Kiswahili ni lugha ya watu gani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kiswahili ni lugha ya watu gani?

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Barubaru, Jun 11, 2009.

 1. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #1
  Jun 11, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Kiswahili ni lugha ya watu gani?

  Risala enuka hima, sikae 'kataghafali
  N'na jambo 'takutuma, ubalegheshe suali
  Nipate jawabu njema, yenye amani na kweli
  Nauliza Kiswahili, ni lugha ya watu gani?

  2
  Lugha nyingi duniyani, zatamkwa mbalimbali
  Na zote ulimwenguni, zina wenyewe mahali
  Si Hindi Si Uzunguni, mewaumbia Jalali
  Jee hichi Kiswahili, ni lugha ya watu gani ?

  3
  Wakamba wana kikwao, lugha yao ya asili
  Na Wazungu piya nao, wana zao mbalimbali
  Na Wameru wana yao, wengine ni Wasomali
  Jee hichi Kiswahili, ni lugha ya watu gani ?

  4
  Wahindi wana Kihindi, kwa kabila mbalimbali
  Na Wanandi ni Kinandi, ndizo zao akuwali
  Wengine ni Wakilindi, wana yao ya asili
  Jee hichi Kiswahili, ni lugha ya watu gani?

  5
  Kuuliza Si ujinga, musinifanye jahili
  Nautafuta niuwanga, tuzinduwane akili
  Ndipo shairi hatunga, kubaleghesha suali
  Nielezwe Kiswahili, ni lugha ya watu gani?

  6
  Mara nyingi husikiya, kuwa hichi Kiswahili
  Hakina mtu mmoya, ambaye ni chake kweli
  Na wengine huteteya, kina wenyewe asili
  Ndipo ha'mba Kiswahili, ni lugha ya watu gani?


  7
  Masai ana kikwao, lugha ya tangu azali
  Na Mahara wana yao, wengine Mashelisheli
  Na Waluo lugha zao, Si sawa na Maragoli
  Jee hichi Kiswahili, ni lugha ya watu gani?
  8
  Na jamii wengineo, wana lugha mbalimbali
  Na kujuwa ya wenzao, ni kujifunza ya pili
  Lakini wana na zao, lugha za tangu asili
  Jee hichi Kiswahili, ni lugha ya watu gani?
  9
  Sasa ambalo nataka, kwa wenye kujuwa hili
  Wa Kenya na Tanganyika, na walo kulla mahali
  Nipani ilo hakika, tubalegheshe ukweli
  Nambiyani Kiswahili, ni lugha ya watu gani?
  10
  Miye mefikiri mno, kuamuwa jambo hili
  Na huona lugha hino, lazima ina asili
  Kwa sababu kulla neno, lina mwanzo wa usuli
  Ndipo ha'mba Kiswahili, hi lugha ya watu gani?
  11
  Na iwapo hivi sivyo, niliyyoamuwa hili
  Nionyeshani viliyyo, mubainishe ukweli
  Nijuwe ambavyo ndivyo, tutowane mushkili
  Kifunuke Kiswahili, ni lugha ya watu gani?
  12
  Na iwapo atakuja, wa kunijibu suali
  Namuomba jambo moja, twambiyane kiakili
  Tusionyane miuja, jambo nisilo kubali
  N'anambiye Kiswahili, ni lugha ya watu gani?
   
 2. Ngorunde

  Ngorunde JF-Expert Member

  #2
  Jun 11, 2009
  Joined: Nov 17, 2006
  Messages: 1,128
  Likes Received: 736
  Trophy Points: 280
  Barubaru ndugu yangu, nimelisikia swali,
  Naona una uchungu, ulioanzia mbali,
  Tangu enzi za ukungu, linakusumbua hili,
  Ila tuliza akili, tulione kiundani.


  Wakisema Kiswahili, "HICHI" ni cha watu gani,
  HICHI ni neno dhalili, tumia "HIKI" nadhani,
  Ila turudie swali, haswa ni cha watu gani,
  Nafikiri ni vigumu, kujua waanzilishi.


  Chazungumzwa Mrima, Mombasa hata Unguja,
  Pwani yote kinavuma, kwa mbwembwe na kwa lahaja,
  Na bara hata Musoma, kote wanakibwabwaja,
  Nafikiri ni vigumu, kujua waanzilishi.


  Kina mengi makusanyo, ya maneno mbalimbali,
  Wa'rabu pia Wayao, Wandengereko Wandali,
  Wote wametia yao, kwa lugha kuipa hali,
  Nafikiri ni vigumu, kujua waanzilishi.


  Kwa leo ninanyamaza, nitakuja tena kesho,
  Nitazidi kuyawaza, wote tupate fundisho,
  Ila usijenyamaza, kwa hii yangu mipasho,
  Endelea kuuliza, mwanzilishi wake nani?
   
 3. A

  AmaniGK JF-Expert Member

  #3
  Jun 11, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,101
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Mkuu Daktari naomba nije baadae kidogo na majibu.Shukrani
   
 4. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #4
  Jun 12, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0


  Daima unapotwanga, ni lazima kupepeta,
  Kutenga chuya na chenga, ungo utaukamata,
  Hapa ukishaboronga, mchele hataupata,
  Nambiyani Kiswahili, ni lugha ya watu gani?


  Ni lugha ya watu gani?, nambieni kiswahili.
  Hata mimi wa omani,Kuongea ni halali.
  Nasriyah wa yemeni, anatamba kila hali.
  Kiarabu chetu sisi, kiswahili ni cha nani?

  Kwa siri yake mtungi, aijuaye ni kata,
  Na nyumba bila msingi, utapasuka ukuta,
  Kila palipo na wengi, na mambo ya yatambata,
  Kiarabu ni cha kwetu, kiswahili ni cha nani?


  Tamati ndio akhiri, na jina langu ni hili
  Hamza wa Yusufali ,Al Naamani la pili
  BARUBARU mashuhuri, makazi yangu Qatari
  Kiarabu lugha yetu, kiswahili ni cha nani?


  Dr Hamza Yusuf Al Naamany(Barubaru)
  Doha. Qatar
   
 5. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #5
  Jun 15, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Nasubiri kwa hamu
   
 6. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #6
  Jun 25, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Hakika subra yavuta heri.
   
 7. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #7
  Aug 23, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli wewe ni mjuzi wa Lugha ya kiswahili. nakufananisha na Marhemu Shaaaban Robert.


  .

  sasa vp tena Dr unakikana kiswahili?
   
 8. Companero

  Companero Platinum Member

  #8
  Aug 23, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Barubaru nami nitarudi kama Malenga na majibu ya kishairi - ila kwa sasa naomba niweke jibu hili la kiinsha:

  Nukuu zifuatazo kutoka kwenye kitabu cha 'Swahili Origins' - na hasa utangulizi wake unaosema 'The Problem of Swahili Identity' - kilichotungwa na James De Vere Allen na kuchapishwa na East African Educational Publishers mwaka 1993 kinaelezea utete na utata wa wasifu wa waasisi, wamiliki na watumiaji wa Kiswahili:

  "For as long as written records exist, groups of Swahilis have described themselves, not only as Mombasans (Swahili waMvita), Pateans (waPate), Kilwans (waKilwa) or whatever, but also as Arabs (waArabu), Persians (waShirazi), or something else - even, in at least one place, Portuguese (waReno) - rather than as Swahilis, and many still do so. Indeed, it is doubtful whether even today most of the people would in all contexts accept the name Swahili" (p. 1).

  "Swahilis do share a language, though with considerable dialectal differences; but efforts to trace their origin and early history solely in terms of the source and development of this language are at best misleading. They also share a culture, though with great regional and some class variation. Yet ironically it is cultural differences which Swahilis themselves most often use to declare others 'not real Swahilis' (si waSwahili haswa). Traditionally the Swahilis themselves were certain that their territory extended somewhere near Kiwaiyu, in the north of Lamu...to Tunge, not far south of the Rovuma River ...and included the offshore islands along this coast and the Comoros . But in practice they often spilled over to the north, south or...west of these territories, while others interpenetrated them, so territory is of little use to define Swahili identity. This leaves us with 'shared historical experience'. On the face of it, there is no single, dramatic historical experience or series of experiences whose legacy enables Swahilis to define themselves as, for instance, the legacy of the American War of Independence permits Americans to define themselves...And yet the inability to discern any historical experience shared by all Swahilis is in large measure due to our failure to look at them as a historical people at all..." (p. 2)

  "For all that Swahili identity is elusive, it is only relatively recently that Western historians have questioned their historical importance, and that some have queried their very existence. The growth of this anti-Swahili prejudice is directly connected with the rise of an 'Arab Myth' of East African coastal history. Early European visitors to East Africa had no difficulty in recognizing a large and important Swahili community with its own rich culture, quite separate from and unrelated to a second group which comprised recent immigrants from Arabia and the Gulf...The Englishman Burton was the first to make a serious attempt to alienate the Swahilis from their history. But when he first visited East Africa in the 1840s and 1850s they were still too large a community for their name to be ignored; and he himself was too honest and acute an observer to omit certain facts and traditions about them which fit ill with their later image..." (pp. 2-3)

  "To most Western Scholars [in the 1800s], race (and in Africa , tribe) were paramount. It was of course, the era of the Hamitic Myth, and of countless other theories about genetic difference linked with Social Darwinism. Culture in Africa was seen as chiefly a function of race and tribe. Naturally the Swahilis, who had come to regard themselves in cultural rather than racial terms, and whose unity melted away once racial and tribal categories were superimposed upon them, were one of the first and most serious casualties of this way of thinking. They were regarded as inferior on two separate and not entirely compatible grounds: first, because they were 'cross-bred' Arab and African, a 'half-caste' or 'mongrel' race, and it was held that such races must be in some sense inferior to 'pure-bred' ones. Secondly, they were regarded as inferior in so far as the 'superior' Arab blood in their veins had been diluted by that of 'inferior' Africans..." (p. 3)

  "It did indeed seem best, from the viewpoint of many [colonial] adminstrators, that the Swahilis should simply disappear. And in adminstrative terms they very nearly did. But one or two problems had to be cleared up before this could happen. First there was the question of their history. The coast was dotted with stone-built ruins, including some very impressive ones, which the Swahilis claimed had been constructed by their forefathers. Burton had begun the process of disinheriting them from this legacy, a process which now gained momentum...The next problem was what to call those residual Swahilis who, for one reason or another, could not plausibly be called 'Arabs' and could not be fitted into any African tribal group either. A solution to this was found in the label 'Shirazi'. 'Shirazi' sounded in some obscure way, 'purer' and less African than 'Swahili', with some connotations of Persian ancenstry at some period in the remote past..." (p. 4)

  "To the assertion, 'There is no such person as a Swahili', there has always been a very simple retort: 'Who, in that case, developed the Swahili language ["a Bantu language [- "not a creole or pidgin or 'hybrid' in any other sense" (p. 12) -] with a proportion of Arabic loanwords" (p. 10)], and who wrote and read or sang Swahili poetry?" (p. 11)
   
 9. Companero

  Companero Platinum Member

  #9
  Aug 23, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Kiswahili lugha yetu, Wabara na Visiwani
  Inavuma hapa kwetu, hadi huko ghaibuni
  Utamu wake Kibantu, maneno yake yakini
  Imekopa vya Uarabu, navyo vya Jerumani

  Itaendelea...
   
 10. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #10
  Aug 23, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Wabara ni watu gani,
  wavisiwani ni nani,
   
 11. Companero

  Companero Platinum Member

  #11
  Aug 24, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Kiswahili lugha yetu, Wabara na Visiwani
  Inavuma hapa kwetu, hadi huko Ghaibuni
  Utamu wake Kibantu, maneno yake yakini
  Imekopa vya Uarabu, navyo vya Jerumani

  Uswahili ni utu, nakwambia bila matani
  Kiswahili chao watu, we chakwashia nini
  Enda kacheze upatu, tuachie si tughani
  Lugha yetu Ubuntu, kamwe haiwi upijini

  Kiswahili siyo kitu, sipojua kwa undani
  Tadhani ni Kisutu, shairi la Uswahilini
  Bongo ikiwa butu, tajuaje yake mizani
  Vina vyenye kutu, je utaviona upenuni

  Ukirioli siyo yakwetu, hii lugha amini
  Zitamu lafuzi zetu, lahaja nazo makini
  Tujifunze lugha yetu, na siache asilani
  Wete hadi Meatu, Utanzania uwe shani
   
 12. Companero

  Companero Platinum Member

  #12
  Aug 24, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Wabara ni Watanzania, Nao wa Visiwani
  Muungano wetu asilia, kabla ya Sultani
  Umoja ndiyo njia, dawa itibuyo Maskini
  Oh Mungu barikia , Tanzania iwe Amini
   
 13. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #13
  Aug 24, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Companero mkuu, hakika umejaribu
  Umetoka kijukuu, bila hata kuharibu
  Ahsante kwazo nukuu, za kutoka ughaibu
  Tuzidi kuutafuta, wapi ukweli ulipo.
   
 14. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #14
  Aug 24, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  campanero ujajibu swali. Unaona mwenzako ameweka bayana anauliza Kiarabu ni cha waarabu, kihindi ni cha wahindi. sasa unaposema kiswahili cha watanzania wa bara na visiwani. Vipi mombasa, lamu, pate ambako wanaongea kiswahili.

  MIE SIJALIZIKA NA JIBU LAKO NAONA KAMA UMEPONDANGA PONDANGA TU
  Pitia suala hapa

  nakufagilia Dokta wewe ni mahiri wa lugha ya kiswahili.
   
 15. Companero

  Companero Platinum Member

  #15
  Aug 24, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mkuu swali limejibiwa. Muuliza swali karidhika. Kiswahili cha 'Waswahili'. Wapwani na Bara. Na Visiwani pia. Lamu nako Lubumbashi. Mombasa hadi Mbarara. Hata huko Ughaibuni. Wabantu na 'Swahil'. Kiswahili lugha yetu.
   
Loading...