Raha na fahari ya Kuongea Kiswahili

Tuttyfruity

JF-Expert Member
Dec 3, 2017
2,405
6,281
Wakati naishi Tz kiswahili nilitumia kama means of communication. Sikuona umuhimu wake hata kidogo.

Sasa nipo nchi za watu ki ukweli hakuna raha nnayoskia kama kukutana na watu wanaongea kiswahili. Kingereza kinachosha jaman.

Kuna muda nataka nipumzishe akili, kingereza Kinahitaji kutumia ubongo mda wote kuchakata "tenses" hiyo kazi nani anaiweza ? Kha! Yani nikutane na wacongo, wakenya au Watanzania alafu tukichape kiswahili najiskia faraja sana.

Leo nilikua supermarket naongea na wifi yangu kiswahili pale pale wakapita wanaume wawili kusikia vile tunaongea basi wakatusalimia. Nikawauliza congo nyie? wakasema ndio, nikawaambia mimi nimetoka Tanzania. Kiswahili cha congo ni tofauti lakini generally speaking tunaelewana

Hua nawashangaa watu ambao wanaona kuongea kiswahili ni ushamba au kukosa elimu. Huo ni ulimbukeni

Nafanya kazi na mcongo na mkenya. Basi hua tunaongea lugha yetu pendwa basi tunajiona kama ndugu vile.

Mungu ibariki Tanzania mungu ibariki Afrika. Kiswahili kidumu milele na milele na kienee afrika yote na duniani kote kwa ujumla.
 
Upo sahihi kabisa Mkuu. Kuchakata English, kunachosha Sana akili. Bahati mbaya wengi tunadhani English, ndio akili, kumbe ni lugha Tu kama kichina, kivyetinamu, kigiriki na Kiswahili. Tupende Lugha yetu jamani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom