Kiswahili katika Redio ONe - KUWAKILISHA

IshaLubuva

JF-Expert Member
Dec 4, 2008
250
11
Habari wana JF.

Jumamosi iliyopita wakati najiandaa kutoka nyumbani nilikuwa nawasilikisa wachambuzi wa lugha ya kiswahili kutoka BAKITA wakihojiwa na mtangazaji wa Radio One. Sehemu ya majadiliano yao yalihusu maneno "Kuwakilisha" na "Kuwasilisha". Ufafanuzi waliotoa kuhusu neno "Kuwasilisha" nilikubaliana nao ila uliohusu neno "Kuwakilisha" kwa maoni yangu naona kama walipotosha. Katika ufafanuzi wao walisema kwamba kuwakilisha ni hali ya kitu kutumika badala ya kingine au kama ni mtu kwenda au kuhudhuria tukio fulani badala ya mtu mwingine.

Kwa mtazamo wangu kuwakilisha siyo kuwa mbadala bali ni kufanya kitu kwa niaba ya anayetakiwa kukifanya. Unapowakilisha unatakiwa kama ni kutoa kauli utowe zinazoendana na msimamo wa unayemuwakilisha. Mfano, ikitokea mkuu wa taasisi fulani amealikwa kwenye mkutano au tukio fulani lakini akakosa nafasi ya kushiriki na kumteua mtumishi wa chini yake kumuwakilisha, mtumishi huyo atakapotakiwa kuongea jambo fulani atawajibika kuongea kwa kuzingati msimamo wa taasisi yake na ambao Mkuu wake ndiyo amewekwa kuitekeleza na kuisimamia.

Lakini unapokuwa umechukuliwa kama mbadala wa mtu mwingine unakuwa na uhuru wa kuwasilisha mawazo yako au ubora wako. Mfano kwenye timu ya mpira mchezaji fulani anawza kupangwa badala ya mchezaji mwingine lakini huwezi kuwa na mchezaji anayemuwakilisha mchezaji mwingine kwenye mechi.

Wabunge ni wawakilishi wa wananchi katika majimbo yao kwenye Bunge na kwa hiyo wanapaswa kuongea kwanza na wananchi wao ili wapate mawazo na maoni yao ili yawe msingi wa Mbunge anapochangia Bungeni. Kama mtakumbuka majuzi kuna wananchi kutoka jimbo moja la mkoa wa Mbeya (nadhani ni Chunya kama sikosei) walisafiri kutoka Jimboni kwao hadi Dodoma kupinga kauli aliyoitoa Mbunge wao kwamba hawajamtuma.

Karibuni kwa maoni.
 
IshaLubuva

.

wasilisha = deliver; send.

maneno yanayoendana nayo ni kama ...... wasilishia; wa-silishika; wasilishana; wasi-lishwa.

&

wakilisha = represent.

maneno yanayoendana nayo ni kama
...... wakilishia; wakilishika; wakilishana; wakilishwa.


Hicho ndicho kiswahili fasaha
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom