Kitanda hakizai haramu ni kauli inayohitaji mjadala makini

Kitanda hakizai haramu ni kauli inayohitaji mjadala makini

Binafsi naiona kama ni kauli ambayo hutolewa na Wanawake ili kujitetea au kutetea
na kufunika uovu wao wa kuzaa na mwanaume mwingine wakati yupo ndani ya ndoa
au mahusiano yanayotambulika Rasmi. Pia hutumiwa na wanaume ambao ni dhaifu kwa
wake zao ambao hawana nguvu wala uwezo wa kuachana nae.

Kwa Mtazamo wangu mwanamke kutoka nje ya ndoa na akabainika wazi ni kosa ambalo
haliwezi kusameheka, hata kama utasamehe kama una akili timamu utaendelea kuteswa
na fikra za usaliti huo katika sehemu kubwa ya Maisha yenu.

Vipi unapokuja kubaini kuwa mtoto unayelea si damu yako ingawa amepatikana ndani ya
mahusiano au ndoa yenu?

Kwa mtazamo wangu KITANDA KINAZAA HARAMU.
Zinaa ni Haramu.

Zinaa inapatikanaje? Kazi kwako.

Je, Haramu inaweza kuzalisha Halali?

[emoji124] [emoji124] [emoji124] [emoji124] [emoji124] [emoji124]
 
Afadhali kitanda kijuletee mtoto, kuna majirani zangu huku kwetu. Baba alipata redundancy kazini. Malipo ya mafao walinunua kuwa kiwanja na kujenga nyumba ya nyuma na kuhamia.

Kazi ikawa kusimesha watoto. Mama alilikumbuka buzi la long time kabla hajaolewa. Ni zee lenye pesa sana hapa mjini.

Mzee alianza kufadhili milioni 3,4 mpaka 5. Watoto walikwenda shule na bila ya baba kwenye fridge haikukosekana.

Kumbe zee lilikuwa na LUKU. Mara mama anapata habari zee limepelekwa South Africa kwa matibabu. Hali ilikuwa mbaya na mzee alifariki.

Mama nae alishaambukizwa na kwa mapenzi mema alimgaia na mumewe pasi wote kufahamu.
Sasa hivi wote wako kwenye kitengo. Mzee anamlaani mke wake kila akiyakumbuka.

Wanaume mjue vyanzo vya pesa vya wake zenu. Mtaishia kuleta watoto wa watu au kunywa njugu.


Bikra ni muhimu jamani, sijui kwa nini sieleweki kwa kizazi hiki cha zinaa
 
Kitanda hakizai haramu kweli wazee waliona mbali tusiwapinge
 
Back
Top Bottom