Kiti cha Ubunge Rorya - Wananchi Jimbo la Rorya muwe makini

Mamboleo

Member
Oct 15, 2008
69
38
Katika wakati huu ambapo watu mbalimbali wenye nia ya kutaka kuchaguliwa kushika nafasi za uongozi kisiasa katika uchaguzi ujao,Jimbo la Rorya linawaniwa na watu mbalimbali kama wafanyabiashara,wanasiasa,wanaharakati katika kuwania nafasi ya mbunge na madiwani.

Mmojawapo wa alionyesha nia ya wazi ni Ndugu Stephen JJ Owawa ambaye ni mtumishi wa ofisi ya CAG huko Bukoba.Amekuwa akizunguka jimbo zima akitafuta kuungwa mkono kupata tiketi ya CHADEMA kama mgombea wa nafasi ya ubunge.Hatuna uhakika kama CHADEMA wamempa hiyo ridhaa ya kuitisha mikutano ya kisiasa!

Taarifa zilizopo ni kwamba Ndugu Owawa amesimamishwa kazi na mwajiri wake kwa tuhuma za ubadhirifu na kuna uchunguzi unafanyika dhidi ya tuhuma hizi.

Inawezekana Ndugu Owawa ana nia kweli ya kuwaongoza wana Rorya kama Mbunge lakini tuhuma hizi za ubadhirifu zinamtia doa hasa anapotaka madaraka hata kabla ya tuhuma hizo kujulikana kama ni za kweli au si za kweli.

Wana Rorya muwe makini sana na wagombea wanaokuja kutafuta ajira mbadala kwa kisingizio cha kutaka kuinua maendeleo ya jimbo lenu.
Nawakilisha
 
Umetumwa kusema haya? Umeshapokea kitu kidogo kama kawa ya chama chetu cha kijani ili uchafue watu tishio katika chaguzi zijazo?
 
  • Thanks
Reactions: Izu
Tupe chanzo cha taarifa ya tuhuma dhidi ya Owawa! Si unakurupuka kama aliyefumaniwa Mamboleo
 
Last edited by a moderator:
Owawa kitu gani, mnajifanya kujimilikisha jimbo la Rorya nyinyi watu wa Utegi, Kowak, Shirati, Ingiri Juu na kuwaacha wenzenu wa Kinesi, Ruhu, Komuge, Nyanchabakenye, Irenyi, Kirumi, Kuruya. Mwaka huu hatutaki lazima Mbunge atoke Irenyi lya Kahenge.
 
Mimi bado sijatangaza nia. Safari hii mimi ndiyo Mbunge na nitatokea CHADEMA na kwetu ni Utegi.
 
Mimi natoka RORYA Kata ya Nyamagaro, kipindi hiki tunachagua Mbunge kutoka Tarafa ya Nyancha, ninyi ambao mmejimirikisha jimbo toka Uhuru sasa tunasema yatosha, kwanza hakuna mlichofanya kipya!! Bungeni hamuongei, maendeleo hakuna.......!!!

Bora tuchague kutoka Nyancha huku...
 
Haswaaaa...Umemaliza mkuu, safari hii lazima Mbunge atoke Tarafa ya Nyancha huku, hawa wajaluo kwa sasa imetosha, hakuna kipya walichofanya....
 
Katika wakati huu ambapo watu mbalimbali wenye nia ya kutaka kuchaguliwa kushika nafasi za uongozi kisiasa katika uchaguzi ujao,Jimbo la Rorya linawaniwa na watu mbalimbali kama wafanyabiashara,wanasiasa,wanaharakati katika kuwania nafasi ya mbunge na madiwani.

Mmojawapo wa alionyesha nia ya wazi ni Ndugu Stephen JJ Owawa ambaye ni mtumishi wa ofisi ya CAG huko Bukoba.Amekuwa akizunguka jimbo zima akitafuta kuungwa mkono kupata tiketi ya CHADEMA kama mgombea wa nafasi ya ubunge.Hatuna uhakika kama CHADEMA wamempa hiyo ridhaa ya kuitisha mikutano ya kisiasa!

Taarifa zilizopo ni kwamba Ndugu Owawa amesimamishwa kazi na mwajiri wake kwa tuhuma za ubadhirifu na kuna uchunguzi unafanyika dhidi ya tuhuma hizi.

Inawezekana Ndugu Owawa ana nia kweli ya kuwaongoza wana Rorya kama Mbunge lakini tuhuma hizi za ubadhirifu zinamtia doa hasa anapotaka madaraka hata kabla ya tuhuma hizo kujulikana kama ni za kweli au si za kweli.

Wana Rorya muwe makini sana na wagombea wanaokuja kutafuta ajira mbadala kwa kisingizio cha kutaka kuinua maendeleo ya jimbo lenu.
Nawakilisha

Magamba mwaka huu mtakuja na story za uongo na uzushi ila standard seven wenu lazima aondoke tu.
 
Back
Top Bottom