Kitovu cha mtoto kimegoma kurudi katika hali ya kawaida ..

Sheriff Rango

Member
Jul 29, 2018
64
105
Wakuu habari na poleni na majukumu , nimekuja mbele zenu sababu najua ndani ya jukwaa hili siwezi kosa solution au mawazo positive kuhusiana na changamoto hii ..

Nina mtoto wangu wa kiume ana umri wa miezi miwili , changamoto iliyopo nitokea kitovu chake kikatike ( kianguke ) hakijajirudi katika hali ambayo mimi binafsi na kaka ake vitovu vyetu vipo , yani kitovu chake kimevimba ivi ..

soo wakuu kama kuna mtu anajua dawa au njia ambayo alishawahi tumia kusolve changamoto hii please msaada , mana nataka nimsaidie handsome boy wangu asije shindwa kujiachia na sixpak zake uko baadae ..

Kama kuna changamoto ya uandishi naomb tuvumiliane maana me sio mzuli kwenye kushuka essay ..

Nawasilisha ..

Sent from my TECNO KB8 using JamiiForums mobile app
 
234789366_295198562397777_5775316544713413987_n.jpg

Lijue tatizo la mtoto kuwa na Kitovu kikubwa..!

Wakati mwingine mtoto anaweza kuwa na kitovu kikubwa. Uvimbe huu unaweza kuja na kuondoka na wakati mwingine unaweza kuwepo muda wote bila kuondoka. Tatizo hili linaitwa henia (hernia) ya Kitovu.

Henia ni nini?
Henia ni uvimbe unaotokana na sehemu ya ndani ya mwili mara nyingi utumbo au mafuta kusukumwa kwa nje kupitia sehemu ya ambayo kuna udhaifu wa misuli. Hivyo henia zinaweza kutokea katika sehemu mbalimbali za mwili.

Henia ya kitovu je?
Kitovu ambacho hujitokeza nje husababishwa na misuli ya tumbo kuachana kidogo. Kawaida misuli ya tumbo inanguvu ya kutosha kuzuia sehemu ya utumbo kutokeza. Sehemu ya kitovu kuna uwazi ambao hupitisha mishipa ya damu wakati mtoto yuko tumboni toka kwa mama kwenda kwa mtoto.

Sehemu hii inapaswa kufunga mara tu baada ya mtoto kuzaliwa. Hata hivyo kwa baadhi ya watoto huchelewa au hushindwa kabisa kufunga hivyo kusababisha uwazi kwenye misuli ya tumbo. Uwazi huo unaruhusu utumbo au mafuta mafuta ya mwili kutokeza hivyo kuonekana kama uvimbe.

Henia ya kitovu inaweza kuongezeka wakati mtoto analia, anacheka ama wakati wa kujisaidia. Hupotea mtoto anapokuwa amelala ama ametulia.

Je ufanye nini iwapo mtoto ana tatizo hili.
Watoto wengi tatizo hili hupotea kabisa kabla ya mwaka mmoja. Hata hivyo iwapo mtoto anaendelea kuwa na tatizo hili mpaka anafikisha umri wa miaka mitano atahitaji upasuaji. Upasuaji husaidia kuziba sehemu ya tumbo yenye uwazi.

Imani ya Kufunga kitambaa, kamba au sarafu za kizamani kukizunguka kitovu haitasaidia kumaliza tatizo.Tafuta ushauri wa daktari iwapo mwanao ana uvimbe kwenye kitovu.

Madhara ya henia
Henia ya kitovu kama zilivyo henia nyingine wakati mwingine inaweza kusababisha kufunga utumbo hivyo kusababisha maumivu makali na hata sehemu ya utumbo kuoza. Inapotokea hali hii mtoto atahitaji upasuaji wa dharura.

Jaribu kutumia dawa ya Asili:
Mafuta ya nazi yana ufanisi mkubwa katika kutibu hernia ya umbilical kwa watoto. Ikiwa umeona kuonekana kwa hali hii katika tumbo la mtoto wako basi inashauriwa mara kwa mara ufanyie massage ya tumbo na tumbo la mtoto na mafuta ya nazi. Massage kwa upole katika mwendo wa mviringo na ufanyie hili angalau mara 6 hadi 7 kwa siku kwa matokeo bora.

Dawa ya pili jaribu kutumia Mafuta ya Zaituni Olive oil.
Mafuta ya Zaituni
Mafuta ya mizeituni pia ni mafuta mashuhuri ulimwenguni kutokana na idadi kubwa ya faida za kiafya zinazohusishwa nayo. Muhimu katika kutibu hernia ya umbilical kati ya watoto wachanga, massage ya kawaida na ya upole ya mafuta ya mafuta kwenye tumbo na tumbo la mtoto inaweza kutengeneza hernia na pia kuzuia maendeleo yake zaidi.
 
View attachment 2856285

mkuu shukrani sana kwa msaada huu ..na nina maswali kidogo ;

a) Hii issue sio kwamba inatokana pia na huko hospital mda ambao mtoto amezaliwa sasa yule anaemkata na kufunga kitovu labda anakua hajakifunga au kukikata katika kipimo kinachotakiwa ..maana Bibi zake na ndugu wengine wanadai aliekifunga alikifungia mbali ndio mana kimebaki ivyo ??

b) upande wa iyo opparation , je kwa umri huu mdogo ni sawa kuwahi kumfanyia yani kulingana na umri wake haitamletea shida ?, au ni vizuli kupambana na izo njia nyengine ulizoshauli and then hii ya opparation iwe last option ?

Pambana na hizo njia nilizo kwambia operesheni itakuwa ni fainali

View: https://www.youtube.com/watch?v=qv8KGQB-bX4&ab_channel=Dr.Mwanyika
Halafu nikuulize swali je kitovu chake kilipo anguka siku 7 mulikiweka wapi?nani alikichukuwa?
 
Mbona bado mdogo huwa kinarudi taratibu. Futa hio picha kuna watu wana macho mabaya
 
Wakuu habari na poleni na majukumu , nimekuja mbele zenu sababu najua ndani ya jukwaa hili siwezi kosa solution au mawazo positive kuhusiana na changamoto hii ..

Nina mtoto wangu wa kiume ana umri wa miezi miwili , changamoto iliyopo nitokea kitovu chake kikatike ( kianguke ) hakijajirudi katika hali ambayo mimi binafsi na kaka ake vitovu vyetu vipo , yani kitovu chake kimevimba ivi ..

soo wakuu kama kuna mtu anajua dawa au njia ambayo alishawahi tumia kusolve changamoto hii please msaada , mana nataka nimsaidie handsome boy wangu asije shindwa kujiachia na sixpak zake uko baadae ..nime attach na picha ili kurahisisha uelewa

Kama kuna changamoto ya uandishi naomb tuvumiliane maana me sio mzuli kwenye kushuka essay ..

Nawasilisha ..View attachment 2856268

Sent from my TECNO KB8 using JamiiForums mobile app

Hakuna sababu ya kuhangaika na chochote. Kama akilia, kucheka au kujisaidia kinarudi ndani. Ni tatizo la kimaumbile kama lilivyoelezwa kuwa misuli ya tumbo haikufunga vyema. Hakuna kosa au sababu maalumu ya kueleza kwa nini haikufunga zaidi ya shida za kiuumbaji.

Hali hii huweza kurejea vyema yenyewe wakati wa ukuaji wa mtoto kulingana na kiasi cha nafasi/tundu lililopo.

Akifika miaka mitano, unaweza kuguatolia ili kujua hitaji la tiba ai la.

Hakuna wa kulaumiwa:

1: mama au baba wa mtoto.

2: nesi aliyezalisha mtoto.

3: hospitali aliyozaliwa mtoto.

4: kitovu kimepelekwa wapi au kuliwa na nini baada ya kudondoka au kilidondoka wapi na kwa njia gani.

MUHIMU:

1: Mwangalie mtoto kama sehemu kitovu kilipokatika pamefunga vyema na panakauka.

2: Mfikishe hospitali mtoto kwa suala hili MARA TU kitovu kitavimba na HAKIRUDI NDANI. Wakati huo pia huwa anapata maumivu.

3: Mwache mtoto na aishi maisha yake ya kawaida mpaka akifikisha miaka mitano kama hakuna shida yoyote. Akifikisha miaka mitano, mpeleke kwa mtaalamu wa afya/hospitali kwa ushauri zaidi.
 
swala la kufunga na kupona ni kikosawa kabisa , changamoto ni huo uvimbe tuu ..shukrani sana kwa ushauri
 
Back
Top Bottom