Kiswahili kipya kimeoza!!!!

Bin Faza

JF-Expert Member
Jun 12, 2013
502
191
Kwa Washwahili wenzangu,

Kwa wale waliondoka tanzania kwa miaka ishirini iliyopita, wakirejea leo wanashindwa kufahamu watu wanazungumzia nini, wanashindwa kufahamu magazeti yanaandika nini. nikisea hivi nakusudia kuna mabadiiko makubwa ya maneno ya kiswhailli, Sisemeni kwamba lugha yote imebadilika lakini kuna fungu kubwa la uwozo ndani ya kiswahili kipya.

Kiswahili asili hasa kimetokea zanizbar, kwasabubu katika wanaozungumza kishwahili wote katika afrika mashariki nakati, wanzibari peke yao ndio wanaozunmumza kiswahili kama lugha yao ya kwanza.

nimeshindwa kujuwa ni nani masuuli wa uchafuzi wa kugha yetu tamu sana, lakini nimesikia kuna watu kutoka tanganyika wanaitwa wataalamu wa kiswahili na wao ndio wanaobadilisha maneno, eti wanatoa maneno ya kiarabu na kuweka ya kiafrika, lakini wafanyalo ni kwamba kila mmoja katika wao huingiza maneno kutoka kabila yake

nahisi kuna haja ya kuandikwa kamisi jipya la kiswahili kwa kiswahili na safari hii lindikwe na maprofesa wa lugha kutoka zanzibar.
 
Nimekugongea LIKE mkuu Bin Faza lakini kuhusu watu ambao Kiswahili ni lugha yao ya kwanza si Wanzanzibari peke yao.
Tupo wengi ambao Kiswahili ni lugha yetu ya kwanza, watu wengi ambao wamezaliwa miaka ya 80 na 90 Kiswahili ni lugha yao ya kwanza, hasa wale ambao wamezaliwa na kukulia mjini. Tatizo kubwa kwa maoni yangu ni huu 'utandawazi' watu wanafikiri kuiga cha Mzungu ndo kufanikiwa.

Kuna mdau ameanzisha mada kuhusu 'tangazo la voda.' Tangazo hilo linamhusu mwalimu ambaye anachanganya lugha ya Kiswahili na lugha ya Kiingereza. Tusisahau kwamba lugha huzaliwa na kukua[kuenea]..matatizo kama hayo uliyotaja yanayotokea wakati lugha inapoendelea kuenea. Jambo la muhimu ni kudhibiti ukuaji na ueneaji wa lugha. Waandishi wa habari na vyombo vingi vya habari havizingatii jambo hili.
 
Tatizo hilo pia linakabili lugha ya Kiingereza. Kwa mfano, Kiingereza kinachozungumzwa Uingereza ni tofauti na kile kinachozungumzwa Marekani. Kiingereza kinachozungumzwa Australia ni tofauti na cha Jamaica. Kiingereza kinachozungumzwa Kanada ni tofauti na kinachozungumzwa Afrika. Tofauti hizo hutokana na umbali kutoka chanzo[asili] cha lugha. Sababu ya pili inayosababisha ni mwingiliano na lugha za wenyeji.

Tukirudi kwenye mada yetu kuhusu Kiswahili, Tanzania ni nchi kubwa yenye watu wa jamii mbalimbali. Kutokana na sababu hizo kunakuwa na tofauti ya matamshi ya Kiswahili ambayo si lazima tuyaite 'makosa.' Kama ujuavyo kuna aina nyingi za tunda la embe, hata hivyo embe ni embe. Naomba kutoa hoja.
 
Kiswahili lugha nzuri, bila kukuru kakara.
Kiswahili ni ufundi, na siyo kuungaunga.
Kiswahili lugha makini, sihitaji kujikomba.
Nawaza kwa Kiswahili, utotoni hadi sasa.

Thamani siyo samani, jua kutofautisha.
Sikiliza kwa makini, niyaseme ya maana.
Maneno yaloshamiri, ya Kiswahili fasaha.
Nawaza kwa Kiswahili, utotoni hadi sasa.
 
Agosti 8,

Kweli kwamba kuna fikra kwamba kila cha mzungu ni chema, zaidi kwa wale waliokuwa hawajawahi kutembelea nchi za ulaya au tuseme nje ya afrika

Sote tunajuwa kwamba lugha hubadilika kila jamii inapobadilika,hili kweli linapatikana katika lugha zote duniani. Mfano katika english ukisoma dictionary za 60s utakuna neno gay limefasirika kama furaha ...yaani siku hizo ukisema he is gay ilikuwa ikileta maana kama he is happy, joyful...........lakini leo ukisikia mtu anaitwa gay inamaanisha kitu kingine kabisa. Lakini hii ilikuwa natural process ya ukuwaji wa lugha pamoja na jamii.

Lakin unapopata watu wakajikusanya na kuamua kubadilisha maneno ya lugha ni kadhia tofauti sana. kama wanavofanya wataalamu wa kiswahili tz

Nakubali sana kwamba new generation ya Dar lugha yao ya kwanza ni kishahili lakini mwanzoni waliozungumza kiswahili kama ndio lugha yao ya wanza ilikuwa wazanzibari tu
 
lakini kuna watu wanalazimisha mabadiliko ya lugha mfano mmoja ni waingereza walikusanyana na kutaka kutowa maneno ya kifaransa katika lugha yao ya English, wakagunduwa nusu ya lugha itabadilika.

na wa pili ni wataalamu wa lugha wa tz wanataka kuondosha maneno ya kiarabu na kiingereza katika kiswahii hatimae tutakuwa na lugha mpya kabisa
 
waliamua wenyewe kwenda kwenye lugha nyingine si vibaya wakirudi wakute lugha nyingine pia
 
Lugha na Fasihi ni utambulisho wa jamii na ni msingi na mhimili wa Umoja na mshikamano wa jamii yetu. Utamaduni ni kielelezo cha utashi na uhai wa jamii yoyoyte.
 
Back
Top Bottom