Kitendawili {malenga wapya} | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kitendawili {malenga wapya}

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Viper, Apr 25, 2011.

 1. Viper

  Viper JF-Expert Member

  #1
  Apr 25, 2011
  Joined: Dec 21, 2007
  Messages: 3,665
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Jogoo lina mafamba, linatamba kiamboni,
  Kwa kiburi lajigamba, hadi kiambojirani,
  Hili jogoo la shamba, sasa lawika mjini,
  Kitendawili na tega, mteguzi ategue.


  Mbawa linavyozipiga, wengine hawasogei,
  Shuti nejawa na woga, wote wamekuwa hoi,
  Kama wenyewe mwafuga, kitoweo halifai,
  Kitendawili na tega, mteguzi ategue.


  MALENGA WAPYA
   
 2. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #2
  May 13, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Jogoo hilo khatari,sasa ilmeelevuka.
  Linasambaza khabari, kula kona laitika,
  Wakati huu shubiri, maradhwi yameitika,
  Haraka apewe jiko, ulinusuru na baa.

  Kuungana walimwengu, ni neno lenye mwafaka,
  Linapendeza kwa Mungu, pamoja na malaika
  Kukwambia fanya langu, Jiko haraka kamata,
  Haraka apewe jiko, ulinusuru na baa.

  Dr Hamza Yousuf Al Naamani( Barubaru)
  1523 Umm Hays
  Doha. Qatar
   
Loading...