Kitabu cha wageni msibani!!.Nani haruhusiwi kusaini?

Kitabu cha wageni msibani!!.Nani haruhusiwi kusaini?

Kile kitabu wanaandika maneno ambayo almost huwa ni ya faraja. Baadae familia huwa zinayasoma na yanawafariji. Unajua JK aliandika nini.....
Wanaaandika kwa mfano mimi naenda kuandika kwenye hicho kitabu cha Mengi. "Nimesikitika sana Mengi umetuacha,ulikuwa mtu muhimu sana. Nakumbuka ulipokuwa kwenye kamati ya Tacaids uliwahi kusema kwa nini mtu afe kwa raha ya dakika moja? Watu watumie condom,Poleni sana familia muendeleze yale mazuri aliyoacha Mzee DR Mengi"mimi Kwangu Masanja.
Asante kwa kunifahamisha hili
 
aisee kama ndio hivyo basi ni jambo la kuiga hata misiba yetu ya uswahilini halafu daftari lihifadhiwe vizuri na familia kama kumbukumbu
Wewe
Uswahili utakuta madeni tu mpaka mtalitupa maana mtu anaandika yaani we jamaa umekufa na deni langu wakati uliniahidi mwisho wa mwezi
 
Kile kitabu wanaandika maneno ambayo almost huwa ni ya faraja. Baadae familia huwa zinayasoma na yanawafariji. Unajua JK aliandika nini.....
Ahsante kidogo niulize huwa wanaandika Nini? Kumbe ni maneno ya faraja!
 
Ila kwa ninavyojua huku uswazi kitabu Cha hivyo kikiwekwa daah itakuwa balaa,unaweza kuta mtu kaandika " Mwajuma umekufa ila najua mi chausiku ndio kakuua kisa unagombea danga na mwanae usijali nitamnyoosha,pole Sana mama Mwajuma,it iz me x girls chata kubwa"
 
Huu ni utamaduni wa majuu, kwanza huko wahudhuriaji wachache, sii huku kwetu adi wanaotaka kula wali tu msibani wanasaini
 
Una saini na unakula hata bila kutoa mchango
Huu ni utamaduni wa majuu, kwanza huko wahudhuriaji wachache, sii huku kwetu adi wanaotaka kula wali tu msibani wanasaini
 
Huu utamaduni sidhani kama unatufaa. Kwenye jamii nyingi utaratibu ni mziri sana.

Kukiwa na msiba
1. Kuna daftari la rambirambi ambalo watu wanatoa fedha au vitu.

2. Jamii nyingine watu wanenda na vyakula

Sasa haya mambo ya kizungu ya kusaini na kupigwa picha naona kama tunapoteza kitu fulani ivi kizuri
Nadhani ni kutokana na mwingiliano wa makabila mbalimbali, wengine hupeleka vyakula, kuni na nguvu kazi na sio pesa.
Makabila mengine mwenye msiba ndo anagharamia kila kitu.
Wengine ndo hivo kutoa fuba jambo liende sawia ..

Ila kurahisha ndo linawekwa jitahu la kumwaga wino na kiasi cha rambirambi utakayo/uliyotoa.
 
Back
Top Bottom