The Businessman
JF-Expert Member
- Jan 9, 2014
- 7,397
- 9,264
Hivi umekisoma alicho kiandika Kitila? ni wapi wana tofautiana na Ndalichako? Anacho hitaji Kitila ni msimamo na Debate! Muulize Kitila atupe mifano ya nchi iliyo andaa Debate ili kujadili mfumo wa elimu au upangaji matokeo!Nashukuru kitila kwa kuliona hili.tatizo wasomi wetu hawaishi na yale waliyoyasomea,wanaishi kwa kufuata mioyo yao na nafsi zao ndiyo maana maamuzi yao yanaonekana ya kukurupuka kwasababu yamejaa chuki,visasi kiburi na dharau.katika hili joice kathibitisha jinsi wasomi wetu wasivyoishi na elimu yao.
Kama ungekuwa umemsikiliza vizuri Prof Ndalichako wala usinge andika haya ... aliwaagiza Necta warudishe na kupitia upya viwango vya ufaulu si kurudisha tuu Division!Ndalichako et...ra... Issue si GPA au DIVISION!! Issue ni viwango/ alama za ufaulu. Kwa uelewa mdogo tu ukipata chini ya 50% katika jambo lolote unalo lifanya umeshindwa!!!!! Sasa, acha tushushe kiwango hadi 40% basi. Vinginevyo hata kama itakuwa Division bado alama ya chini ya ufaulu ni 21% bado utakuwa hujasaidia kupandisha kiwango cha elimu Tanzania!
Wangefanya kama chuo 2.0 pass below that failIwe mfumo wa GPA ambao ni (unajumlisha alama na kugawanya kwa idadi ya masomo unapata wastani) au Division (unajumlisha alama) tofauti ni ndogo, karibu ni kitu kile kile ISIPOKUWA kilicho fanyika ni kupanua wigo wa wanafunzi kushinda kwa malengo ya kisiasa. Mfumo wowote unafaa ikiwa tu alama za ufaulu si chini ya asilimia 40. GPA inaanzia 0 hadi 5. Kichekesho kipo hivi eti mwanafunzi aliye pata GPA 0.1 kwamba amefaulu (PASS). Ukitafuta asilimia ya 0.1 ya 5.0 ina maana kuwa ufaulu una anzia 2%!!!! Huu in mzaha. Hitimisho ni alama za kufaulu. Kiwango cha chini cha kufaulu isiwe chini ya asilimia 40%.
Prof. Ndalichako amerejesha mfumo wa zamani uliobadilishwa bila utafiti wala ushirikishi wa wadau. Prof. Ndalichako ameirudisha wizara kwenye ground zero au back to square one ili ijipange kutafuta mfumo mpana wa kupima ufaulu wa watahiniwa katika ngazi mbali za elimu. Mfumo utakaopatika sharti utokane na utafiti ambao matokeo yake yaongoze mjadala shirikishi wa kitafa. Waziri alichokiuka ni kutoa agizo badala kanuni na kuzitangaza kwenye gazeti la serikali. It can be done retrospectivelyProfesa hajakosea kumkosoa mama Ndalichako, nadhani anakubaliana naye, sasa kama vipi wananchi waulizwe kuwa wanataka mgumo upi?
Ila thuu wa division wakati unaendelea ndio wananchi na wadau mbali mbali waulizwe, wasisikilize vilio vya mashehe misikitini
Sasa huyu Prof naye shida tu naye anataka kuwa profesa wa siasa. Tulikuwa na mfumo wa Division akaja mwingine akauondoa akaleta mfumo wa GPA huyu wa sasa ka-restore system, hivi ku-restore ni kufanya kitu kipya? Mimi nadhani sasa ni nafasi kwa huyu profesa kutoa maoni yake kwanini anadhani tuhame kwenye division na kwenda kwenye GPA maana kwa jinsi nilivyomsoma ni kwamba waziri wa elimu aliyeondoa division na kuleta GPA hakushrikisha wadau kwa hiyo huyu sasa ame-restore sysytem ili mtoe mawazo yenu
Ndalichako na serikali wawaeleze watanzana ni namna gani wataboresha au kuongeza maarifa ya watoto wao. Elimu haiboreshwi kwa mfumo wa Division au GPA!
Watu wanatakiwa kujua hapa ni kuwa kibaya zaidi Necta wametumia mfumo wa GPA vibaya na kushusha viwango vya ufaulu...Iwe mfumo wa GPA ambao ni (unajumlisha alama na kugawanya kwa idadi ya masomo unapata wastani) au Division (unajumlisha alama) tofauti ni ndogo, karibu ni kitu kile kile ISIPOKUWA kilicho fanyika ni kupanua wigo wa wanafunzi kushinda kwa malengo ya kisiasa. Mfumo wowote unafaa ikiwa tu alama za ufaulu si chini ya asilimia 40. GPA inaanzia 0 hadi 5. Kichekesho kipo hivi eti mwanafunzi aliye pata GPA 0.1 kwamba amefaulu (PASS). Ukitafuta asilimia ya 0.1 ya 5.0 ina maana kuwa ufaulu una anzia 2%!!!! Huu in mzaha. Hitimisho ni alama za kufaulu. Kiwango cha chini cha kufaulu isiwe chini ya asilimia 40%.