Kitabu kipya cha Obama kinatarajiwa kutoka Novemba 17, nakala milioni 3 zimeagizwa kuchapishwa

Sam Gidori

Senior Member
Sep 7, 2020
165
414
A Promised Land.jpg


Kitabu cha Rais wa zamani wa Marekani kitakuwa mitaani siku chache baada ya uchaguzi wa Novemba 3, kwa mujibu wa taarifa ya Kampuni ya Penguin Random House mchapishaji wa kitabu hicho, iliyotolewa siku ya Alhamisi.

Kitabu hicho chenye kurasa 768 kilichopewa jina "A Promised Land" ama Nchi ya Ahadi, ni cha kwanza kati ya mfululizo wa vitabu viwili vinavyoeleza historia ya kiongozi huyo mweusi wa kwanza kuwahi kuliongoza taifa la Marekani.

Sehemu ya kwanza ya kitabu hicho kitakuwa kikieleza safari yake ya mwanzo ya maisha ya siasa, kampeni yake ya uraisi ya mwaka 2008 hadi kifo cha Osama Bin Laden mwaka 2011. Kitabu hicho kitaanza kuuzwa rasmi Novemba 17 katika lugha 25, ikiwamo Kihispaniola, Kichina, Kiarabu, Kifinland na Kivietnam.

Tayari watu wengi wameanza kuagiza kitabu hicho kiasi cha kufanya kampuni tanzu ya Penguin Random House, ya Crown, kuagiza kuchapishwa kwa nakala milioni 3 nchini Marekani pekee. Ili kukidhi mahitaji hayo makubwa, kampuni hiyo ya Crown inatarajiwa kwenda kuzichapisha nakala milioni moja nchini Ujerumani, kisha kusafirisha mzigo wa nakala hizo katika makontena 112 kwenda nchini Marekani.

Obama na mkewe Michelle wameuza haki ya uchapishaji wa nakala hizo kwa kampuni ya Crown kwa thamani inayovunja rekodi ya dola milioni 65 za Marekani, lakini wingi huo wa nakala haujafikia ule wa kitabu chake chenye jina "Becoming" ambacho kimeuza nakala zaidi ya milioni 8.1 nchini Marekani na Canada tangu kuchapishwa kwake mwaka 2018.

Kitu gani tukitarajie kutoka katika kitabu hicho kipya cha Obama?
Kitabu hiki kinaonekana kuchukua muda mrefu tangu kuanza kuandikwa kwake. Obama amesema kuwa ameanza kukiandika mara tu baada ya kuondoka White House mwaka 2016 na amekuwa akikiandika akiwa nyumbani kwake, Washington, DC., akiwa safarini na akiwa katika bustani ya nyumba yake, Massachussets.

"Hakuna furaha kama unayoipata baada ya kumaliza kuandika kitabu," Obama aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter.

"Nimetumia miaka michache iliyopita kurudia kutazama kipindi changu cha urais, na katika "A Promised Land" nimejaribu kueleza kwa uwazi kampeni yangu ya urais na kipindi changu ofisini: matukuo muhimu na watu waliohusika, nimeeleza mambo ambayo nimeyafanya kwa usahihi na makosa niliyoyafanya, pamoja na changamoto za kisiasa na kiuchumi ambazo mimi na timu yangu tumekabiliana nazo wakati huo - ambazo kama taifa bado tunaendelea kukabiliana nazo."



Obama anasema kuwa kitabu hicho kinatoa undani wa maisha yake na Michele wakati huo pia, kwa kuangalia mafanikio na changamoto walizozipitia katika safari yao, akisema kitabu hicho kiatoa mwanga wa jinsi ya kuponya taifa hilo lenye migawanyiko, huku akiamini kuwa kitawasaidia vijana kutambua nafasi zao katika kuifanya dunia kuwa sehemu salama zaidi.

Hiki si kitabu cha kwanza cha Obama. Kitabu chake chenye jina "Dreams From My Father" kilichochapishwa mwaka 1995 kiliuza zaidi ya nakala milioni 3.3 nchini Marekani na Canada pekee, huku kitabu chake kingine chenye jina "The Audacity of Hope" kilichochapishwa mwaka 2016 kikiuza nakala milioni 4.3.

Obama pia aliwahi kushinda tuzo ya Grammy kwa simulizi ya vitabu vyake vyote viwili, kama ilivyokuwa kwa Michelle katika kitabu chake cha "Becoming." Obama anatarajiwa pia kutoa toleo la sauti la kitabu chake "A Promised Land."

Tarehe ya kutolewa kwa toleo la pili ya kitabu hicho bado haijawekwa wazi.

Chanzo: New York Times
 
Ni matumaini yangu pia atakiri kuwa alimuua Gaddafi kwa nakosa na aimbe msamaha
Ewaah! Atuambie pia jeshi lao kipindi chake liliua wasio na hatia wangapi...duniani!

Na je, sehemu ya mapato kutokana na mauzo ya kitabu, atasaidiaje wahanga middle east!

Zile zama utopolo zimeisha!

Everyday is Saturday............................. :cool:
 
Nasubiri cha Bill Clinton atuambie kuhusu ile scandal yake na yule mrembo Monica Lewinsky.
 
Back
Top Bottom