Kitila Mkumbo awashangaa Upinzani wanaotetea vihiyo

Ishu sio kutetea vihiyo..walichokuwa wanadai ni utaratibu wa kuwaondoa chuoni ambao ulikuwa umewadhalilisha utu wao..Naona watu wamehamisha magoli kutafuta siasa za maji taka
Kuna utaratibu wowote wa kumuondoa mwizi, mdanganyifu?
 
Kuinyoosha elimu yetu lazima kuna watu watatimuliwa vyuoni na makazini pia hakuna namna .
Elimu yetu hii ni balaa kuna walimu wana sifa zina mashaka sana mpaka unashangaa alikuaje mwalimu
Sasa kama mtu ana D tu ya Biology na aliacha Physics na Chemistry form 2 atasomaje ualimu wa sayansi
Wote wanaowatetea ni Vilaza, sina jibu lingine, rais ameshasema.
 
Kazi ya wana sasa ni kupindisha HOJA, wapinzani hawajatetea suala la "vilaza" wana tetea utaratibu uliotumika kuwaondoa chuoni. Hili Kitilya analijua, Magufuli analijua, Joyce Ndalichako analijua na hata Dr. Tulia Mwansasu analijua lakini kwasababu ni wana siasa wameamua kupindisha ukweli, Profesa Kitilya nae kawa mwana siasa na ame toa comment za kisiasa.
 
Hebu Lumumba lete source hapa, au ni ile kauli ya Magu jana an si unachanganya kweli habari??

Kwani umesha sign buku 7, ukanywe chai kwanza, then uridi?
Hoja yenu humu hivi sasa ni buku saba, mmeishiwa kwelikweli.
 
Ishu sio kutetea vihiyo..walichokuwa wanadai ni utaratibu wa kuwaondoa chuoni ambao ulikuwa umewadhalilisha utu wao..Naona watu wamehamisha magoli kutafuta siasa za maji taka
Ilibidi wapewe muda mfupi kwani walikuwa wamepanga kufanya fujo (na ukizingatia ni form IV wangewatesa bura kaka na dada zao)
 
Wakaishtaki serikali kwa kutimuliwa chuoni na nafikiri wanasiasa wasilizungumzie kwenye keyboard, waende mahakamani wakawasaidie kufungua kesi ya kuonewa kama wameonewa watalipwa, naona watu wanatamani Rais aseme kitu sasa naye kakomaa, saa nyingine tuwe kama binadamu, hizi kelele kwa hii serikali hazitasaidia kitu, mssada wanohitaji hao vijana kama wana haki ni kupelekwa vyuo vya private na sio mijadala ya kujijenga kisiasa, kama watu mlitaka kuchanga hela za kuonyeshea Bunge mnashindwa vipi kujichanga muwarudishe vyuoni ili serikali iumbuke?
 
Kitila Mkumbo siku nying alijua udahili huo wa UDOM ila alikaa kimya! Alitarajiwa atoe neno kwa serikali wakati inafanya hayo ila alinyamaza! Huyu jamaa siyo wa kuaminika hata chembe!
 
Kitila ni mchumia tumbo, uchu wa madaraka. Watanzania msiwe wepesi wa kusahau! Huyu alitimuliwa CHADEMA kwa ajili ya kutaka kufanya "mapindizi" kutafuta madaraka kwenye chama. Maadamu amempata rais anayetaka watu wa kujikomba, atafanya "vituko" vingi!
Sasa kama Prof ni mchumia tumbo je wewe ni mchumia nini mgongo? Kila mtu anachuma sababu kuu ni tumbo!!!
 
Hoja yenu humu hivi sasa ni buku saba, mmeishiwa kwelikweli.

Uzuri Mwenyezi Mungu amewapa akili na mawazo ya utambulisho wenu, yaani humu ndani mnajulikana kwa hoja zenye Ulemavu wa AKILI ambazo ni beyond DHAIFU.
Mfano ni sawa na Mtu anayepigwa Ngumi anamrudishia mwenziye kwa kumpiga kwenzi, you see now it's very unfair & irrelative.

Mnapaswa kuja na hoja zenye vision,facts,logic etc.

Siyo vioja kama watoto vile, yaani oooh mara huyu kanikonyeza,oooh mara huyu kanisunya, oohhh mara huyu kani zomea...what's the hell is this?????????
 
Ukiona mpinzan anasifiwa nachama tawala anza kutia Maji
Kitila kusifiwa tu jana basi kaona yeye ndiyo peke yake mwenye solution ya matatizo ya elimu Tanzania!!

Hawa vijana walipofukuzwa sababu zilizotolewa na Waziri zilikuwa tofauti na alizozitoa Rais!! Kuwalaumu watu ni kuwaonea kwa vile walicomment kwa sababu zilizotolewa mwanzo na mazingira ya kuondolewa/kufukuzwa kwao!!

Sasa kwa vile Rais katuambia ukweli naona hata comment zimebadilika.

Issue sasa Bungeni Wabunge wamuhojia Waziri Ndarichako kwa kulidanganya Bunge sababu za kuwafukuza Wanafunzi!!
 
Mwenyekiti wa chama cha ACT-WAZALENDO Tanzania Prof. Kitilya Mkumbo amewashangaa Wapinzani wanaowatetea wanafunzi "vihiyo" waliotimuliwa.

Aidha amesema kuwa alishawahi kuandika makala ya namna ya kutatua tatizo la uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi ila hayakufanyiwa kazi.
Huyo Professor nae kilaza, hakuna anayetetea reason ya kuwafukuza bali utaratibu wa kuwafukuza ndio kimeo, kwann hawakuwaondoa kwa mafungu? read between the line and not making you conculusion via the Heading.
 
Mwenyekiti wa chama cha ACT-WAZALENDO Tanzania Prof. Kitilya Mkumbo amewashangaa Wapinzani wanaowatetea wanafunzi "vihiyo" waliotimuliwa.

Aidha amesema kuwa alishawahi kuandika makala ya namna ya kutatua tatizo la uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi ila hayakufanyiwa kazi.
Aache roho mbaya. Kwanza wale wanafunzi siyo VIHIYO kwani wana div 1&2. Pili ni kwamba njia iliyotumika kuwaondoa chuoni haikuwa sahihi. Hiyo ndiyo hoja ya upinzani. Kama na yeye anataka ukuu wa wilaya au mkoa aseme. Aeleze pia Jesca alifikaje chuo kikuu huku akiwa KILAZA.
 
Mwenyekiti wa chama cha ACT-WAZALENDO Tanzania Prof. Kitilya Mkumbo amewashangaa Wapinzani wanaowatetea wanafunzi "vihiyo" waliotimuliwa.

Aidha amesema kuwa alishawahi kuandika makala ya namna ya kutatua tatizo la uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi ila hayakufanyiwa kazi.
Mwenyekiti wa chama cha ACT-WAZALENDO Tanzania Prof. Kitilya Mkumbo amewashangaa Wapinzani wanaowatetea wanafunzi "vihiyo" waliotimuliwa.

Aidha amesema kuwa alishawahi kuandika makala ya namna ya kutatua tatizo la uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi ila hayakufanyiwa kazi.
Tangu lini Kitila Mkumbo akawa mwenyekiti wa ACT-Wazalendo
 
Back
Top Bottom