Kitovu Kikubwa kwa mtoto

Pole sana. Kama walivyosema wengine ni kweli kabisa, hiyo ni kutofunga mlango wa kitovu kwa ndani. Wa kike akija kuwa mkubwa pia inamletea shida wakati wa kujifungua kwani hujaa hewa.
Hilo la kumfunga sijui coin ni kukusaidia kupaminya halafu hewa irudi tumboni na baada ya muda, misuli inakaza tu. Hakuna uhusiano wowote wa ile coin na hiyo deformity. Kaza kile kitovu hewa itoke kwa mda ili misuli ya tumbo ipafunge yenyewe
 
Mkuu hiyo tape unamzungushia mpaka mgongoni?
Hapana
Unafunga kwa mistari kama mitatu au minne, mpaka ile sarafu haionekani about 5inch. Kila baada ya masiku unabilisha tape nyengine. itaondoka.

Ni kitu ambacho tulishamfanyia mtoto wangu kwa ushauri wa doctor hospitalini.
 
hiyo ni umbilical hernia,kwa umri hilo inaweza tundu linaweza kujifunga with time,au akahitaji upasuaji ili kulifunga hilo tundu,inaweza kuwa emergency kama hiyo hali inamletea matatizo kama maumivu makali or obstruction au elective kama hayo hana emergency condition na self closing after sometime imeshindikana.,onana na dr kwa ushauri zaidi
 
Hapana
Unafunga kwa mistari kama mitatu au minne, mpaka ile sarafu haionekani about 5inch. Kila baada ya masiku unabilisha tape nyengine. itaondoka.

Ni kitu ambacho tulishamfanyia mtoto wangu kwa ushauri wa doctor hospitalini.
nakushukiru sana mkuu
 
Hongera kwa kushare tatizo hapa JF.
Ni kweli kama walivyosema waliotangulia kitovu kutofunga ndani na hewa kupenya kuja sehemu ya nje.
Nami pia nimepitia malezi ya namna hii. Mwanangu akiwa na mwezi ndipo kitovu kilianza shida hiyo pia alikuwa ni mlizi sana hivyo kitovu kilikuwa kinajaa wakati aliapo kiasi cha kutaka hapa kupasuka.

Nilifadhahika kwa hali hiyo ndipo nilipotafuta maelezo kwenye mtandao na kukutana na hili suala la kufunga kitofu kwa sarafu.

Hivyo nilinunua bandage nyeupe famasi ,spirit ,pamoja na pamba. Nilitumia sarafu ya sh 200 .

Namna ya kufanya. Sikuwa na imani sana na hiyo sarafu kugusana na ngozi ya mtoto... hivyo niliizungushia kitambaa laini chepesi... bandika sarafu huku ukiwa umekiingiza kitovu cha mtoto ndani kwa kushikilia... tumia bandage kushikiza sarafu na mwili wa mtoto , urefu wa vipande vya bandage vinaweza kuwa sentimita sita hivi... tumia hadi vipande sita hivyi. Funga kwa ufanisi ili isiweze kutoka.
Mambo ya kuzingatia. Kila baada ya siku takriban 4 unaweza badilisha bandage ili pia uweze kusafisha sehemu hiyo ya ngozi iliyozibwa... hapa ndipo spirit itatumika.

Wakati hili zoezi linaendelea.. ngozi ya mtoto itaharibika na hapa kupata vipele... zingatia ubadilishaji wa bandage kwa kusafisha ngozi kila wakati ufanyapo ubadillishaji.

Jambo lingine ni je huyu mtoto hataoga... na akioga si bandage italowa ni kweli kabisa... hapa mzazi au mlezi anatakiwa awe mbunifu iwapo atahitaji mtoto aoge kila siku au unaweza ukawa unamuogesha siku za kubadili bandage tu na siku zingine ukawa unamfuta kwa kitambaa.
Zoezi hili lilimponesha kabisa binti yangu kwa takribani mwezi mmoja maana nilianza kumfunga akiwa na mieze miwili hadi alipotimiza miezi mitatu.

Sinahakika mtoto akishakuwa mkubwa ila yote yanawezekana uweza ukajaribu na kuona matokeo yake.
La msingi ni kuwa na determination bila uzembe kwani ni zoezi gumu pia kidogo.

Natumai maelezo haya yanaweza kutoa picha kidogo. Kama kuna maswali nitumie PM nitakuwa tayari kutoa maelekezo zaidi.
 
Navipi kama mtoto anamwezi mmoja hakuna daliki yote yakuwa nasubira labda mpaka baada ya miezi mitatu labda kitovu kinawezafunga kwa ndani chenyewe bila kutumia sarafu.Naomba kueleweshwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom