Kitabu Kipya: Mwongozo wa Maisha ya Mafanikio

Makirita Amani

JF-Expert Member
Jun 6, 2012
1,781
3,074
Rafiki yangu mpendwa,

Huwezi kutoka nyumbani kwako na kwenda popote kama huna mwongozo unaoufuata.
Hata kama haujauandika mahali, unajua kabisa utapita wapi na wapi ndiyo ufike kule unakotaka.

Na hata unapokuwa njiani na kukutana na njia nyingine, hutahangaika nazo kwa sababu unajua njia sahihi kwako ni ipi, utaifuata hiyo na utafika ulikopanga kwa uhakika.

Swali la msingi kabisa kwako rafiki yangu ni hili; najua unayataka mafanikio kwenye maisha yako, lakini je una mwongozo sahihi wa kukufikisha kwenye mafanikio hayo?

Nimekuuliza swali hilo kwa sababu hapo ndipo watu wengi wamekuwa wanashindwa.
Wanayataka mafanikio, lakini hawana mwongozo sahihi wa kuyapata.

Kinachotokea ni watu kujikuta wakihangaika na kila njia au fursa inayopita mbele yao. Kila kipya anachosikia kinaleta mafanikio anahangaika nacho.

Mwisho anajikuta amehangaika na mengi, amechoka lakini hakuna matokeo mazuri ambayo ameyazalisha.

Hicho ndiyo ninataka kukuepusha nacho wewe rafiki yangu, kwa kuhakikisha unakuwa na mwongozo sahihi unaoufuata ili kuweza kufika kwenye mafanikio makubwa kwenye maisha yako.

Ninayo furaha kubwa kukufahamisha kwamba kitabu kipya cha MWONGOZO WA MAISHA YA MAFANIKIO kimeshakuwa tayari.

Kitabu kimechapwa na unaweza kukipata popote ulipo Afrika Mashariki.

Huenda umesoma vitabu na maarifa mengi kuhusu mafanikio.

Na huenda umeshaona siri za mafanikio ni zile zile, kujua unachotaka, kujitoa kweli kukipata na kuwa mvumilivu katika kukifanyia kazi.

Je unahitaji tena kusoma kitabu hiki cha MWONGOZO WA MAISHA YA MAFANIKIO?

Jibu ni ndiyo, kwa sababu kitabu hiki ni cha tofauti kabisa na vitabu vingine vya mafanikio.

Wakati vitabu vingi vya mafanikio vikikupa hamasa ya kukuonyesha inawezekana na unaweza, kitabu hiki ni mwongozo, kinakupa yale ya kufanyia kazi ili kweli ufanikiwe.

Hiki siyo tu kitabu cha kusoma na kujisikia vizuri kuhusu mafanikio, ukapata hamasa na ikaishia hapo. Bali ni kitabu cha kuenda nacho kwa maisha yako yote, kukitumia kama rejea kwenye safari yako ya mafanikio.

Ni kitabu kinachogusa maeneo yote muhimu kwenye safari yako ya mafanikio.

Kikianza na maana ya mafanikio, ambayo haijawahi kufanana kati ya mtu mmoja na mwingine.

Wengi wanahangaika kukimbizana na mafanikio ambayo siyo yao, kwa sababu hayaendani na maana yao ya mafanikio.

Kitabu kitakusaidia kutengeneza maana yako ya mafanikio inayoendana na wewe.

Halafu kuna ubatizo wa mafanikio, kitu muhimu mno ambacho watu wengi wanakikosa na ndiyo maana hawafanikiwi.

Ninachoweza kukuambia ni hiki, watu wote waliofanikiwa wamepata ubatizo wa mafanikio na watu wote walioshindwa wamekosa ubatizo huo.

Kitabu kitakuonyesha jinsi ya kupata ubatizo huo ili ujipe uhakika wa kufanikiwa.

Kuna swala la maamuzi, ambalo kwa wengi limekuwa mtihani. Wengi hufanya maamuzi kwa mazoea au kwa kusukumwa na hisia, kitu ambacho huwa hakileti matokeo mazuri.

Maamuzi unayofanya kila siku yanajenga au kubomoa mafanikio yako.

Kitabu kitakuongoza kufanya maamuzi bora kwako ili uweze kufanikiwa.

Falsafa ni muhimu sana kwenye maisha ya mafanikio. Kama huna unachosimamia basi jua chochote kitakuangusha. Wengi wanaishi falsafa wasizozijua na ambazo hazina manufaa kwao.

Kwenye kitabu hiki unakwenda kujifunza falsafa bora kabisa inayoendana na maisha ya mafanikio ambayo ni falsafa ya Ustoa (Stoicism). Hii ni falsafa ambayo wengi wa waliofanya makubwa hapa duniani wamekuwa wakiishi.

Kwenye kitabu utajifunza mazoezi muhimu ya kuiishi falsafa hii kila siku.

Kikubwa zaidi ni sheria 100 za maisha ya mafanikio unazokwenda kujifunza kwenye kitabu cha MWONGOZO wa maisha ya mafanikio.

Bila sheria ni rahisi mtu kuendeshwa na hisia ambapo matokeo yake huwa siyo mazuri.

Ili upate mafanikio makubwa kwenye maisha yako, unapaswa kuzijua na kuzifuata sheria 100 muhimu utakazojifunza kwenye kitabu.

Na mwisho kitabu kina shuhuda za watu mbalimbali walioshiriki changamoto ya siku 30 za kufanya kitu bila kuacha hata siku moja.

Hii ni changamoto tuliyoianzisha kwenye KISIMA CHA MAARIFA na ambayo imeleta matokeo makubwa sana kwa kila aliyeishiriki.

Kupitia kitabu utapata pia nguvu ya kujipa changamoto ya kufanya makubwa kwa upande wako.

Rafiki, hiki ni kitabu ambacho hupaswi kukikosa, maana ndiyo mwongozo sahihi kwako kufikia kwenye mafanikio makubwa ambayo unayataka kwenye maisha yako.

Maarifa hayo yote mazuri unakwenda kuyapata kwa gharama ya tsh elfu 20 (20,000/=).

Jipatie nakala yako ya kitabu cha MWONGOZO WA MAISHA YA MAFANIKIO leo hii ili ukae sawa kwenye safari yako ya mafanikio na usibabaishwe na yeyote.

Kupata kitabu hiki, wasiliana na namba 0752 977 170 na utaletewa kitabu kama upo Dar na kama upo mkoani utatumiwa kule ulipo.

Usiendelee kujichelewesha kwenye safari yako ya mafanikio, jipatie nakala yako leo hii ili uwe na mwongozo sahihi wa kufanikiwa kwenye maisha.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda sana.
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani.
 
Wasomaji wa vitabu tunafurahi tukioana vitu hivi japo vitabu vingi vya disaini hii almost vyote vina same idea don't do this don't do that blah blah blah

All in all kongore nyingi kwako mkuu mitano tena
 
Mafanikio ni nini?
Mafanikio yana maana tofauti kwa watu tofauti.
Maana ya mafanikio ni tofauti kwa kila mtu.
Kitabu kinakusaidia kuijua maana ya mafanikio kwako na upambane nayo, uache kuhangaika na mengine.
Karibu ujipatie nakala yako ya kitabu ili ujue maana sahihi ya mafanikio kwako na uifanyie kazi.
 
Nini maana ya mafanikio kwako? Pata jibu sahihi hapa ili uweze kufanikiwa.​

Rafiki yangu mpendwa,
Mafanikio ni dhana pana mno.
Hakuna maana moja ya mafanikio inayoweza kuwafaa watu wote.

Maana ya mafanikio inatofautiana kwa kila mtu.
Kwa sababu watu wanatofautiana, kuanzia uwezo, kusudi na hata ndoto, mafanikio hayawezi kufanana kwa wote.

Kwa maana rahisi kabisa, mafanikio ni pale mtu anapoweza kutumia uwezo wake wa ndani, kuishi kusudi lake na kufikia ndoto kubwa alizonazo.

Kwa maana hiyo, mafanikio yanaanzia ndani ya mtu na siyo nje. Hivyo mafanikio ya kweli kwa mtu ni yale yanayoanzia ndani yake.

Changamoto kubwa kwenye safari ya mafanikio ni watu kuhangaika na vitu visivyokuwa na tija kwao.
Watu wanakimbizana na mafanikio ambayo hayatoki ndani yao.

Watu wanakuwa wamehadaiwa na jamii ambayo imekuwa inawadanganya ukifanya hivi au kuwa vile ndiyo utakuwa umefanikiwa.
Wanapambana kweli kama walivyoambiwa, wanavifikia viwango hivyo walivyowekewa na jamii.

Lakini bado ndani yao wanakuwa na utupu mkubwa. Licha ya kuonekana wamefanikiwa kwa viwango vya nje, ndani wanakuwa hawana furaha. Hiyo ni kwa sababu mafanikio hayo hayajaanzia ndani yao.

Jamii ina ushawishi mkubwa sana wa kukuteka na kukuweka kwenye njia ya mafanikio ambayo haina maana kwako.
Jamii itakushindanisha na wengine na kukuonyesha kama hujawa kama wao basi una tatizo.

Usipokuwa na mwongozo sahihi unaoufuata kwenye maisha yako, utahangaika na mambo mengi lakini hutapata mafanikio ya kweli.
Utapambana kufikia mafanikio ambayo jamii imekuambia, lakini ndani yako hutapata ridhiko.
Na japo watu wanaweza kuona kwa nje umefanikiwa, ndani yako utajiona ukiwa mtupu na hujafanikiwa.

Ninayo furaha kukufahamisha kwamba kitabu kipya cha MWONGOZO WA MAISHA YA MAFANIKIO kipo tayari kwa ajili yako.
Hiki ni kitabu kitakachokufundisha dhana moja kubwa na muhimu sana kwenye safari yako ya mafanikio.
Dhana hiyo inaitwa; KIMBIA MBIO ZAKO MWENYEWE.

Mafanikio kwenye maisha ni mbio ambazo hazifanani.
Kila mtu ana mbio zake.
Unapoacha mbio zako na kwenda kushiriki mbio za wengine, unakuwa umechagua wewe mwenyewe kujipoteza.

Upo usemi kwamba tatizo la kushiriki mbio za panya, hata ukishinda unabaki kuwa panya.
Hivyo pia ndivyo ilivyo kwenye mafanikio. Kuhangaika na mafanikio ambayo hayajaanzia ndani yako, hata ukishinda bado unakuwa hujafanikiwa.
Mafanikio ya kweli ni yale yanayoanzia ndani yako mwenyewe.

Kwenye kitabu cha MWONGOZO WA MAISHA YA MAFANIKIO utapata nafasi ya kujitafakari wewe mwenyewe kwa kina, kujitambua, kujua kusudi la maisha yako na ndoto kubwa ulizonazo na kisha kupambana na hayo.

Wakati wengine wanahangaika na mafanikio yasiyokuwa na maana kwao, wewe unakuwa unayajua mafanikio yenye maana kwako na ndiyo unapambana nayo.

Usikubali kuendelea kupotezwa na jamii ili uendelee kubaki kwenye mbio za panya. Maana hata ukishinda mbio hizo, unabaki kuwa panya.
Jipatie nakala yako ya kitabu cha MWONGOZO WA MAISHA YA MAFANIKIO leo ili uanze kukimbia mbio zako mwenyewe na mafanikio utakayoyapata yawe na maana kwako.

Kitabu ni hardcopy na unaweza kukipata ukiwa popote ndani ya Afrika Mashariki.
Wasiliana na namba 0752 977 170 kupata kitabu chako leo hii ili uweze kupambana na mafanikio yenye maana kwako.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana.
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani.
 
Hongera Muuza Matumaini Dr Amani Makirita. KAZI na jitihada zako zinaonekana. Sambaza ujumbe wako kwa watu wengi zaidi wapate like wanachotaka ili nawe upate unachohitaji.
Fikiria jukwaa hili hapa la www.calipa.co.tz kuongeza WiGo na urahisi wa kuuza matumaini.
"CAS LIFE PURPOSE ACADEMY"- Limitless Growth
Rafiki yangu mpendwa,
Huwezi kutoka nyumbani kwako na kwenda popote kama huna mwongozo unaoufuata.
Hata kama haujauandika mahali, unajua kabisa utapita wapi na wapi ndiyo ufike kule unakotaka.

Na hata unapokuwa njiani na kukutana na njia nyingine, hutahangaika nazo kwa sababu unajua njia sahihi kwako ni ipi, utaifuata hiyo na utafika ulikopanga kwa uhakika.

Swali la msingi kabisa kwako rafiki yangu ni hili; najua unayataka mafanikio kwenye maisha yako, lakini je una mwongozo sahihi wa kukufikisha kwenye mafanikio hayo?

Nimekuuliza swali hilo kwa sababu hapo ndipo watu wengi wamekuwa wanashindwa.
Wanayataka mafanikio, lakini hawana mwongozo sahihi wa kuyapata.

Kinachotokea ni watu kujikuta wakihangaika na kila njia au fursa inayopita mbele yao. Kila kipya anachosikia kinaleta mafanikio anahangaika nacho.

Mwisho anajikuta amehangaika na mengi, amechoka lakini hakuna matokeo mazuri ambayo ameyazalisha.

Hicho ndiyo ninataka kukuepusha nacho wewe rafiki yangu, kwa kuhakikisha unakuwa na mwongozo sahihi unaoufuata ili kuweza kufika kwenye mafanikio makubwa kwenye maisha yako.

Ninayo furaha kubwa kukufahamisha kwamba kitabu kipya cha MWONGOZO WA MAISHA YA MAFANIKIO kimeshakuwa tayari.
Kitabu kimechapwa na unaweza kukipata popote ulipo Afrika Mashariki.

Huenda umesoma vitabu na maarifa mengi kuhusu mafanikio.
Na huenda umeshaona siri za mafanikio ni zile zile, kujua unachotaka, kujitoa kweli kukipata na kuwa mvumilivu katika kukifanyia kazi.

Je unahitaji tena kusoma kitabu hiki cha MWONGOZO WA MAISHA YA MAFANIKIO?
Jibu ni ndiyo, kwa sababu kitabu hiki ni cha tofauti kabisa na vitabu vingine vya mafanikio.

Wakati vitabu vingi vya mafanikio vikikupa hamasa ya kukuonyesha inawezekana na unaweza, kitabu hiki ni mwongozo, kinakupa yale ya kufanyia kazi ili kweli ufanikiwe.

Hiki siyo tu kitabu cha kusoma na kujisikia vizuri kuhusu mafanikio, ukapata hamasa na ikaishia hapo. Bali ni kitabu cha kuenda nacho kwa maisha yako yote, kukitumia kama rejea kwenye safari yako ya mafanikio.

Ni kitabu kinachogusa maeneo yote muhimu kwenye safari yako ya mafanikio.

Kikianza na maana ya mafanikio, ambayo haijawahi kufanana kati ya mtu mmoja na mwingine.
Wengi wanahangaika kukimbizana na mafanikio ambayo siyo yao, kwa sababu hayaendani na maana yao ya mafanikio.
Kitabu kitakusaidia kutengeneza maana yako ya mafanikio inayoendana na wewe.

Halafu kuna ubatizo wa mafanikio, kitu muhimu mno ambacho watu wengi wanakikosa na ndiyo maana hawafanikiwi.
Ninachoweza kukuambia ni hiki, watu wote waliofanikiwa wamepata ubatizo wa mafanikio na watu wote walioshindwa wamekosa ubatizo huo.
Kitabu kitakuonyesha jinsi ya kupata ubatizo huo ili ujipe uhakika wa kufanikiwa.

Kuna swala la maamuzi, ambalo kwa wengi limekuwa mtihani. Wengi hufanya maamuzi kwa mazoea au kwa kusukumwa na hisia, kitu ambacho huwa hakileti matokeo mazuri.
Maamuzi unayofanya kila siku yanajenga au kubomoa mafanikio yako.
Kitabu kitakuongoza kufanya maamuzi bora kwako ili uweze kufanikiwa.

Falsafa ni muhimu sana kwenye maisha ya mafanikio. Kama huna unachosimamia basi jua chochote kitakuangusha. Wengi wanaishi falsafa wasizozijua na ambazo hazina manufaa kwao.
Kwenye kitabu hiki unakwenda kujifunza falsafa bora kabisa inayoendana na maisha ya mafanikio ambayo ni falsafa ya Ustoa (Stoicism). Hii ni falsafa ambayo wengi wa waliofanya makubwa hapa duniani wamekuwa wakiishi.
Kwenye kitabu utajifunza mazoezi muhimu ya kuiishi falsafa hii kila siku.

Kikubwa zaidi ni sheria 100 za maisha ya mafanikio unazokwenda kujifunza kwenye kitabu cha MWONGOZO wa maisha ya mafanikio.
Bila sheria ni rahisi mtu kuendeshwa na hisia ambapo matokeo yake huwa siyo mazuri.
Ili upate mafanikio makubwa kwenye maisha yako, unapaswa kuzijua na kuzifuata sheria 100 muhimu utakazojifunza kwenye kitabu.

Na mwisho kitabu kina shuhuda za watu mbalimbali walioshiriki changamoto ya siku 30 za kufanya kitu bila kuacha hata siku moja.
Hii ni changamoto tuliyoianzisha kwenye KISIMA CHA MAARIFA na ambayo imeleta matokeo makubwa sana kwa kila aliyeishiriki.
Kupitia kitabu utapata pia nguvu ya kujipa changamoto ya kufanya makubwa kwa upande wako.

Rafiki, hiki ni kitabu ambacho hupaswi kukikosa, maana ndiyo mwongozo sahihi kwako kufikia kwenye mafanikio makubwa ambayo unayataka kwenye maisha yako.

Maarifa hayo yote mazuri unakwenda kuyapata kwa gharama ya tsh elfu 20 (20,000/=).

Jipatie nakala yako ya kitabu cha MWONGOZO WA MAISHA YA MAFANIKIO leo hii ili ukae sawa kwenye safari yako ya mafanikio na usibabaishwe na yeyote.

Kupata kitabu hiki, wasiliana na namba 0752 977 170 na utaletewa kitabu kama upo Dar na kama upo mkoani utatumiwa kule ulipo.

Usiendelee kujichelewesha kwenye safari yako ya mafanikio, jipatie nakala yako leo hii ili uwe na mwongozo sahihi wa kufanikiwa kwenye maisha.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda sana.
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani.
IMG_20220413_102439_985.jpg
 
Back
Top Bottom