Watanzania hatujawa na desturi ya kuwa na sauti moja katika kudai haki zetu, kila mtu hudai kivyake, wasanii hudai haki zao kivyao, madaktari hudai haki zao kivyao nk. huku kada zingine zikisema madai hayo hayawahusu kwa sababu sisi sio wasanii sisi sio madakitari.
Pamoja na kuwa Watanzania ni waoga wa kudai haki kwa pamoja lakini kuna wakati kutokana na mazingira na misukumo ya kijamii, kimaisha hulazimika kuungana na kujenga sauti moja.
Mwanzoni mwa miaka ya 90 tulishuhudia wimbi kubwa la wananchi kutoka kwa kada mbalimbali wana sheria, wanasiasa na wananchi wa kawaida bila kujali itikadi zao wakiungana kutaka mabadiliko ya utawala, vuguvugu ambalo lilizaa mfumo wa vyama vingi.
Kikundi cha Wazanzibari KAMAHURU kilichokuwa kinapigania demokrasia kiliungana na Civic Movement lililokuwa kundi la kupigania haki za binadamu Tanzania Bara na kuunda Chama cha Wananchi CUF. Chama cha NCCR - Mageuzi kilitokana na Wajumbe wa Kamati iliyoundwa kwa ajili ya mageuzi ya Katiba, National Committee for Constitution Reform - NCCR.
Kitendo cha wanasiasa wachache kutaka kubadili katiba ili kuongeza muda kwa maslahi ya wachache bila ridhaa ya wananchi walio wengi kinakwenda kuzalisha vuguvugu jingine ambalo litawafanya wananchi kuungana kupinga mabadiliko hayo. Ikumbukwe kuwa sio wana CCM wote wanaotaka mabadiliko hayo.
Kitawafanya wakulima, wanasiasa, wafanyabiashara, machinga, walimu, wahadhiri, madereva, wana sheria nk wote kuungana pamoja na wanaharakati kupinga mabadiliko hayo, tutaanza kushuhudia kamati mbalimbali kama zile za National Committee for Constitution Reform - NCCR zikiazishwa na huo ndio utakuwa mwanzo wa harakari za mabadiliko chanya kama yaliyofanywa miaka ya 90.