Kiswahili cha BBC | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kiswahili cha BBC

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by MJIMPYA, Aug 27, 2011.

 1. MJIMPYA

  MJIMPYA JF-Expert Member

  #1
  Aug 27, 2011
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 465
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Wakuu
  Nisaidie hiki kiswahili cha BBC


  Umoja wa Mataifa umeziomba pande zote katika vita vya Libya,
  kuzuwia vitendo vya kulipiza kisasi.


  Taarifa hiyo imetolewa baada ya kuarifiwa kuwa wanajeshi wa Kanali Gaddafi wameuwa watu, na kwamba Waafrika waliokuwa wakipigana kwa niaba ya serikali piya wameshambuliwa.

  Huku kukiwa na ripoti kuwa Waafrika waliokuwa katika jeshi la Kanali Gaddafi wanauwawa, wengi wao wamekuwa wakivuka mpaka na kuingia Mali na Niger.

  Inaarifiwa magari 60 yameingia Niger kutoka Libya, lakini yalizuwiliwa mjini Agadez.

  Watu hao wengi ni wapiganaji wa zamani wa kabila la Tuareg, ambao walipatana na serikali ya Niger mwaka 2009.
  Inaarifiwa kuwa magari 10 nayo yameingia Mali.
  Mapema mwaka huu, wakuu wa Mali waliiambia BBC, kwamba Wa-Tuareg wakilipwa dola elfu 10 kujiunga na serikali ya Libya, na kila siku ya mapigano wakipata dola 1000.
  Duru za mataifa ya magharibi zinasema Waafrika kama elfu 10 waliajiriwa na Gaddafi.
  Sasa ndege za Nato zinarusha vikaratasi na kutoa matangazo, kuwasihi Waafrika waasi na watapokelewa kufwatana na sheria.
   
 2. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #2
  Aug 28, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Kipo sawa tu kaka, tatizo lipo wapi?
  Rahaja za Kiswahili zipo nyingi ndugu, na zote zinatambuliwa kuwa ni Kiswahili:

  Mfano:
  Kibajuni
  Kiamu
  Kifundi
  Kimatondoni
  Kimgao
  Kimrima: spoken around Pangani, Vanga, Dar es Salaam, Rufiji and Mafia Island.
  Kimvita
  Kimwini
  Kipate
  Kipemba
  Kishamba
  Kisiu
  Kiunguja: spoken in Zanzibar City and environs on Unguja (Zanzibar) Island. Other dialects occupy the bulk of the island.
  Chichifundi
  Chijomvu
  Chimwiini
  Kimrima
  Kimvita
  Kimwani
  Kingare
  Kitikuu
  Kitumbatu
  Kivumba

  Remember, Modern standard Swahili is based on Kiunguja

  Mfano mwingine soma ili shairi, ni Kiswahili cha Kibajuni:

  NALILIA UBAJUNI

  Nalilia ubajuni, ilahi achusitiri
  kivakumbuka moyoni, dua dhangu hukithiri
  Mungu atachuawini, achupe kula la kheri
  hali dhechu masikini, dhiko kachika hatari

  Kidhikumbuka dhamani, dhangu imi kunyukiya
  chwaliko chuna samani, vabajuni nakwambiya
  chuki-ishi mahondeni, kwa dhakula na afiya
  siku hidhi masikini, mangi amechupoteya
   
 3. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #3
  Aug 28, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Ahsante Mkuu. Kiswahili fasaha kiko Unguja.
   
 4. Viper

  Viper JF-Expert Member

  #4
  Aug 28, 2011
  Joined: Dec 21, 2007
  Messages: 3,665
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  standard kiswahili ni cha unguja & kikifuatiwa na mombasa na cha tanga ukiwatoa " wasambaa "
   
 5. Inanambo

  Inanambo JF-Expert Member

  #5
  Aug 28, 2011
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 2,864
  Likes Received: 1,147
  Trophy Points: 280
  tuandamane nami katika kuwaletea habari
   
 6. Suki

  Suki JF-Expert Member

  #6
  Aug 28, 2011
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 373
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Lahaja?
  Ila kiswahili sasa hivi kweli shaghalabhaghala tu. The worse it is, the better it sounds.
   
 7. Sita Sita

  Sita Sita JF-Expert Member

  #7
  Aug 30, 2011
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 1,197
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Mi nachekaga wanaposema KOROKORONI
  Kwa nini wasiseme ┬┤rumande┬┤
  Kuna misemo yao mingine ni vere vere strange kama Wadukuzi,
   
 8. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #8
  Aug 30, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160


  Kiswahili
  kimepatikana kwa namna au lahaja mbalimbali. Wakati wa ukoloni wa Uingereza azimio lilitolewa kutumia Kiswahili cha Unguja kuwa Kiswahili rasmi katikaTanganyika, Kenya na Zanzibar. Waingereza walikitumia pia kama lugha ya polisi najeshi katika Uganda.Kati ya lahaja za Kiswahili ni zifuatazo:
   
Loading...