Kitanda 6 x 6, Why m'banane?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kitanda 6 x 6, Why m'banane??

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Shark, Oct 19, 2012.

 1. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #1
  Oct 19, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,059
  Likes Received: 7,260
  Trophy Points: 280
  Wadau, nina rafiki yangu mmoja tunafanya nae kazi, leo kaja na story za ajabu kuhusu ulalaji wake kitandani, yeye na mkewe. Kaja kachelewa kazini, kisa kalala saa 10 ya usiku, baada ya kuuliza sababu ndipo akashuka na mzigo wa lawama dhidi ya mkewe.

  Anavyodai ni kua yeye anapenda kulala mwanzoni kabisa mwa kitanda, yaani anameza kama futi 2za mwanzo, sasa anacholalamika eti mkewe badala ya kuacha gap katikati la kama futi 2 hivi kisha akamalizia zile 2 za mwisho, ye hua anambana kabisa mpaka saa zingine anataka kudondoka. Mpaka saa zingine hua anamuuliza mkewe kama ile nafasi ya ukutani anamuwekea mtu mwingine aje kulala.

  Anafika mbali zaidi pale anapodai kua anashindwa hata kupumua usiku maana akivuta au kutoa pumzi basi kunakua na obstacle ya mtu karibu hivyo anapata tabu.

  Anazidi kukolezea kua hata wakati wa joto ambapo miili ikigusana inatoa jasho, bado mkewe anapenda kumbana kabisa badala ya kila mtu kulala kwa kujiachia.

  Anasema saa zingine akimaliza "shughuli", anapenda apate upepo na hewa ya kutosha ili kupumzisha mwili lakini mkewe bado atamganda.

  Nimeshindwa kumshauri maana sijaoa, ndio nikaileta hapa mnisaidie nimfikishie.
   
 2. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #2
  Oct 19, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,174
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  mwambie akue zaidi kindoa ataelewa kwanini mkewe anafanya hayo!
   
 3. COURTESY

  COURTESY JF-Expert Member

  #3
  Oct 19, 2012
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 2,018
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Wanawake wanaitaji kubembelezwa,kukumbatiwa kama watoto,sasa sijui huyu jamaa ako wa wapi unashindwa kumpa mke wako perfect care,unataka nani ampe!watu wengine bwana
   
 4. happiness win

  happiness win JF-Expert Member

  #4
  Oct 19, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 2,478
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Wakati mwingine mwanamke humkumbatia mumewe kama ishara ya kutaka mambo. Inawezekana huwa kiu yake haikatwi itakiwavyo!
   
 5. gobore

  gobore JF-Expert Member

  #5
  Oct 19, 2012
  Joined: Aug 17, 2009
  Messages: 730
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Anashindwa kutoa dozi ipasavyo huyo! Ukimvuruga vya kutosha unamkumbatia kidogo tu anachapa usingiz yani hata ukitaka kulala uvunguni atakua hana habari! Mwambie aongeze juhudi wala hatasumbuliwa
   
 6. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #6
  Oct 19, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,459
  Likes Received: 3,710
  Trophy Points: 280
  ni dalili hajafikishwa anapokwenda
   
 7. Catherine

  Catherine JF-Expert Member

  #7
  Oct 19, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 1,263
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  atakuwa anaenda wapi vile? Lol
   
 8. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #8
  Oct 19, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,459
  Likes Received: 3,710
  Trophy Points: 280
  mt. Kilimanjaro
   
 9. Philipo Kidwanga

  Philipo Kidwanga Verified User

  #9
  Oct 19, 2012
  Joined: Jul 12, 2012
  Messages: 2,063
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  mwambie ampe talaka ili abaki peke yake kitanda kizima sasa mtu asmkumbatie mumewe wanaume wengine bana kama mazoba.
   
 10. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #10
  Oct 19, 2012
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Kwa hakika bado hajajua kuwa kuna wanaume wengi ambao wanaota kupata anachokipata yeye,kumbatio linaonesha upendo haijalishi mtu ameridhika na mapenzi au hajaridhika.

  Siku akiacha kusumbuliwa utaona anakuja hapa na mada nyingine ooh!Mke wangu siku hizi hata kunikumbatia hataki yaani ni kama vile ana mwanaume mwingine yaani tukishapeana mambo tu anageukia kwake.

  Ridhika na ulichonacho maana wenzio wanakitafuta na wakikipata utabaki kulaumu.
   
 11. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #11
  Oct 19, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,187
  Likes Received: 563
  Trophy Points: 280
  Mafundisho ya ndoa yanahitajika sana maana hayo wala sio ya kuja kusema mbele za watu wala kumhadithia mwenzio
  Wengine wanalitafuta hilo kumbatio hawalioni yeye analalamika Blaki Womani, Kaunga, gfsonwin, snowhite hebu mpeni mafunzo ya nini maana ya ndoa huyu jamaa maana anaikosea ndoa maana yake
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #12
  Oct 19, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Sting huyo hampendi tu mke wake... Hilo sio yeye tu! Hata mtu yeyote unapokuwa na mtu usiempenda kiasi kwamba anakukera ule uwepo wake tu unaona kama unakuwa 'suffocated', hivi kweli mkeo/mmeo umuwekee mpaka wa kulala kitandani?

  Maeneo ya joto ina maana huwa wanakutana tu na kuto kumbatiana na wapenzi wao sababu tu ni joto? Hapa tatizo lipo kwa huyo rafikiyo na mkewe yupo sahihi kabisa. Na ilistahili umwambie kwa uwazi kabisa kuwa kama hampendi mkewe ni bora akawa wazi kuliko kumlaumu kwa vitu ambavyo sio msingi wala haki.

  Alafu inabdi awaelewe wanawake... Mimi mwenyewe mpenzi wangu tukimaliza hio shughuli nataka anikumbatie hata kama hatufanyi tena. Kuna raha, siri ni kum feel tu huyo mtu ambae unakutana nae kimwili... That is to say hata akipata mwanamke mwingine she will want the same thing.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #13
  Oct 19, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,187
  Likes Received: 563
  Trophy Points: 280
  AshaDii kama ulikuwa kwenye mawazo yangu
  hapo hakuna upendo hicho anachosingizia eti anamyima raha ya kupumua vyema eti anambana bana ni kujitetea ambako hakuna lolote
  mafundisho ya ndoa ni ya muhimu sana aise maana kwa mwelekeo huu mume analalamika hataki kukumbatiwa au ahisi jote wala ukaribu wa mke ni issue
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #14
  Oct 19, 2012
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,004
  Likes Received: 3,187
  Trophy Points: 280
  Hii ishu inakuhusu,,kwanini usifunguke tu kwamba na wewe?

  Kwanza unatumia jina feki, sa unaogopa nini?
   
 15. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #15
  Oct 19, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  Mapenzi mchezo wa ajabu saana, tena ni mbaya ukiuchukulia kama mcheza kamali... Kutokuwepo upendo juu ya mkewe kumemfanya asione "UPENDO WA DHATI" wa mke ila kuona kero ambayo anapta tokana na yale ambayo hataki kufanyiwa.

  Mie nawasihi sana kaka/baba zangu, kwa kiasi kikubwa nyumba na familia inajengwa na mke... Kama mke wako ana upendo wa dhati juu yako lakini akawa na madhaifu kama uvivu, kutojua kupika na the like; MWESHIMU sana huyo mwanamke... La sivyo utatumbukia mahala ambapo siyo kabisaaa! Ukawa na mwanamke bala wewe ukiwa kama kisima cha kumfikisha pale anapotaka na kile atakacho...

  Bahati mbaya saana huwezi fukuza upepo, kama hupendi, hupendi... BUT walau mtu akikupenda heshimu hayo 'Mapenzi' anayokupa.
   
 16. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #16
  Oct 19, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,187
  Likes Received: 563
  Trophy Points: 280
  AshaDii ndo maana huwa nikikukosa humu jamvini napata shida sana (mhhh usifikirie vingine)
  hakuna kitu kibaya kama unakaa na mtu unajua kuwa humpendi na mapenzi yameshuka ila humwambii na unamuona kero anapokuwa na wewe
  Huna mapenzi naye wala humfeel ila kumwambia inakuwa ngumu
  Huyo mtu ambaye unamsema kuwa akikukaribia unahisi kero ni mkeo sio mtu baki
  Huyo mtu ambaye anajaribu kukuonyesha upendo na kukukumbatia may be anakupa asante kwa ulichomfanyia au kukuonyesha kuwa wewe ni ubavu wake then badala ya kurudisha upendo huo unamgeuzia mgongo na kumuona ni kero ipo siku utalitafuta hilo kumbatio ulikose
  Au utamfanya aende mahali ambapo atakumbatiwa usiku mzima
  Hebu geuka muonyeshe upendo kama anaokupa wewe tena kwa kumkumbatia hata kama ni usiku mzima kama kumbikumbi ni sawa kwake
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. Bushloiaz

  Bushloiaz JF-Expert Member

  #17
  Oct 19, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 482
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Wanaume tunatakiwa kuwajua wanawake,kinyume na hapo ndio haya
   
 18. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #18
  Oct 19, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  hahaha! R' mbona unakuwa mwoga? Kuna ubaya ukipata shida kwa kunikumbuka? Lol :wink2: I am humbled, na usijali... I understand kabisa.

  Kuna totauti ya kuwa na mwanamke/mwanaume kama mwenza ambaye upo nae kwa vigezo kuwa anafaa kuwa mwenza na ile ya kusema upo nae sababu wa mpenda.

  Sijaelewa imekuwaje hao wamefika walipo... Majibu kama mda gani wameoana/ kama walioana wakipendana? na mengine mengi ambayo yanaweza towa picha halisia ya kuonesha tatizo lipo wapi...

  Katika mahusiano moja ya njia ya kusema/kujua kuwa mtu wako ana ku feel ni kiwango cha yeye kutaka kuwa karibu na yule ambae ni mpenzi wake, sio lazima kwa kufanya mapenzi, bali hata company.. Inapokuwa mpenzi wako anaona kuwa na wewe karibu ni kero; basi tatizo hilo ni kubwa sana, na ndio msingi wa matatizo meengi yatayofuata ndani ya mahusiano.
   
 19. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #19
  Oct 19, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,187
  Likes Received: 563
  Trophy Points: 280
  AshaDii hapo ndipo ninapofikiria kwa mapana na marefu yake. Je ndoa hiyo ipo kweli kama ndoa au ni kwa vile tuu wamebanwa na mazingira hawawezi kuachana either wana watoto ambao wakiachana ni issue au basi tuu jamaa anakaa nae kuficha ile aibu kuwa wameachana na mkewe
  Maana kwa hali halisi hakuna mapenzi hapo na inawezekana walilazimishwa kufikia hapo ndio maana amekuja kumuona ni kero
  Kitanda hata kikiwa cha nane kwa nane mke na mume hawawezi kila mmoja kulala kwenye kona eti kwa kuwa kitanda ni kikubwa wapeane nafasi ni mkeo ambaye anapaswa kuwa karibu na wewe apate na ajisikie upendo wako na apate ulinzi kutoka kwako kama mumewe
  Zaidi ya hapo eti kitanda ni kikubwa kila mtu alale kwenye kona yake hapo nachelea kusema ndoa imebaki doa sio ndoa
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #20
  Oct 19, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  Huwa anataka amwamngushie uvunguni mmewe
   
Loading...