marcoveratti
JF-Expert Member
- Sep 21, 2017
- 1,110
- 1,952
Wanasema kitabu cha Wakorintho kilieleweka zaidi na Wakorintho wenyewe kuliko kilivyosomwa na watu wa Efeso, kwa sababu anayebeba uzito wa jambo fulani ndiye anayejua kina chake kuliko anayelitazama akiwa mbali au kusimuliwa.
Labda hiyo ndiyo sababu kumuelewa Bruno Fernandes kunahitaji zaidi ya kuangalia takwimu, mabao au hasira zake uwanjani. Ili kumuelewa Bruno, lazima kwanza uelewe mzigo wa nafasi anayoicheza na ukubwa wa klabu anayoiongoza.
Soka la kisasa limebadilisha maana ya kiungo mshambuliaji. Zamani, namba 10 alikuwa msanii wa mwisho wa mashambulizi
mtu aliyesubiri mpira ili kuleta uchawi wake.
Lakini zama zimebadilika. Leo, kiungo mshambuliaji anatakiwa kuwa msanii na mpiganaji kwa wakati mmoja.
Anatakiwa kutengeneza nafasi, kufunga mabao, kusaidia presha, kuongoza wenzake na wakati mwingine kubeba hasira za mashabiki.
Hapo ndipo Bruno Fernandes alipojitengenezea ufalme wake.
Alipofika Manchester United Januari 2020, hakukuta timu iliyokuwa ikitembea kwa kujiamini. Alifika kwenye klabu iliyokuwa bado ikitafuta utambulisho baada ya kuondoka kwa kizazi cha mafanikio.
Ndani ya muda mfupi, mchezaji kutoka Sporting Lisbon akawa kitu ambacho United ilikuwa imekikosa kwa muda mrefu nae ni mtu anayefanya mambo yatokee.
Alikuwa mchezaji aliyekuwa tayari kuomba mpira hata wakati mchezo ulikuwa mgumu. Wakati wengine walitaka kujificha baada ya kosa, Bruno aliendelea kutafuta mpira mwingine baada ya makosa matatu mfululizo.
Bruno si mchezaji wa ukimya. Hisia zake ziko wazi. Anaweza kuonyesha hasira baada ya kosa, anaweza kubishana, anaweza kuonekana mwenye presha. Lakini nyuma ya yote hayo kuna kitu kimoja ambacho mara nyingi husahaulika, anajali.
Katika soka, wachezaji wanaojali zaidi ndiyo wanaobeba lawama nyingi zaidi.
Kwa sababu mtu anayekwepa majukumu hawezi kukosolewa kwa kutoyabeba.
Kipaji cha Bruno hakipo tu kwenye pasi zake za mwisho au uwezo wake wa kupiga nje ya box. Kitu kinachomtofautisha ni ujasiri wa kufanya maamuzi ambayo wachezaji wengi huogopa kuyafanya.
Mpira wa miguu ni mchezo wa makosa. Lakini wachezaji wabunifu wanaishi kwenye eneo hatari zaidi kuliko wengine. Wanajaribu pasi ambayo inaweza kufungua nzima ya ulinzi , lakini ikikosekana ndiyo hiyo hiyo itakayowafanya waonekane kama wamekosea.
Bruno amekuwa akiishi kwenye mstari huo kwa miaka mingi.
Ni rahisi kumpima kwa kile alichokosa.
Ni rahisi kukumbuka pasi iliyopotea au nafasi iliyokosekana. Lakini wale wanaoangalia ndani zaidi wanaona thamani ya mchezaji ambaye kila mara anataka kuhusika.
Katika kizazi ambacho viungo washambuliaji wanatakiwa kuwa kila kitu kwa wakati mmoja, Bruno Fernandes amekuwa mfano wa aina mpya ya namba 10. Sio yule anayesubiri mchezo umfuate, bali yule anayelazimisha mchezo ubadilike.
Ana sehemu za De Bruyne kwenye ubunifu, ana roho ya wapiganaji wa kiungo wa zamani, na ana tabia ya viongozi ambao hawajifichi wakati timu inapokuwa kwenye matatizo.
Ndiyo maana anaweza kugawa maoni.
Wengine wataona malalamiko yake. Wengine wataona mapambano yake.
Wengine wataona makosa yake.
Lakini wenzake wanaona kitu ambacho mashabiki walio mbali hawaoni mchezaji anayekubali kubeba mzigo wa lawama.
Historia ya soka mara nyingi huwakumbuka wale waliokuwa wakamilifu. Lakini, wale wanaokumbukwa zaidi ni wale waliokubali kuingia kwenye moto.
Bruno Fernandes hajajenga jina lake kwa kuwa mchezaji asiye na makosa.
Amelijenga kwa kuwa mchezaji ambaye bado anataka mpira hata baada ya kufanya kosa.
Na labda hiyo ndiyo alama kubwa ya kiungo mshambuliaji wa kisasa:
Sio kutengeneza uzuri tu.
Ni kuwa tayari kubeba uzito wake.