Prof. Kitila Mkumbo anatamani madaraka hata kama ni dhuluma kwake; yeye ushindi wowote unaompa kula ni sahihi

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
877
4,106
Nimemsikiliza Prof Kitila Mkumbo , kwanza napingana na wanaoamini kila Prof ana akili. Baadhi wana uwezo wa kufaulu mitihani ya darasani aidha kwa kukariri au kubahatisha ila siyo akili. Moja ya takwa la mtu mwenye mwenye akili hapa Duniani ni kuhakikisha akili zake zimetumika kutatua changamoto zilizopo.

Nimesoma machapisho mengi, sijaona popote ambapo Prof. Mkumbo amewahi kubuni au kuwa na Mradi uliovadilisha jamii. Badala yake amewahi kuandika machapisho yakufanya awe na Masters na Phd. Kwamba alifanya utafiti unaogusa jamii hapana.

Kwenye siasa, Prof Mkumbo hana uwezo wa kushawishi wananchi wakamsikiliza. Leo mwaka wa tatu nani amewahi kumwona akihitisha mikutano kwenye jimbo? Anasubiri dola impe ubunge na si kutumia ushawishi wa sera na elimu yake kupata wapiga kura

Tunapokuwa na wasomi wanaotegemea dola kama alivyofanya Dr. Bashiru last time tunatengeneza Taifa la wasomi wanapanda mbegu ya chuki na ukatili.

Maisha ya siasa siyo theories za kwenye vitabu. Leo matumizi ya dola kama ya akina Hitla yangekuwa kimbilio la Siasa Mataifa yaliyoendelea yasingefanya uchaguzi wa kidemokrasia na wanasiasa wasingekabidhiana madaraka. Wenzetu wasomi hawa wanaamini dola na siyo demokrasia.

Mwisho, Kitila ,Bashiru na Kabudi wanatoka chuo kikuu cha DSM. Chuo hiki kimefuta kabisa mijadala na kubaki kuwa sekondari ya juu kama alivyowahi kukiita Jenerali Ulimwengu. Kufa kwa chuo cha DSM nimawazo ya maprofesa na Phd nyingi zilizopo pale. Hawa watatu ni sign ya aina ya wasomi waliobaki shuleni. Tunao waalimu ambao ni waalimu waliopata nafasi nje ya ualimu wanaosimamia ualimu. Tunatakiwa kuondokana na taifa la waalimu twende kwenye Taifa la wasomi na wafanyabiashara.

Most of Profs Tanzania wanakosa business mind. Ukiminya demokrasia nchini automatically umeminya haki na maendeleo. Maprofesa wetu wanashindwa kuwaza kesho ya nchi wanawaza wao na familia zao. Hakuna mwenye biashara watu genge, wanaishi kwa mishahara na kodi za wananchi maisha yao yote. Huu uprofesa wakutegemea kulishwa na wasiosoma una faida gani kwa nchi?
 
Mkuu tatizo sio uprofesa wao, bali ukiingia ndani ya CCM na kukabidhiwa madaraka, basi itakupasa kuishi kwa mawazo, maneno, na matendo ya kipuuzi ya ki CCM.

Kamwe hawawezi kuishi ndani ya kasha katika fikra zao huru za kisomi, ni lazima woteke nje ya kasha na kuishi kama "majority" ya vilaza wanavyoishi kutokana na utamaduni wao uliotamalaki matendo ya kinafiki.
 
Chuki zimekujaa dhidi ya wengine, si ufanye utafti wewe utakoleta mabadiliko. Unatajataja majina tu kwa mistari isiyo na vina.

yaani umekaa tu unasubiri chapisho la kitila kutatua changamoto zako...
 
Siku hizi uchawa unazalisha vyeo, wakipata vyeo kwa kigezo cha uchawa usitegemee hata dakika moja kiumbe wa sampuli hiyo kuna siku atatumia akili zake kwenye kufikiria kabla hajaongea.
 
Back
Top Bottom