Kiswahili kinaliangamiza taifa

Hoja imetoka kwa kukurupuka, ngoja na sisi tuoneshe mwitikio huo huo.
Uingereza wapo mataahira wa kutosha, nadhani kwa ujuvi wao wa Kiingereza wanafaa kuajiriwa kuliko wasomi wetu wanaozungumza brokeni Inglish...
Si eti eh?
sijui kama umenielewa..... au umekataa kunielewa,
 
kwa kuunga mkono alieanzisha hii thread kwamba "kiswahili kinaangamiza nchi" upande wangu nasema NDIO.
Ebu tujiulize kwamba tofauti na library zilizoko vyoni na shuleni, tanzania ina library ngapi za uma? honestly ni za kuhesabu. Tulipeleka msiba kijiji kimoja kenya mwaka 2001, sikuamini, kuna library kubwa tu kilichojengwa na wana kijiji wakanunua vitabu vichache, wakaomba serekali ikaongeza vitabu na kuajiri librarians pale. hili jambo lilinigusa sio siri! sisemi kwamba kwasababu wanaongea kingereza ndo maana waliweza kufanya hivi, hapana, lakini kwa bongo hii strategy isingefaa kwasababu wangapi watatumia facility kama hii kijijini tuseme hata mjini? vitabu vingi lazima vitakua vya kingereza sasa wangapi watasoma?
Tusijidanganye muamko unapatikana unapokua na information na muamko huo ndo unaskuma maendeleo! watanzania hatuna culture ya kusoma na tukisoma mara nyingi ni kuhusu michezo au udaku siku imeisha!!!
 
Kwa mawazo haya tuna kazi kubwa kufikia maendeleo, mbona hujiulizi wao walisaidiwa na nani mpaka wamefika hapo walipo, tuna kila kitu ila tumeamua kuwa masikini, misaada haisaidii kama hatuchukui hatua,
 
ndugu yangu unayo yasema huyajui, hata huko nje ya nchi uliko sijui ni wapi! mimi kwa sasa niko uholanzi, hawa jamaa ni kidachi kwa kwenda mbele, kingereza kinatumika mara chache saana katika sehem maalum zinazo husisha watu wa mataifa mengine, shule zote ni kidachi, wanashangaa kwa nini sisi tunasoma kwa lugha ya kiingereza!
nimekuwa mwalim najua namna walim wanavyo pata shida kufundisha kwa kiingereza, wanafunzi wanapata shida uelewa kwa sababu wanafikiria kwanza kwa kiswahili wanatafsiri ndo waanze kupata maana, ni kosa kubwa saana tulilotenda kuacha kiswahili kisitumike ktk mashule yetu.
Mara ngapi tumeshindwa kupata tafsiri halisi ya matatizo yetu kwa kikwazo cha lugha!
Halafu kumbuka kiswahili pamoja na kudidimizwa bado ni kati ya lugha kubwa duniani inayotumika tanzania, kenya, uganda, congo, rwanda, burundi, na nchi nyingi za afrika, tunge kithamini kingeweza kutuweka pazuri. Mataifa yote yenye nguvu sasa yanatumia lugha ya kwao!
kuthamini lugha ya kigeni ni ukoloni wa aina fulan kama tutakuwa makini kuchunguza, sisemi kwamba tuache kabisa lugha za kigeni, ni muhim kujifunza kwa sababu ya globalization ila tukumbuke siyo ligha zetu!
kunamsemo unasema "kitaka kumtawala mtu haribu, utamaduni wake" kumbuka lugha ni kiungo muhim saana katika kutunza utamaduni wa mahali, nafikiri wewe pia wa weza kuwa shuhuda kwa sasa Tz tusivyo kuwa na utamaduni wa kueleweka, uzungu si uzungu! uafrika si uafrika! watu kutaka kuishi kiingereza engereza! ndio kuliko badirisha style za watu kuongea, kuvaa, kutembea na tunathamin vyovyote wanavyo fanya wazungu kwa sababu tumedharau vya kwetu! kwa mfano utashangaa dada zetu siku hizi wanalazimisha kuvaa stockings na joto la dar lilivyo!!!!!! huku wenzetu wanavaa hivo kwa sababu ya baridi!!!!!!!!!
Ninasikitika mtu anaposisitiza tujifunze lugha za kigeni kwa gharama ya lugha yetu!
Nakipenda kiswahili lugha ya nchi yangu
 
Tanzania is not an island but we spend so much time and enrgy trying to make it one, acting like we dont need the rest of the word, trying to impose swahili like its the corner stone to mankind! really?!
Pole. Naona umelewa kabisa na Kiingereza na kwa bahati mbaya hata mwenyewe kinakutatiza. Ukweli ni kinyume chake; kwamba wasiokijua vema Kiingereza ndiyo wanakitetea sana na kukiabudu! Kiswahili kinaangamizwa na watu kama nyinyi na ni ukweli unaouma kwamba Kiswahili hakipigi hatua kubwa kwa kukosa msukumo wa kisiasa tu, hebu tafakari hata wabunge wetu wanavyokichakachua hadharani! Watanzania wengi wanadhani kujua Kiingereza ni kuelimika na ndiyo maana watu wasiojiamini huchapia kiingereza hata cha kuvunjavunja ili angalau waonekane wasomi. Historia itawahukumu. Binafsi sina shaka kabisa kwamba Kiswahili kinaweza kutumika kuanzia darasa la kwanza hadi chuo kikuu ili mradi kipate msukumo wa dhati wa kisiasa.
 
Mkuu umesema yote niliyotaka kuyasema. Inasikitisha kuona hata baada ya kujitawala kwa karibu nusu karne wapo watanzania wanaoshobokea Kiingereza! Sijui huyu masauni yuko katika nchi gani na upeo wa uelewa wake. Waswahili tunasema ukiona chaelea ujue kimeundwa; ndivyo ilivyo kwa Kiingereza. Historia inaweka wazi kuwa Kiingereza haikuwa mojawapo ya lugha kubwa hapo awali kama ilivyo sasa duniani. Waingereza kama yalivyokuwa mataifa mengi ya ulaya yalitumia kilatini na baadae Kifaransa kilikuwa lugha rasmi ya hao wanaoabudiwa na kina masauni hadi uamuzi mgumu ulipofanywa na kuamua kutumia lugha ya 'nyumbani' kwa ajili ya kufundishia. Waingereza waliienzi lugha yao na kufanya bidii ya kuikuza hadi hapa ilipofika. Si kweli eti tutapoteza hela 'kibao' au kupata hasara ya kukimbiwa na wawekezaji tukiamua kutumia kiswahili tu, bali hao wageni kwa shida zao watafanya bidii ya kujifunza ili wapate wanachokitaka! Wachina hawazungumzi Kiingereza lakini dunia nzima sasa inahaha kujifunza lugha yao ili waweze kufanya biashara nao. Si kweli kwamba lugha itakuwa kikwazo kwa wageni watakaotaka kushiriki nasi katika nyanja za kilimo, madini, biashara n.k. ati kwa sababu tu hatuzungumzi kiingereza; mbona hata wawekezaji wengi tu tunaowapata kiiingereza si lugha yao rasmi?
 

Hujakosea... kingereza kinanitatiza sana, hasa kwenye spelling ya maneno kama "enrgy"!!!
There you have it, I think i soothed your ego enough!!
kukomya, hivi vitu havihitaji maneno tu Tukimwaga mabillioni ya hela itawezekana baada ya miaka kama 50 hivi. naamini hela zipo hata kama asilimia karibia 30 ya budget ni donor funded, na mda ndo usiseme.. tunao mwingi mno!!
.........mtaalam, nichekie chekie spelling hapo kama vipi..........
 
kama ni ukoloni kwanini tusivue nguo tukatembea uchi kama babu zetu? tukaishi kwenye pango tukaachana na magari tusitumie tena sahani, sufuria wala vijiko, tusisikilize mziki wala kuangalia tv, jf ifungwe, hatutaki tena computer na internet zao, madawa kama ARV hatutaki tena, treni ya dar irudishwe ilikotoka, bandari ifungwe na meli ziondoke na makontena yao ili turudi kuwa waafrika halisi na mila zetu?!!! zote hizi ni za wazungu au kuna za waafrika kati ya hivyo nilivyotaja?!
 
Hydogen achana nao nao bwana usinipotezee hewa yangu nzuri ya hydrogen bure bure tu hapa tuko watu mchanganyiko ambao ht ungekaa nao darasani wangekuwa wanapata sifuri kila siku lakini huku kwenye mitandao wanajiona wajanja wanabwabwaja tu bila reference wajitahidi tu kututengenezea search engines za kiswali pia na watafute rights za kutafsir google, yahoo, na engines zingine kwa kiswahili. Hawajui ht duni inaelekea wapi wao wamepiga about turn wanaelekea kwa mababu
 
Hydogen achana nao nao bwana usinipotezee hewa yangu nzuri ya hydrogen bure bure tu hapa tuko watu mchanganyiko ambao ht ungekaa nao darasani wangekuwa wanapata sifuri kila siku lakini huku kwenye mitandao wanajiona wajanja wanabwabwaja tu bila reference wajitahidi tu kututengenezea search engines za kiswali pia na watafute rights za kutafsir google, yahoo, na engines zingine kwa kiswahili. Hawajui ht duni inaelekea wapi wao wamepiga about turn wanaelekea kwa mababu
 
Waafrika tukitaka kutozarauliwa tuwe tuinafikiria kiumakini, na sio kijuu juu tu.TUWE MAKINI WA KUFIKIRI !!Wewe hapa mtanzania chakula unachokula je kinalimwa na mtu anayeongea kiingereza?Kiingereza ni lugha tu, wako wengi ulaya wanaongea kiingereza kizuri tu lakini hawana ujuzi wowote.Cha muhimu ni kujiuliza, lugha gani itaniwezesha mimi kumudu mazingara yangu? Kama upo kijijini,kama asilimia 80 ya watanzania ni hizo lugha zetu za asili sio kiingereza. Uliza, wajapani, waholanzi, waitaliani, wakorea,wanatumia kiingereza mashuleni kwao? Je wamalawi, waganda, wazambia wanaotumia kiingereza wametuzidi nini sisi tunaotumia Kiswahili kwa ‘maendeleo’?Tujenge maarifa kwa kutumia lugha tunazozifahamu kwanza, maarifa haya tutayakumbuka na kuyatumia kinadharia ipasavyo kama tutajifunza katika kiswahili au hata katika kilugha chetu ambacho tunakijua moyoni!. Na mimi naunga mkono Kiswahili kifundishwe mpaka chuo kikuu, wewe fikiria, tukianza kutumia Kiswahili kuanzia sekondari, ni watoto wangapi watafaulu? Na ni vipaji vingapi tunavyopoteza kila mwaka kwa sababu vijana ambao wana akili nyingi tu lakini lugha tu ndio inayowakwaza?Ninasema tukitaka kuwa na maisha bora lazima tufanye maamuzi magumu, tuangalia ukweli kiundani sio kijuu juu tu, au kufuata mkumbo, kama hatujipendi nani atatupenda? Kama tunadharau lugha zetu nani atatuheshimu?Kujiamini kunaanzia kwenye vitu vidogo vidogo tu, kama hujiamini haka kwenye lugha yako tu, sidhani utaweza kujiamini kufanya mambo makubwa.Sisemi tusijifunze kiingereza, ninachosema ni kwamba, kiingereza kitumiwe kama somo tu, lakini kiswhili kiwe ndio lugha kuu ya ufundishaji.
 
Hawa jamaa wenye mawazo mgando wanazunguka hapo hapo sasa kama wanaelekea kwa mababu si na kila kabila lifundishe kilugha shule za msingi na sekondari na kila kabila liwe na chuo kikuu chake si ndio watafaulu vizuri zaidi? nani kawaambia huko vijijini ni mabingwa wa lugha ya kiswahili? Tumetoka huko tukaunganishwa kama nchi kwa kiswahili na lazima tutoke hapo tukaunganishwe kama dunia moja kwa kiingereza. Tatizo hamjibu hoja mnapigapiga maneno tu kama wanasiasa vitabu mtaandika mpaka vya kina Einstein, Gauss, Newton, nk? hao ma professor wenu wataenda kutoa mihadhara ya kimataifa? wataenda kutafuta kazi nje ya nchi? acheni hizo
 

Hivi lile panga langu liko wapi nianze kuwapunguza wazembe wa kifikra kama huyu Masauni?
 
Heshima mbele!
Wanajamvi! Hapanshaka yoyote kuwa nyerere alitoa mchango mkubwa sana katika kukieneza Kiswahili, naam sote kwa njia moja au nyingine tunashiriki katika kukieneza Kiswahili lakini nyerere kwa kutumia nafasi yake ya Urais alifanya zaidi yetu.

Ni nini hasa kilichomfanya nyerere ajikite kwenye kukieneza Kiswahili?, tafadhali mwenye welewa atujuze

*Nilipitia kule jukwaa la lugha nikakutana na hii:
DHEHEBU LA PILI

2) "Kiswahili Sanifu": dhehebu hili lilianza kuundwa kati wa karne ya kumi na tisa na karne ya ishirini. Sababu ya kuundwa dhehebu kama hili ni ile haja ilyokuwepo ya watu (Waswahili) wote kutoka Lahaja mbali mbali waweze kukutana na waelewane katika uzungumzi au utumiyaji wa Kiswahii ambao utakuwa ni sahali kwa wote.

Fikra hii iliungwa mkono na wataalamu wengi wa Kiswahili na ikaanza kusambaa. Ndiyo wakati huu huu piya, Wanamisheni (Christian Missionaries) waliokuwa na hamu kubwa kusambaza ukiristo miongoni mwa Waswahili, na kufunguwa njiya kwa wakoloni kuingiya Kenya, kama ilivyokuwa kawaida ya wakoloni kabla ya kuja wao mwanzo hutuma wanamisheni kufunguwa mlango kwa jina la yesu kristo, walichangiya katika usambazaji wa Kiswahili.

Wanamisheni wenyewe walikuwa ni wageni katika lahaja yoyote ile ya Kiswahili. Kwa hivyo waliona kuwa wakilemeya upande mmoja watakosa wafuwasi wa pande nyingine, basi nao wakaunga mkono fikra kama hii. Na kwa kuwa wao walikuwa na uwezo mkubwa wa kifedha na kitaaluma mbali mbali, basi waliweza kwa muda mfupi sana kubuni uwandishi wa Kiswahili kwa kutumiya dhehebu hili jipya la "Sanifu".

Vitabu vingi vikaanza kuandikwa, ambapo lengo kubwa kwa upande wa wanamisheni ilikuwa ni kutafsiri Bibliya kwa lugha ya Kiswahili, hasa baada ya kuona kuwa Kiswahili ilikuwa ni lugha inayoeneya kwa haraka na kuzungumzwa na watu wengi sana, hata wale wasiokuwa Waswahili, walipendeleya kutumiya Kiswahili".
 
Baba wa taifa yeye alisoma kwa kiingereza akasoma na akakijua,kwanini baada ya kupata madaraka akaamua lugha ya kiswahili iwe ya kufundishia na iwe ya taifa,kwanini? Au hakutaka sisi wengine tusiifahamu lugha hiyo,basi hata ingekuwa ndo lugha rasmi ya taifa lakini ya kufundishia ingebaki lugha ya kiingereza.

Kiswahili ndio chanzo cha umasikini Tanzania kwani kuna vijana wengi wamekosa kazi kwa kushindwa kuzungumza kiingereza vizuri.
na hata hawa wasanii wetu wataimba mno sana lakini mwisho wa siku hawatafika mbali sana,ingawaje diamond ananishangaza,huyu jamaa angekuwa na uwezo wa kuchanganya kalugha kama V MONEY angefika mbali sana.

USHAURI: Naomba serikali ifanye lugha ya kufundishia iwe ya kiingereza toka chekechea mpaka elimu ya juu.
 
Mawazo mgando. Mbona nchi nyingi hazitumii kiingereza na wamepiga hatua kubwa kimaendeleo hata kushinda wanaotumia kiingereza? Tatizo lako ni inferiority complex. Pole sana.
 
Kama ndivyo basi Uganda wangekuwa ndo superpower hapa East Africa!! By the way, wale akina Awilo, Kanda Bongoman, Pepe Kale, Amitabh Bachchan, Aamir Khan na wengine ambao walikuwa wanawabamba na wanaendelea kuwabamba; nao walikuwa wanatumia Kiingereza?

In short, sisi ni maskini kwa sababu hatujui chanzo cha umaskini wetu ni nini!!
 
Kama ulitegemea kingereza kikuletee msosi hapo ulipokaa endelea kusubiri
 
Eti ni kweli zamani alikuwa na Tv peke yake anaona taarifa za habari halafu asubuhi anawaambia watu ameota sehemu flani kuna kitu kinaendelea?? (au ni stori za mtaani tu
)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…