Kama pilau huwezi, kuipika ikanona
upewe tui la nazi, na viungo kila aina
utapika upuuzi, walaji kukutukana
upewe tui la nazi, lilochujwa vyema sana
kutoa mafuta kazi, kama hujui namna
yatakutoka mashuzi, ubaki kugunaguna
Ni kazi tuiwezayo, ndo mana tunaifanya