Kitanda: Shahidi asiyesema wa mambo yetu ya siri!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
Ukiondoa shughuli nyingine za kitandani, kitanda kwa kawaida ni mahali pa kupumzika. Kitandanni mahali ambapo mtu anatakiwa awe na amani napo na kwa kweli ni mahali pa faragha. Na wote tunajua kuwa kitanda kwa kawaida ni mahali pa binafsi sana. Lakini japo watu wanachukulia kitanda kama kitu cha kawaida katika nyumba ukweli ni kuwa kitanda ndio rafiki yetu wa karibu sana labda kuliko hata ndugu wa damu. Ni shahidi wa furaha zetu, machozi, vicheko, faraja n.k Kitanda ni yule rafiki asiye kuhukumu wala kujali umekosea nini kwani daima anakukaribisha.

Lakini kuna mambo mengi ambayo yanaweza kutufanya tufikirie kuhusu kitanda kwani wengine wanafikiria kitanda ni mahali pa kwenda kufanya mazoezi ya kuumba watoto. Kitanda ni zaidi ya hivyo. Hata hivo kuna watu wengine wakifikiria kitanda hukosa amani kwani kwao si mahalij pa kutulia ni mahali pa mawazo. NI hapa wanapokesha usiku kuwaza na wengine ni mahali ambapo wanajua wakiamka asubuhi wanakuwa wamechoka kabisa mwili una maumivu. .

Vile vile japo kitanda ni mahali pa kwenda kulala kuna watu wana riituals za ajabu kabla ya kwenda kulala. Wengine hawana lolote wao wakisikia usingizi wanaenda kujilaza tu vile vile waliivyo wakati wengine huijandaa kwa kuoga na nimewahi kusikia habari ya baadhi ya wanawake ambao hujipara kwanza kabla ya kwenda kulala - ati wakishtushwa wasije kukutwa hawana make up! Lakini hebu tushirikiane hasa mawazo yetu kuhusu kitanda hasa tunapoenda usiku kwenda kulala.

a. Je unaamua kwenda kitandani kabla ya kupata usingizi (unaenda kutafutia usingizi huko kitandani)?
b. Je ni kitu gani kinakufanya ulale vizuri (usingizi mtamu usio na mang'amu ng'amu au majinamizi)?
c. Je, ni vitu gani vinakufanya uende kulala mapema - je ni usingizi
d. Ni kitu gani ambacho kinaweza kukupeperushia usingizi wako wakati uko tayari kitandani?
e. Ikitokea umekosa usingizi unafanya nini?
f. Je umewahi kupitisha siku kadhaa bila kulala na ni kitu gani kinakufanya usilale kabisa (ukiondoa mikesha ya misiba au kidini au kuparty) yaani upo nyumbani lakini hutaki kulala kabisa!
g. Je katika maisha ya mahusiano umezoea kulala na mtu mwingine kitandani au ukiwa kitandani hutaki mwenzako akuguse kabisa?
h. Vipi kuhusu wale ambao wana wenza wanaomka kabla yao je wanaonesha kujali kuwa bado umelala au wewe hujali mtu akianza kuwasha taa na kutafuta nguo asubuhi asubuhi na wakati mwingine kuamsha nyumba nzima?
i. Una ritual (tabia) ambayo unafanya kabla ya kwenda kulala kila siku (kunawa uso, kuoga, kusali, kusoma kitabu nk)?
j. Je ni wazo zuri kuwa na TV chumbani kwa watu wenye wenza au hata single?
k. Vipi kuhusu watoto kuingia chumbani - unawaruhusu au ni sanctuary of solace ambapo watoto kuingia lazima wafikirie mara mbili maana ndio muujiza wa uumbaji unakoanzia huko?
l. Nini kinakufanya uhame kitanda chako?

Una mawazo gani mengine kuhusu kitandani ambayo unaweza kutushirikisha.
 
ukiondoa shughuli nyingine za kitandani, kitanda kwa kawaida ni mahali pa kupumzika. Kitandanni mahali ambapo mtu anatakiwa awe na amani napo na kwa kweli ni mahali pa faragha. Na wote tunajua kuwa kitanda kwa kawaida ni mahali pa binafsi sana. Lakini japo watu wanachukulia kitanda kama kitu cha kawaida katika nyumba ukweli ni kuwa kitanda ndio rafiki yetu wa karibu sana labda kuliko hata ndugu wa damu. Ni shahidi wa furaha zetu, machozi, vicheko, faraja n.k kitanda ni yule rafiki asiye kuhukumu wala kujali umekosea nini kwani daima anakukaribisha.

Lakini kuna mambo mengi ambayo yanaweza kutufanya tufikirie kuhusu kitanda kwani wengine wanafikiria kitanda ni mahali pa kwenda kufanya mazoezi ya kuumba watoto. Kitanda ni zaidi ya hivyo. Hata hivo kuna watu wengine wakifikiria kitanda hukosa amani kwani kwao si mahalij pa kutulia ni mahali pa mawazo. Ni hapa wanapokesha usiku kuwaza na wengine ni mahali ambapo wanajua wakiamka asubuhi wanakuwa wamechoka kabisa mwili una maumivu. .

Vile vile japo kitanda ni mahali pa kwenda kulala kuna watu wana riituals za ajabu kabla ya kwenda kulala. Wengine hawana lolote wao wakisikia usingizi wanaenda kujilaza tu vile vile waliivyo wakati wengine huijandaa kwa kuoga na nimewahi kusikia habari ya baadhi ya wanawake ambao hujipara kwanza kabla ya kwenda kulala - ati wakishtushwa wasije kukutwa hawana make up! Lakini hebu tushirikiane hasa mawazo yetu kuhusu kitanda hasa tunapoenda usiku kwenda kulala.

A. Je unaamua kwenda kitandani kabla ya kupata usingizi (unaenda kutafutia usingizi huko kitandani)?
B. Je ni kitu gani kinakufanya ulale vizuri (usingizi mtamu usio na mang'amu ng'amu au majinamizi)?
C. Je, ni vitu gani vinakufanya uende kulala mapema - je ni usingizi
d. Ni kitu gani ambacho kinaweza kukupeperushia usingizi wako wakati uko tayari kitandani?
E. Ikitokea umekosa usingizi unafanya nini?
F. Je umewahi kupitisha siku kadhaa bila kulala na ni kitu gani kinakufanya usilale kabisa (ukiondoa mikesha ya misiba au kidini au kuparty) yaani upo nyumbani lakini hutaki kulala kabisa!
G. Je katika maisha ya mahusiano umezoea kulala na mtu mwingine kitandani au ukiwa kitandani hutaki mwenzako akuguse kabisa?
H. Vipi kuhusu wale ambao wana wenza wanaomka kabla yao je wanaonesha kujali kuwa bado umelala au wewe hujali mtu akianza kuwasha taa na kutafuta nguo asubuhi asubuhi na wakati mwingine kuamsha nyumba nzima?
I. Una ritual (tabia) ambayo unafanya kabla ya kwenda kulala kila siku (kunawa uso, kuoga, kusali, kusoma kitabu nk)?
J. Je ni wazo zuri kuwa na tv chumbani kwa watu wenye wenza au hata single?
K. Vipi kuhusu watoto kuingia chumbani - unawaruhusu au ni sanctuary of solace ambapo watoto kuingia lazima wafikirie mara mbili maana ndio muujiza wa uumbaji unakoanzia huko?

Una mawazo gani mengine kuhusu kitandani ambayo unaweza kutushirikisha.
kweli mwanakijiji kitanda ni sehemu nzuri sana kwetu sisi wanadamu na ndo maana hata mtu anapoanza maisha anaanza kununua at least kitanda kwanza.
Mwili wa binadamu ni kama mashine mwisho wa siku unaitaji kupumzika na raha ya kupumzika lazima iwe kwenye sehemu murua kitanda.
Kitanda pia ni sehemu nzuri kwa faragha zingine kama sex nk
 
Hiki kichwa cha Mwanakijiji sijui kinafanyaje kazi tu!

Binafsi nakipenda sana kitanda changu. Nakipenda kwa sababu kinanipa fursa ya kujiachia nipendavyo. Na kwa kweli kina matumizi kadha wa kadha.

Huwa nakitumia kulalia. Huwa nakitumia kujipumzishia. Huwa nakitumia kukalia na kusoma au kuangalia runinga. Huwa nakitumia kucheza.
 
Ndio maana wahenga walisema kitanda hakizai haramu.......ingawa hakibebi mimba vilevile........mmesahau tumizi moja........ni uwanja wa mapambano kwa wanandoa wengi......magomvi yote huishia kitandani
 
laiti kama vitanda vya gesti vingesema inayoshuhudia.....

kwangu mimi chumbani, kitandani kwangu ni sehemu ya kupumzika, hasa nikiwa na uchovu sana au kama sitaki ghasia za hapa na pale,

tv chumbani? hapana ni marufuku, tv yangu ni mwenza wangu tucheze tucheke tulale, naona kama tv inaharibu concentration, unless kama unapenda kuangalia porn movies tv chumbani ni sehemu muafaka. ingawa kuna kipindi fulani nilikua naishi na ndugu wengi walokua wakipenda mpira na mie sio mpenzi niliweka tv chumbani ili nisiwabughudhi na movies zangu, hali ilipojirekebisha nikaiondoa.

mm watoto kuingia chumbani huwa wanaingia, lakini ni pale ninapomtuma kitu fulani au ana shida labda anataka kuongea private, au anataka kuja kudeka si unajua, ila kabala hajaingia anatakiwa agonge asubiri mlangoni mpaka nimfungulie, akiona sijafungua anajua hatakiwi muda huo.

all in all chumbani, kitandani kwangu ndo sehemu niipendayo kuliko yote nyumbani kwangu, natumia kupumzika, kushiriki uumbaji, kukimbia madeni(hahahahahahah), ninapohitaji kuwa peke yangu kuwaza mambo kadhaa au ninapohitaji utulivu.
 
rnin14l.jpg


rnin103l.jpg
 
kwa heshima ya kitanda nasema "Kitanda hakizai haramu"


Mkuu hiyo ilikuwa mwaka 47, 2011 machale yakikucheza kuna kitu kinaitwa DNA hakikawii kumuumbua mtu na wengi wameshaumbuka katika nchi nyingi duniani. Kwa hiyo kitanda kinazaa haramu.




 
Last edited by a moderator:
Baada ya Bafuni (kuoga) ambayo ni moja ya burudani maridadi sana maishani
Kitandani ndio sehemu ingine ninayoienjoy nikiwa uchi kabisa, raha mstarehe.
 
Back
Top Bottom