Kitila Mkumbo awashangaa Upinzani wanaotetea vihiyo

sirluta

JF-Expert Member
Nov 28, 2012
6,325
2,491
Mwenyekiti wa chama cha ACT-WAZALENDO Tanzania Prof. Kitilya Mkumbo amewashangaa Wapinzani wanaowatetea wanafunzi "vihiyo" waliotimuliwa.

Aidha amesema kuwa alishawahi kuandika makala ya namna ya kutatua tatizo la uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi ila hayakufanyiwa kazi.
 
Wapinzani na wale wa Chama Tawala walitetea logistics za kuwaondoa pale chuoni,especially wale wanafunzi walikua under 18years. Kwa kweli mimi naona hii issue inakuwa twisted kila sisiku na sababu zinazotolewa zinabadilika.Tuzidi kuliombea hili taifa letu,tukiendelea kuwalaumu wapinzani wakati haya yote yamefanyika chini ya Chama Tawala,hatuta fika.Cha muhimu ni kujisahihisha pale palipo kosewa na kwenda mbele.Sio wakati wa kutafuta mchawi.
 
Mwenyekiti wa chama cha ACT-WAZALENDO Tanzania Prof. Kitilya Mkumbo amewashangaa Wapinzani wanaowatetea wanafunzi "vihiyo" waliotimuliwa.

Aidha amesema kuwa alishawahi kuandika makala ya namna ya kutatua tatizo la uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi ila hayakufanyiwa kazi.
Kwani kitila siku hizi ni mwenyekiti wa ACT-wazalendo?
 
Naona huyu professor anatafuta kick kiaina maana hata yeye anajua kuwa hoja ya "watetezi wa vihiyo" si utetezi juu ya viwango/vigezo vya kudahiliwa tu bali zaidi sana ni namna walivyoondolewa. Professor alishatoa maoni yake kuhusu kuongeza waalimu na kama anafikiri alipuuzwa na uongozi uliopita aushairi uliopo. Prof aangalie asijeonekana anatafuta recognition kisiasa.
 
Mkuu sirluta kabla ya kutaka ueleweke utakavyo,hakikisha unaandika kwa usahihi. Kwanza,hakuna Prof. Kitilya Mkumbo. Kuna Prof. Kitila Mkumbo. Prof. Mkumbo si Mwenyekiti wa ACT. Mwenyekiti ni Mama Mghwira. Uandishi wako ni ushahidi tosha wa kukurupuka kwako na kuwa kilaza. CCM itakushinda kijana. Wasalimu Arusha!

Mzee Tupatupa
 
Nadhani huenda raisi Magufuli hajui waliotimuliwa UDOM walikuwa nanasomea digree ama diploma ya miaka mitatu. Bado anachanganya wale wa St. Joseph na wa UDOM. Anahoji f4 wamefikaje chuo kikuu na mkopo wakapata pasipo kujua wanasomea degree ama diploma kwani kama kati ya waliotimuliwa kuna wenye div 4, wapo wenye 1 na 2 na 3 pia ambao walipata hizo nafasi kihalali na hawakupaswa kufukuzwa kwa makosa ya wenzao waliopata div 4 ama walimu wao waliokataa kuwafundisha.

Yaani hii movie haina tofauti na ile mtu anapewa kibali cha kujenga mahali na serikali, anajenga, anaishi na mamlaka za serikali zinapeleka maji, umeme, vituo vya afya, halafu baadae serikali hiyo hiyo inakubomolea na kukufukuza!
 
Mwenyekiti wa chama cha ACT-WAZALENDO Tanzania Prof. Kitilya Mkumbo amewashangaa Wapinzani wanaowatetea wanafunzi "vihiyo" waliotimuliwa.

Aidha amesema kuwa alishawahi kuandika makala ya namna ya kutatua tatizo la uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi ila hayakufanyiwa kazi.
Kitila ni mchumia tumbo, uchu wa madaraka. Watanzania msiwe wepesi wa kusahau! Huyu alitimuliwa CHADEMA kwa ajili ya kutaka kufanya "mapindizi" kutafuta madaraka kwenye chama. Maadamu amempata rais anayetaka watu wa kujikomba, atafanya "vituko" vingi!
 
Ishu sio kutetea vihiyo..walichokuwa wanadai ni utaratibu wa kuwaondoa chuoni ambao ulikuwa umewadhalilisha utu wao. Naona watu wamehamisha magoli kutafuta siasa za maji taka
Hakuna aliyedhalilishwa. Shule zote siku zote zikifungwa huwa ni immediately kesho yake huwa hakuna huduma. Watoto na wazazi hawana tabu kupewa 24 hours hii ndiyo kawaida. Nani kalalamika kashindwa kuondoka? UKAWA as usual walitaka political capital out of other people's misery: mngewapa mwezi mmoja kurudi nyumbani ingesaidia nini zaidi ya kuleta wachochezi?
 
Mkuu sirluta kabla ya kutaka ueleweke utakavyo,hakikisha unaandika kwa usahihi. Kwanza,hakuna Prof. Kitilya Mkumbo. Kuna Prof. Kitila Mkumbo. Prof. Mkumbo si Mwenyekiti wa ACT. Mwenyekiti ni Mama Mghwira. Uandishi wako ni ushahidi tosha wa kukurupuka kwako na kuwa kilaza. CCM itakushinda kijana. Wasalimu Arusha!

Mzee Tupatupa
wenzako wameelewa, vilaza kama wewe ndo hujaelewa. Unadhani wote huku ni wajaluo ndo tujue majina yenu yanaandikwaje? Kikubwa ni ujumbe, hata wewe najua umeelewa vema na pengine unajua zaidi ila kwakuwa huna la maana la kuongeza, basi utaamua tu uchafue mazingira kama wale wanaojisaidia kwenye vituo vya mabasi ya mwendokasi et kwakuwa tu vyoo havijakamilika!
 
Mwenyekiti wa chama cha ACT-WAZALENDO Tanzania Prof. Kitilya Mkumbo amewashangaa Wapinzani wanaowatetea wanafunzi "vihiyo" waliotimuliwa.

Aidha amesema kuwa alishawahi kuandika makala ya namna ya kutatua tatizo la uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi ila hayakufanyiwa kazi.
Tunaomba chanzo cha taarifa yako mkuu lkn kitilya sio mwenyekiti wa ACT
 
Mwenyekiti wa chama cha ACT-WAZALENDO Tanzania Prof. Kitilya Mkumbo amewashangaa Wapinzani wanaowatetea wanafunzi "vihiyo" waliotimuliwa.

Aidha amesema kuwa alishawahi kuandika makala ya namna ya kutatua tatizo la uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi ila hayakufanyiwa kazi.

Mama Anna ameacha lini kuwa mwenyekiti wa ACT? Au ndiyo kama Mwighamba alivyofanyiwa?
 
Hakuna aliyedhalilishwa. Shule zote siku zote zikifungwa huwa ni immediately kesho yake huwa hakuna huduma. Watoto na wazazi hawana tabu kupewa 24 hours hii ndiyo kawaida. Nani kalalamika kashindwa kuondoka? UKAWA as usual walitaka political capital out of other people's misery: mngewapa mwezi mmoja kurudi nyumbani ingesaidia nini zaidi ya kuleta wachochezi?
kuna mbunge alisema alikuwa anawasomba na pick up yake! Kwani pick up ni gari la kubeba abiria? Trafic wangemkamata pia angelalamika. Lakini, alikuwa anawasombea wapi? Ukute ni kwenye yale madanguro yao!
 
Huyu profesa kitilya mkumbo amekuwa kama dr. Bana, hawa wote hawana tofauti na watu kama Hamad rashid au mrema au shibuda

Kwani tatizo la Dr. Bana ni lipi? Na tatizo la Profesa Mkumbo Ni lipi? Na matatizo ya Mrema na Shibuda ni yapi? Vipi Kuhusu Hamad Rashid?
 
Back
Top Bottom