Kitimoto mwenye mapembe

Kitimoto mwenye mapembe

Juma Ponda Mkandamizaji.
Hizi fasihi zenu hizi....
24e5e3af58123973c743a3abe5c4b0a5.jpg
preying eye is always wide open
 
Msahana jr mi nimeamka na mning'inio sijaelewa kabisa nitafsirie kipare ili wanajamvi wasielewe. na kama kuna mpare mpofue macho asisome tafsiri.
 
6ef34be96e8a8dbb194caa516c797e2a.jpg


Basi nilipokuwa najiandaa kuandika hii mada nikamkumbuka nyoka mwenye makengeza. Nikashangaa kweli nikamkumbuka kitimoto mwenye
Mapembe
Chongo
Mikia miwili
Mguu mmoja

Kwa hakika huyu ni kitimoto wa aina yake ni tofauti kabisa na wengine na pengine analijua hili au halijui lakini kwa sifa hizi anabaki kuwa wa kipekee huku wenzake ama wakisita au kumgwaya kumwambia! Kumbeza?! Nani atathubutu! Wewe huna mapembe yeye anayo wewe una miguu minne yeye ana mmoja ole wako.

Kitimoto mwenye mapembe ni kiwakilishi cha Sanaa yenye uhalisia katika maisha yetu ya kila siku kuanzia majumbani mwetu makazini mpaka kwenye majukumu mazito yahusuyo mustakabali wa Taifa. Kote huko chochote chenye kutia shaka kubwa kisicho cha kawaida kabisa chenye kuacha maswali mengi yasiyo na majibu. Hicho hakina tofauti na kitimoto mwenye mapembe na mguu mmoja.

Ukiwaza ya nyoka mwenye makengeza(fasihi kubwa hii)na sanaa ya Mr Ebbo RIP ya samaki aliyepaka wanja unaona wazi kabisa ni kama maono ya kushangaza ambayo wengi hawakujanasibu nayo. Kila nikigeuka kila nikikata kona kila nikichungulia namuona kitimoto mwenye mapembe halafu anatisha kweli...!

Naamini hii si ndoto na siko pekeyangu[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji115] [emoji115] [emoji115] [emoji115] [emoji124] [emoji124] [emoji124] [emoji124] [emoji124] [emoji124] [emoji124] [emoji124]


Pata wimbo hapo
 
Msahana jr mi nimeamka na mning'inio sijaelewa kabisa nitafsirie kipare ili wanajamvi wasielewe. na kama kuna mpare mpofue macho asisome tafsiri.
[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji115] [emoji124] [emoji124] [emoji124] [emoji124]
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom