Kiswahili na Kingereza ni ushamba

prezdesho

Senior Member
Dec 30, 2015
150
78
Lugha ndiyo nyenzo muhimu popote pale duniani kujipatia maendeleo.Hakuna nchi duniani imeendelea kwa lugha ya mwenzake

Niajabu kumkuta mswahili akichanganya kiswahili na kingereza au mswali ndani ya jamii ya kiswahili akizungumza kingereza.Kwanza niuite ushamba na ulimbukeni wa lugha

Unafikiri usipo ithamini lugha yako unazani nani ataithamini usipopenda cha kwako unafikiri nani atakipenda.Hatuwezi kutumia lugha ya wenzetu tukaelewa mambo

Ajabu sasa mtu yupo chuo kikuu unamwambia zungumza hicho kingereza basi past,future,present zote kazichanganya kueleza tukio la sasa unajiuliza sasa huyu atajua kiswahili hawez kingereza ndiyo kabisa bora liende halafu unategemea tunawataalamu tanzania

Kasumba hili limeingia kwenye elimu ambapo baya zaidi.Leo hii wasomi wengi wanakariri na siyo kuelewa madhara yake swali hilo hilo alilokariri akapata mgeuzie kidogo utasikia sijafundishwa..Matokeo yake tunatoa injinia kwanza ukimpa ajenge baada ya mwez nyufa pili injinia hawezi kushindana na mchina mwenye cheti

Sasa tuendelee kutumia kingereza watoto wa shule za kata wa feli na watoto wa intenational wazidi kufaulu..lugha hii ifundishwe kama lugha nyingine ila mtoto afundishwe kwa lugha yake aelewe na siyo akariri
 
Mkuu

Inategemea na yule anae ongea kazaliwa wapi, kwa mfano mwanangu hivi sasa ana miaka mitatu, nimemzaa njee ya Tanzania, lugha ya kiswahili ndio tunayo ongea nyumbani, anafahamu everything na ana ongoea japo sio sana, kwa vile ameanza nursery akiwa na Miaka 2, ana peak English kuliko kiswahili, yaani tunashindwa kuelewana lugha kwa kiswanglish, yaani English na swahili.

Sasa mtoto huyu unataka kusema mshamba ? Nina watoto wa brother wangu wamezaliwa nje ya Tanzania, wanaongea kiswahili kama kazaliwa Tanzania, lakini hawawezi kuongea moja kwa moja bila ya kiengereza, hii ni kutokana ni lugha zao mama.

Hata ndani ya Tanzania hasa wale wenye uwezo na walio educated wanawafundisha watoto English kama mother tongue. Hakulia mazingira ya kuongea lugha mbili kwa pamoja.

Ila pia kuna kata bia ya visichana siku hizi wanaongea English kwa kuweka poz tu, ila mi naona kama wana jifunza, lugha bila ya kuongea huwezi ku learning
 
We fanya yako, so hata Jf ni ushamba maana imeandikwa kiswahili Na kiswa na kingereza! After all no 1 dictates what lingue I should use as long as its not academic formal comm
 
Mkuu

Inategemea na yule anae ongea kazaliwa wapi, kwa mfano mwanangu hivi sasa ana miaka mitatu, nimemzaa njee ya Tanzania, lugha ya kiswahili ndio tunayo ongea nyumbani, anafahamu everything na ana ongoea japo sio sana, kwa vile ameanza nursery akiwa na Miaka 2, ana peak English kuliko kiswahili, yaani tunashindwa kuelewana lugha kwa kiswanglish, yaani English na swahili.

Sasa mtoto huyu unataka kusema mshamba ? Nina watoto wa brother wangu wamezaliwa nje ya Tanzania, wanaongea kiswahili kama kazaliwa Tanzania, lakini hawawezi kuongea moja kwa moja bila ya kiengereza, hii ni kutokana ni lugha zao mama.

Hata ndani ya Tanzania hasa wale wenye uwezo na walio educated wanawafundisha watoto English kama mother tongue. Hakulia mazingira ya kuongea lugha mbili kwa pamoja.

Ila pia kuna kata bia ya visichana siku hizi wanaongea English kwa kuweka poz tu, ila mi naona kama wana jifunza, lugha bila ya kuongea huwezi ku learning
We umeandika kitu gani sasa? Utakua muhaya tu
 
Nadhan tz ni moja ya nchi zinazothamin sana lugha yake kwa hiyo post yako sio kweli kuchanganya inategemea kuna wakat maneno ya kiswahil ni magumu kurahisha mtu unachanganya, kwangu mm natofautiana na ww kama hukujua ni kwamba moja ya factor kubwa japo cjui kama kuna (empirical study imewah kufanyika) ni kwamba ubovu wa elimu yetu umechangiwa kwa kiasi kikubwa na kuipenda zaid lugha yetu wakati maarifa tunayatafuta kwa kutumia lugha za watu wengine hili ni kosa kubwa sana, masomo yalipaswa kuwa kwa kiswahili hata kama ni kigumu, au kama sio basi kiingereza kingekuwa pia moja ya lugha ya taifa, kama nigeria, kenya na nchi nyingine nyingi, watu wengi huwa wanasingizia lugha wakat wa presentations mbali mbali lkin ukweli ni kwamba watz wengi hawana content kichwan unamkuta dk. Kabisa au profesa anatoa presentation yan anasoma mstari kwa mstari, hata viongoz.
 
Code-switching mkuu siyo kwetu peke yake ni duniani kote. Ni zao la utandawazi ( wa kale na mpya). Watu wanachanganya misimbo na kuingiza lugha zenye hadhi zaidi kijamii (kwetu ni lugha rasmi za watawala wetu) wakidhani kuwa kwa kufanya hivyo nao wataonekana wana hadhi zaidi. Ndiyo maana bungeni hata Profesa Maji Marefu au Kibajaji nao utakuta wanatupia vimaneno vya Kiingereza ili kuonekana kuwa nao wamo. Hali hii huwezi kuizuia lakini ni kiashiria kizuri cha kuonyesha yupi ni mtawala na yupi ni mtawaliwa kijamii na hata kisaikolojia.
 
Lugha ndiyo nyenzo muhimu popote pale duniani kujipatia maendeleo.Hakuna nchi duniani imeendelea kwa lugha ya mwenzake

Niajabu kumkuta mswahili akichanganya kiswahili na kingereza au mswali ndani ya jamii ya kiswahili akizungumza kingereza.Kwanza niuite ushamba na ulimbukeni wa lugha

Unafikiri usipo ithamini lugha yako unazani nani ataithamini usipopenda cha kwako unafikiri nani atakipenda.Hatuwezi kutumia lugha ya wenzetu tukaelewa mambo

Ajabu sasa mtu yupo chuo kikuu unamwambia zungumza hicho kingereza basi past,future,present zote kazichanganya kueleza tukio la sasa unajiuliza sasa huyu atajua kiswahili hawez kingereza ndiyo kabisa bora liende halafu unategemea tunawataalamu tanzania

Kasumba hili limeingia kwenye elimu ambapo baya zaidi.Leo hii wasomi wengi wanakariri na siyo kuelewa madhara yake swali hilo hilo alilokariri akapata mgeuzie kidogo utasikia sijafundishwa..Matokeo yake tunatoa injinia kwanza ukimpa ajenge baada ya mwez nyufa pili injinia hawezi kushindana na mchina mwenye cheti

Sasa tuendelee kutumia kingereza watoto wa shule za kata wa feli na watoto wa intenational wazidi kufaulu..lugha hii ifundishwe kama lugha nyingine ila mtoto afundishwe kwa lugha yake aelewe na siyo akariri

Hoja yako ni ya msingi sana. Kujua lugha ni kuipenda na hasa inapokidhi matakwa ya mtumiaji. Maadalizi yetu sio sahihi kwa watoto wetu. Kosa halipo kwa walimu peke yao hata sisi wazazi tumekuwa na kasumba ya kuchanganya lugha. Hata tunapotumia lugha yetu ya kiswahili kuna maneno hatuyatumii kwa usahihi. Mfano wa neno linalotumiwa vibaya, ni neno "mwafaka". Utasikia mtu anasema ; afadhali ,umekuja muda mwafaka kwa sababu tu alikuwa anamhitaji. Muda mwafaka unatokana na maridhiano. Imepengwa tukutane saa 12.00 jioni. Akifika muda huo, ni sahihi kusema amekuja muda mwafaka na si vinginevyo.

Kukosoa kosa hili tunahitaji tuandae walimu wazuri wa kufundisha lugha kwa kufuata sayansi ya lugha na sayansi ya kufundisha.
 
Nakubaliana na michango ya wengine waliotangulia lakini naomba kuweka jambo moja sawa. Kwa mtazamao wangu, watanzania wengi hizi lugha mbili sio lugha zetu (Kiswahili na kiingereza) tuna makabila yetu ambayo ndio lugha mama ila kwa bahati nzuri Tanzania tuna lugha ya taifa (Kiswahili) ambayo inazungumzwa kote na inatuunganisha kama watanzania. Hii ni tifauti na nchi nyingi za kiafrika ambazo zinaunganishwa na lugha ya kigeni au kabila moja kubwa.

Katika elimu yetu tatizo hili linaonekana zaidi pale tunaposhuhudia ufaulu wa wanafunzi kwenye somo la kiswahili hauridhishi sana na wengi hawafanyi vizuri kwa sababu ni lugha tunajifunza tofauti yake tu ni kwamba, tunaizungumza sana tunapokua nyumbani. Tupo kwenye ulimwengu wa utandawazi na ushindani wa hali ya juu mno kimaendeleo, teknolojia. Unaweza kuimudu lugha vizuri kama unaitumia mara kwa mara na unapata nafasi ya kuizungumza kwenye maeneo mengine ukiachilia mbali shuleni, ndio maana watanzania wengi tumeenda shule lakini kiingereza bado ni tatizo.

Nakubaliana na wewe kwamba kuchanganya kiingereza na kiswahili sio jambo zuri japo inategemea na mazingira yenyewe.
 
Hoja yako ni ya msingi sana. Kujua lugha ni kuipenda na hasa inapokidhi matakwa ya mtumiaji. Maadalizi yetu sio sahihi kwa watoto wetu. Kosa halipo kwa walimu peke yao hata sisi wazazi tumekuwa na kasumba ya kuchanganya lugha. Hata tunapotumia lugha yetu ya kiswahili kuna maneno hatuyatumii kwa usahihi. Mfano wa neno linalotumiwa vibaya, ni neno "mwafaka". Utasikia mtu anasema ; afadhali ,umekuja muda mwafaka kwa sababu tu alikuwa anamhitaji. Muda mwafaka unatokana na maridhiano. Imepengwa tukutane saa 12.00 jioni. Akifika muda huo, ni sahihi kusema amekuja muda mwafaka na si vinginevyo.

Kukosoa kosa hili tunahitaji tuandae walimu wazuri wa kufundisha lugha kwa kufuata sayansi ya lugha na sayansi ya kufundisha.
Mwafaka au muafaka? Maana kiswahili kigumu
 
Back
Top Bottom