwa dhidi ya fedha ya nchi nyingine kutegemeana Na mahitaji. Tunapomiliki (kwa mfano US dollar) nyingi baada ya kuuza bidhaa zetu nj'e mahitaji yetu kwa US dollar hupungua hivyo thamani ya fedha yetu hupanda dhidi ya US dollar , lakini tunaponunua bidhaa nyingi kutoka nj'e mahitaji yetu kwa US dollar huongezeka hivyo thamani yake hupanda dhidi ya fedha yetu, Na kinyume chake Ni hivyohivyo!. Wenye ujuzi zaidi wataongezea/kosoa nipopungua/kosea!, Nawasilisha.

Shukran tena kwenu wakuu, kwa kueleza vzr ila hebu nielimishini hapa zaidi

Je, ni nan anahusika hasa na kupanga thamani pale hela moja inaposhuka thamani dhidi ya mwenzie? mfano dollar moja iwe labda ni sh. 2000, euro iwe ni sawa labda na 3000. Je, ni watu wenyiwe wanavyoamua kupandisha bei au inakuaje?
 
Kuna namna mbili zinazohusiana na thamani ya fedha moja dhidi ya nyingine:-
1. "Depreciation"-Hii hutokea pale thamani ya fedha inaposhuka kutokana na nguvu ya uvutano Kati ya ugavi Na mahitaji (supply and demand) sokoni, kinyume chake Ni "Appreciation".
2. "Devaluation"-Hii huokea pale serikali kupitia benki kuu unapoamua kupunguza yenyewe thamani ya fedha kwa kupanga "exchange rate" dhidi ya fedha za nchi nyingine, hii mbinu hutumika zaidi Na nchi zinazokua kiviwanda kuzuia bidhaa shindani kutoka nje,(China kwa mfano wanafanya Sana huu utaratibu kupambana Na bidhaa za ulaya Na U.S.A.), kinyume chake Ni "Revaluation!".
 
Wengi wamechangia vitu na kuweka msingi mzuri. Mimi nami naomba niongeze kidogo.

Kuhusu kushuka thamani kwa pesa kunakochochewa na mfumuko wa bei (inflation). Kuna mfumuko wa bei unaosababishwa ndani ya nchi na mwingine hutokea njema ya nchi kupitia uingizaji wa bidhaa kutoka nje (importation). Kwa tafsiri hii wakati mwingine uingizaji wa bidhaa kama huko zinakotoka Kuna mfumuko wa bei huchangia kushuka kwa thamani ya pesa ndani ya nchi iliyoagiza.

Uzalishaji duni wa bidhaa na huduma ndani ya nchi ni sababu kubwa ya kuagiza bidhaa na huduma hizo. Kwa maana hiyo nchi inapohitaji kuagiza bidhaa na huduma nje uhitaji wa fedha za kigeni ($) dhidi ya pesa ya ndani huwa mkubwa. Hii husababisha kushuka kwa thamani ya pesa.

Sera za nchi husika kupitia benki kuu ya nchi husika. Mfano South Africa huuza huduma na bidhaa zake ndani ya nchi kwa kutumia pesa yao (rand). Kwa maana hiyo mahitaji ya rand ni makubwa kuliko $ ndani ya South Africa. Hali hii husaidia kuinua thamani ya pesa ya ndani.
 
Back
Top Bottom