Kiswahili kinabanagwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kiswahili kinabanagwa

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Kipilipili, May 22, 2011.

 1. Kipilipili

  Kipilipili JF-Expert Member

  #1
  May 22, 2011
  Joined: May 25, 2010
  Messages: 2,207
  Likes Received: 478
  Trophy Points: 180
  Kiswahili kinabanangwa na kuvizwa hasa na wasomi ambao huchanganyanya lugha ya kiswahili na kingereza makusudi wakijinaki kuwa wao ni wasomi,jamani eleweni kuwa kujua kingereza haimaanishi kuwa mtu amesoma,kingereza ni lugha yenye dhima sawa na nafasi sawa kama kiswahili,kidigo au kibondei.utasikia mtu anasema" i wish ningekuwepo nimcheki alivyo shine".eti huyu ni mswahili mzawa asiejua kiswahili kiasi cha kushindwa kutafuta kiswahili cha i wish,check,shine.wasomi wengi wana mawazo mgando na fikra potofu.kidumu kiswahili milele daima!
   
 2. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #2
  May 22, 2011
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,739
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Sio suala la usomi.
  Kuna maneno mengine ambayo ukiyatafsiri kutoka kiingereza kwenda kiswahili, maana inapoteza mvuto. Na kuna wakati msikilizaji anaweza kuelewa vizuri zaidi ukimchanganyia lugha kuliko kuweka kiswahili peke yake. Kiswahili ni kigumu, na kipo nyuma kwenye mambo mengi.
  Kama wewe unajua kiswahili, naomba unitafsirie sentensi hizi kwa kiswahili. Na uniambie umechukua muda gani kuzipata tafsiri hizo.
  1. Can you tell me the recipe for apple pie?
  2. How can I make a tropical juice from carambola and java plums?
  3. My smartphone is using android and not symbian system.

  Kama utatafsiri kiusahihi katika muda wa dakika kumi, basi sentensi hizo ni rahisi kuongea kwa kiswahili.

  Nakupa siku nzima.

  Kidumu kiswahili kigumu!
   
 3. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #3
  May 22, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,259
  Trophy Points: 280
  sio suala la kujidai,manake hata wakati wa kusoma sekondari (o-level, manake sijui hata kiswahili chake), unajikuta english language una A, kiswahili una C. Kiswahili ni kigumu sana na tukiongea kiswahili kitupu sidhani kama tutaelewana,hasa kama tunaongelea sayansi ngumungumu. ni kujitahidi,lakini tusiwacheke wanaotohoa mkuu.
   
 4. Kipilipili

  Kipilipili JF-Expert Member

  #4
  May 25, 2011
  Joined: May 25, 2010
  Messages: 2,207
  Likes Received: 478
  Trophy Points: 180
  Kiswahili c kigumu ila waswahili ndio wagumu.hudhan kuwa kwa vile wamezaliwa wanaongea kiswahili basi wanajua kiswahili.ni lazma tujifunze kiswahili ili tuwe weledi.suala la tafsiri ni kwamaa hiyo ni taaluma inayojitegemea na c kila mtu anaweza kufanya,hvyo kuweka misamiati ya kisayans ya kingereza haimaanishi kua kiswahili hakina msamiati wa maneno hayo.ntakupa mfano maneno ya kingereza"download" na "upload" yanamaana ya KUPAKIA na KUPAKUA.maneno haya yamekuja baada ya ujio wa ngamizi{computer}.neno kama ANTIBODY lina neno la kiswahili FINGOMWILI.ukiangalia kiswahili ni tajiri ila waswahili wenyewe ni masikini wa lugha
   
 5. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #5
  May 25, 2011
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,739
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Hebu angalia hii sentensi iliyotokana na kiswahili ulichoniwekea hapo.

  "Nimeshindwa kupakua lile faili la fingomwili, nafikiri ngamizi yangu ina matatizo."

  Hivi kweli unaweza ukaongea hivi halafu watu wakuelewe?

  Ndio maana pale juu mimi nimesema kiswahili kipo nyuma kimaendeleo. Hao wanaotafsiri speed, (mwendokasi) yao ipo nyuma ukilinganisha na mabadiliko ya kiteknolojia na kisayansi. Sisi kama watumiaji wa kawaida wa kiswahili, tunafahamu vitu vipya kwa lugha ya kigeni kabla hatujafahamu kwa kiswahili, ni kwanini?

  Pale juu nilikupa sentensi zenye maneno ambayo ni kiingereza cha kawaida-"recipe" , "apple pie", "tropical juice", "carambola" , "java plums", "smart phone". Haya wala sio ya kisayansi.

  Carambola ni matunda yapo pwani na zanzibar (sijui kiswahili chake), ona picha yake hapa:
  http://www.gastronomiavasca.net/glosario-file/917/Carambola.jpg , na java plums ni mazambarao. http://t0.gstatic.com/images?q=tbn:ANd9GcSK2lPtf4-jDGBUjoMrLiq6okqgpk9pid_tlfERrXwg8ENz__JkDA

  Maneno kama android na symbian, haya ndio ambayo ni ya kisayansi.

  Sasa ndugu yangu, ni kweli tukipende kiswahili, lakini lazima tukubali, ni KIGUMU!
   
 6. M

  Mtu Mmoja JF-Expert Member

  #6
  May 25, 2011
  Joined: Mar 18, 2010
  Messages: 596
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  hiyo yote ni kwa sababu ya kukiendekeza kiingereza

  kichina ni kigumu kuliko kiswahili lakini kwa kuithamini lugha yao, kuna maprofesa kule hawajui hata kutamka good morning! na wachina leo hii wanatesa karibu kila eneo, sio teknolojia, biashara, uchumi, siasa, sanaa nk

  kwa kweli kiingereza ni moja ya factors zilizotudumaza sana
   
 7. Kipilipili

  Kipilipili JF-Expert Member

  #7
  May 25, 2011
  Joined: May 25, 2010
  Messages: 2,207
  Likes Received: 478
  Trophy Points: 180
  Nakushangaa na ntaendelea kukushangaa,tatzo ni kwamba wewe ni muhafidhina{consevative},mdhanifu{idealist} na una mawazo mgando kuhusu kisw{samahan cjakutukana}.umeweka sentens hapo juu halaf ukasema kua ukiongea hvyo watu hawatakuelewa,nadhan unakubal fika sasa kuwa kumbe kiswahili kinacho msamiati wa kutosha lakini waswahili hawakijui sawia kiswahili kias ambacho hukiona kigumu{ikiwemo wewe}.kwa hiyo hoja sasa ni kueleweka na sio tena kiswahili hakina msamiati toshelevu.nikushauri tu uwasiliane na wataalam km una uvulivuli wa mambo na si kuhukumu lugha kuwa ni ngumu.kumbuka kiswahili kina mlea binaadam tangu kuzaliwa kwake hadi kufa mf.ni ushairi simulizi hasa kipengele tanzu ya nyimbo.kuna nyimbo za kuzaliwa mtoto,nyimbo za kubembeleza mtoto"oooh mtoto oooh,babio kenda mjini kafungwa,kafungiwa debe mbili za mpunga...",nyimbo za mtoto ajifunzapo kutembea"...kasimama peke yake,amuonesha mchumba wake...",nyimbo za jando na unyago,nyimbo za harusi,na nyimbo za mazishi.ukiangalia mtiririko huu utaona kuwa lugha inabadilika kutegemea hitajio na mabadiliko ya binadam,nacho kiswahili kimefata mkondo huohuo.kutokujua kwetu kiswahili,tusihukumu kiswahili kigumu bali sisi ndo vchwa maji wa kisw.
   
 8. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #8
  May 25, 2011
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,739
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
   
 9. S

  Senior Bachelor Member

  #9
  May 28, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 86
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana kabisa na pangu Pakavu, na kiasi na Nanren. Nadhani alichokuwa anamaanisha mwanzisha mada sio kuwa kila neno lililopo kwenye kiingereza (au lugha nyingine yoyote) basi lina tafsiri yake kwenye kiswahili, na kuwa watu watumie. Hapana. Na alivyojibu Nanren kwa kutoa maneno/sentensi ili zitafsiriwe sio sahihi. Je nikimwambia Nanren "kitawa" au "kitalolo" (vyakula vya kichagga) anitafsirie kwa kiingereza akashindwa itakuwa sababu ya kusema kiingereza ni kigumu? Lugha ni sehemu ya utamaduni na ndio maana kuna kutohoa maneno ya lugha moja na kuyatumia kwenye lugha nyingine.

  Nilivyomuelewa Pangu Pakavu, na nakubaliana naye, ni kuwa kuna wazungumzaji wanajifanya wao hawawezi kuzungumza sentensi nzima bila kuweka maneno au viambishi vya kiingereza hata kwa maneno ya kawaida sana. Na watu hao hao wamezaliwa na kukulia hapa Tanzania. Kwanza hicho kiingereza nacho pia hawajui. Kwa nini mtu aanze kitenzi (verb) kwa kiswahili halafu aimalizie kwa kiingereza. E.g "nilimuinform", "alinicall" "nikiprove nitaconfirm kwako". Na utamsikia mtu anazungumza hivyo katika mazingira rasmi kabisa mf kwenye mahojiano na vyombo vya habari n.k. Hasa vijana na kinadada wanaoitwa "masista du". Hawa ndio hovyo kabisa. Je hapo nako kuna kuachwa nyuma kwa kiswahili? Kwa nini akizungumza Kiingereza hafanyi hivyo? Huu ni utumwa tuliojijengea baada ya kuaminishwa kuwa Kiingereza ni elimu na kuwa ukionekana unakipenda au kukitumia basi wewe ni tofauti na wengine. Upuuzi mtupu.

  Kama ni taaluma mpya au kuna neno ambalo bado kiswahili hakijatengeneza la kwake au ┬┤mtu hulijui sio mbaya ukatumia la kiingereza. Lakini sio kuchanganya maneno ya kawaida tena viambishi vya lugha 2 kwenye neno 1. Mbona wakihojiwa kwa kiingereza hatusikii wakisema "Recently, the rate of inflation has kwenda juu to the extent kwamba we cannot mudu to buy even the very basic goods". Hata kama ni malimbukeni wa kiingereza hawataongea hivyo bali wataongea kiingezera kibovu lakini cha kiingereza hivyo hivyo.
   
 10. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #10
  May 28, 2011
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,739
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Senior Bachelor!

  Kwa ulivyojieleza, kwa kweli sina la kuongeza.
  Kama mtoa hoja, Pangu pakavu, angekuwa ameeleza hivyo toka mwanzo, nisingechangia kabisa hii post, kwa vile kila kitu kingekuwa kimeeleweka.

  Ni kweli hata mimi binafsi nimewahi mara kadhaa kuwasikia watu wakitumia maneno ya kiingereza bila ulazima, wakati maneno ya kiswahili yapo na yamezoeleka. Watu wa namna hiyo ni malimbukeni.

  Lakini kama nilivyoeleza kwenye posts zangu hapo juu, kwa sasa wapo watu ambao hata kama hawapendi kuingizia maneno ya kiingereza, bado wanalazimika kuchanganya kiingereza na kiswahili. Lengo zima ni kuhakikisha ujumbe unafika kama unavyotakiwa. Mfano mzuri kwa sasa ni mambo ya sayansi na teknolojia. Ni rahisi zaidi kueleweka ukiwa unachanganya kuliko ukitafuta misamiati mitupu ya kiswahili. Utakuta kwamba misamiati hiyo ni mipya kwa watu wengi (au sio mipya ila haijazoeleka). Katika mazingira kama hayo, si sahihi mtu kukulaumu kuwa unaendekeza kiingereza au unajidai na kisomo chako.

  ***** ***** ***** *****
  Kwa kuhusina na hili, hivi CD na DVD zina maneno ya kiswahili?
  Naomba kama mtu anafahamu aniambie maneno hayo. Halafu tulinganishe maneno gani yamezoeleka zaidi.
  Kama hayapo, basi, ni bora ifahamike kuwa tunatohoa na kuendelea kutumia CD/DVD. Vinginevyo, BAKITA wataleta maneno rasmi miaka ya baadaye wakati jamii nzima ya waswahili tunajua neno CD na DVD.
   
 11. Sijali

  Sijali JF-Expert Member

  #11
  May 29, 2011
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 2,062
  Likes Received: 424
  Trophy Points: 180
  Hata Waingereza wamekopa maneno kama video, thug, safari n.k . Kama tungekuwa na imani na lugha yetu hakuna kitu kingetushinda. Mbona Waarabu, waajemi, Wachina, Wahindi nk wana maneno yao kwa kila neno jipya linalojitokeza katika dunia? tatizo sisi ki-akili ni watumwa na tunapenda utumwa. Huo ndio ukweli. Yaani, hata suala dogo tu la kufanya elimu tangu msingi hadi Chuo Kikuu iwe ya Kiswahili, halijapatiwa ufumbuzi tangu 'kile kinachoitwa' uhuru?
  Kiswahili kinaweza kukidhi mahitaji yote ya jamii yetu lakini wakuu wetu bado wana asili ya utumwa wa kifikra. Mkuu wetu wa sasa ndiyo kwanza anaona kuzungumza Kiingereza, ambacho hakijui, ndio udokta!
   
 12. Pharaoh

  Pharaoh JF-Expert Member

  #12
  May 29, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kiswahili sio lugha bado, kwa kifumuliwe na replace maneno ya kigeni yanayofanya asilimia 90 ya kiswahili na badala yake yatiwe maneno ya makabila ya afrika kwa kuchagua maneno rahisi. Halafu ndio tujivunie kuwa tuna lugha ya waafrika, eti neno shukran au rais ni ya afrika? Tunapata aibu sana kwa wageni wanapokuja kujifunza lugha hapa
   
 13. Kipilipili

  Kipilipili JF-Expert Member

  #13
  Jun 5, 2011
  Joined: May 25, 2010
  Messages: 2,207
  Likes Received: 478
  Trophy Points: 180
  Wadau nimpongeze sn"senior bachelor" kwani ameninavya uso,na nadhan huwenda amepitia taaluma ya fasihi.nakubal bla shaka wala uvuli vuli kuwa c kiswahili 2 bali ht lugha nyingine zinapwaya katika baadh ya mambo hasa taaluma mbali mbali ikiwemo fasihi yenyewe.cha msingi ni kuwa c kila wakati tuchanganye lugha,tuchanganye lugha pale tu inapobidi na kuhalisi kufanya hvyo.kila lugha imepwelea kwa kias chake na wala kiswahili hakija achwa nyuma kwa kias hcho kikubwa ambacho wadau wamekitaja.hebu angalia lugha km kiarabu,kichina na kijapani.utagundua kuwa kinatosheleza na kukidhi mahtaj ya jamii hucka.nasi tukichuchuuze kiswahili ili kitononoke na kupea mawanda mapana zaidi.KISWAHILI HAZINA YA AFRIKA KWA MAENDELEO ENDELEVU.
   
 14. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #14
  Jun 5, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Mimi nafikiri kinacho-matter ni kama ujumbe umefika. Naona msikilizaji atanielewa zaidi kama nikimwambia anaweza ku-download lile file JF badala ya kupakuwa faili. Au anasome emails zake badala akasome barua pepe zake. Sioni tatizo so long ujumbe umefika. Pia kumbuka lugha huwa zinaendelea kwa ku-borrow maneno toka lugha nyingine. Lugha ya Kingereza imeazima maneno mengi sana toka lugha nyingine. Pia Lugha ya Kiswahili imeazima maneno mengi tuu toka lugha ya Kiarabu.

  Kwa vile tunaishi kwenye dunia ya utandawazi na maendeleo ya sayansi na teknologia, kuna wakati inatubidi kuazima maneno kwenye lugha nyingine ili tuweze kuwasiliana kwa ufasaha zaidi. Sioni kama kuna tatizo lolote. Katika dunia ya sasa hatuwezi ku-avoid code-switching, substrata or lexical borrowing. kwa hiyo kuna uwezekano baada ya miaka 50 sentensi "I wish ningekuwepo nimcheki alivyo shine" ikawa ni sahihi kabisa kwenye lugha ya Kiswahili. By the way, mbona tuna-mix Kiswahili na lugha zetu za makabila, na hapo hakuna tatizo lolote?
   
 15. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #15
  Jun 5, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Mkuu unajua kuwa miaka 20 ijayo China itakuwa inaongoza duniani kwa kuwa na watu wengi wanaongea Kingereza?


  Mkuu umesema ukweli. Hata mimi nilidhania internet ni mtandao kumbe sio. Baadae kabisa wahusika wakaja kusema kuwa ni wavuti. But that was too late. Watu wameshazoea kusema mtandao na ukiomwambia mtu wavuti yangu haifanyi kazi sijui kama atakuelewa.
   
 16. Kipilipili

  Kipilipili JF-Expert Member

  #16
  Jun 5, 2011
  Joined: May 25, 2010
  Messages: 2,207
  Likes Received: 478
  Trophy Points: 180
  EMT.nawe una ugonjwa wa kuchanganya lugha ndo mana unaunga mkono.hatujakataa lugha kukopa,kila lugha duniani hukopa.hv muingereza akitaka kutamka kwa kingereza"BADA"ambao ni ugali wa muhogo,au BEMBE,SORO unadhan atafanya nn zaidi ya kutohoa maneno hayo kwan hayapo katika utamadun wake!ndo hapo lugha hukopa na kutumia maneno yenye asili ya lugha nyingine.maneno hayo yanapoingizwa kwenye kisw kwa mfano,hayawi tena ya kingereza au kiarabu bali huwekwa na kusanifishwa ili yaendane na sarufi ya kiswa.mfano syntax ni neno la kimombo linaposanifishwa linakua SINTAKSIA,hili neno jipya si kimombo tena bali ni kisw kwan neno sintaksia linafata kanuni za sarufi ya kisw na km ukimwandikia muingereza neno hlo{sintaksia}hawezi kuelewa kwa vile lipo nje na sarufi ya kingereza.
  Hebu angalia ujumbe wko utaona ume2mia kingereza mahali ambapo kisw kipo na ungeeleweka vzr tu.angalia maneno AVOID,BORROW,LEXICAL BORROWING,BY THE WAY,MIX. hv kweli hatuna kiswa kinachoeleweka kwa maneno hayo.borrow{kukopa},avoid{kuzuia},mix{kuchanganya},lexical borowing{kukopa kileksika}.tafsiri hii ni kwa mujibu wa ulivyoyatumia maneno katika sentens zako.hivi ungeongea kisw usingeeleweka??c kila wakati kisw hakijitoshelezi,tuchanganye lugha ikiwa tu hakuna budi kufanya hivyo.kinyume chake 2nakiviza kisw cc wenyewe.TUSITAFUTE MCHAWI...
   
 17. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #17
  Jun 5, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Mkuu the good thing ni kuwa ujumbe uliupata. That's what matter. Ungekuwa umejibu kwa kusema kuwa hukuelewa nilichosema, ningekuelewa. Pia inawezekana ningetumia kiswahili tuu bila kuchanganya ungenielewa lakini inawezekana sio wote wangenielewa. Tusijaribu ku-make assumptions kuwa kila Mtanzania anakielewa Kiswahili kama unavyokielewa wewe. After all, kwa wengine Kiswahili is not their mother tongue. Wengine tumeanza kijifunza Kiswahili sambamba na Kingereza tulipoanza shule.

  Tatizo wewe uko too idealistic. Unataka kila mtu aongee Kiswahili bila ku-mix na lugha nyingine. Ningependa iwe hivyo lakini kwa dunia ya sasa that is not possible. Kuchanganya lugha sio ungonjwa bali ndio reality ya dunia ya sasa. Hata ninapoongea lugha ya kabila langu huwa na-mix na Kiswahili pale ambapo nahisi watu watanielewa zaidi. Wengi tuu wanafanya hivyo. Pia kumbuka sio sisi tuu Watanzania tunaochanganya lugha. That is the reality whether or not you admit.

  Baada ya hapo nifafanulie hapo kwenye red ulikuwa unamaanisha nini?
   
 18. Kipilipili

  Kipilipili JF-Expert Member

  #18
  Jun 5, 2011
  Joined: May 25, 2010
  Messages: 2,207
  Likes Received: 478
  Trophy Points: 180
  Hahahaha!c kweli ht kdogo mm naongea lugha zaid ya kingereza na kisw lkn sichangany kwa 7bu kila lugha ina miko yake.kwanini huchangany kingereza na kisw"i want to kutembelea that mbuga of animal at ngorongora mbuga ya nation"km ni kwel ulijifunza lg zote sambamba??mm si mdhanifu(idealist) ila u2mwa wa fikra ndo unaokutia uvulivuli.m2 chake bwana!
  Hv hujui kisw cha "red" mkuu?hahaha!SISI NDIO 2NAOKIHARIBU,nlimanisha hvyo.neno kuviza linatokana na VIZA,ushawah kusikia"yai viza".sisi wamatumbi wa kibongo 2kipitapita shule 2natabu sn.hv ukiongea na bibi kule kijijin unachanganya na kimombo?hahaha
   
 19. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #19
  Jun 6, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Mkuu kwa nini unaongelea tuu lugha za Kiswahili na Kingereza wakati suala hili lipo kwenye lugha zaidi ya hizo? Mbona kuna watu wanachanganya Kiswahili na Kifaransa? Au hao ni ruksa kuchanganya? Vipi hao wanachanganya kifaransa na Kingereza? Sawa mkuu kama utumwa wa fikra ndio unanitia uvulivu, lakini hiyo ndio reality. You cannot turn the clock back.

  Kuhusu kiswahili cha red, la muhimu ni kuhakikisha ujumbe umefika. Badala ya kupoteza muda kueleza maana neno viza, ni bora kwanza kuangalia your audience na kutakafari utumie lugha ya aina gani kufikisha ujumbe. Nafikiri hilo ni la muhimu zaidi. Kuongea kiswahili kigumu ili kuidhihirishia audience kuwa unajua Kiswahili ni sawa na wale wanaongea Kingereza kigumu ili wajulikane kuwa wanakijua. Kwa staili hii sidhani kama utakuwa unawatendea haki wasikilizaji au wasomaji wako. Cha muhimu zaidi ni kuhakikisha ujumbe umefika.

  Mkuu kuhusu bibi yangu, naona tayari umeshafanya assumption au ku-generalise kuwa akina bibi huwa wanaishi vijijini tuu na pia huwa hawaelewi kimombo. Ndio maana nimekuambia wewe ni idealistic sana. Otherwise, utakuwa una-think backward. Mkuu sio akina bibi wote wanaishi vijijini. Pia sio akina bibi wote hajui Kingereza.
   
 20. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #20
  Jun 6, 2011
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,739
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Upo Sahihi kabisa ndugu EMT.
  Cha muhimu ni kwamba ujumbe umfikie mlengwa. Haijalishi umeongea vipi. Ya nini kutumia nguvu na kutoa jasho kutafuta misamiati ya kiswahili ambayo wewe mwenyewe huna uhakika nayo eti ilmradi tu usichanganye lugha? Mtu unapoongea unataka kufikisha ujumbe kwa msikilizaji. Na huo ndio msingi wa mawasiliano ya lugha-kufikisha ujumbe.

  Kwa mabadiliko na maendeleo ya maisha kwa sasa hata kama bibi yako anakaa kijijini au mjini, bado utakuta kwamba kuna sentensi utalazimika kuchanganya lugha. Ama kiingereza na kiswahili au kiswahili na kilugha cha kikabila au hata kikabila, kiingereza na kiswahili n.k. Maana kutokana na maendeleo, utakuta kuna vitu unavijua, ambavyo havina maneno kwenye kabila lako au hata kwenye kiswahili. Kwa mfano utatumia neno gani kwenye kichaga ukimaanisha "internet"?. Hapo lazima uchanganye lugha tu lengo likiwa ni kufikisha ujumbe.
   
Loading...