KISUTU: Kesi namba 456(Jamhuri v Maxence Melo na Micke William) yapigwa tena kalenda

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Kesi namba 456 (Jamhuri v Maxence Melo na mwenzake Micke William) ambapo kampuni ya OilCom iliandikwa katika mtandao wa JamiiForums ikidaiwa kukwepa kodi na kuchakachua mafuta bandarini Dar (iliyopo chini ya Hakimu Thomas Simba) imetajwa tena leo Julai 17, 2018

Upande wa Jamhuri leo umewakilishwa na Wakili Mwandamizi, Patrick Mwita huku upande wa utetezi ukiwakilishwa na Wakili, Jebra Kambole.

Akitoa maelezo mbele ya Hakimu Simba, Wakili wa Jamhuri amesema kuwa Washitakiwa wote wapo na Mawakili wao pia, bahati mbaya Wakili anayeendesha mashitaka, Mutalemwa Kinyeshi amepata dharura na ameomba kesi ipangwe tarehe yoyote kuanzia kesho.

Baada ya maelezo hayo Hakimu Simba alisema kwa kuwa kama Wakili kapata dharura kesi inabidi kuahirishwa lakini kesi hiyo imechukua muda mrefu sana hivyo inabidi kupangwa tarehe mbili za kusikilizwa.

Aidha, amesema kuwa kwa namna kesi ilivyo inaonesha kuwa mashahidi wote wanaotoa ushahidi wanatoka Dar hivyo hata shahidi huyu anayesubiriwa atakuwa anatoka Dar pamoja na vielelezo vyote vya kesi hiyo, hivyo kuchukua muda mrefu haina maana.

Hakimu Simba pamoja na Mawakili(Upande wa utetezi na Jamhuri) wamekubaliana kuahirisha kesi hiyo mpaka Julai 26 na Agosti 01, 2019).

Ikumbukwe kuwa mara ya mwisho shauri hili lilipokuwa linasikilizwa(Julai 11, 2018) Upande wa Jamhuri walikuwa hawana shahidi na waliahidi kuleta shahidi leo

Hakimu Simba aliuambia upande wa Jamhuri wahakikishe wana shahidi kwa siku ya leo
================

UPDATES:
Kesi namba 456 (Jamhuri v Maxence Melo na mwenzake Micke William) ambapo kampuni ya OilCom katika mtandao wa JamiiForums ilidaiwa kukwepa kodi na kuchakachua mafuta bandarini Dar (iliyopo chini ya Hakimu Thomas Simba) imetajwa tena leo Julai 26, 2018.

Katika shauri hili kwa siku ya leo, Upande wa Jamhuri unaongozwa na Wakili Mutalemwa Kishenyi huku upande wa Utetezi ukiwakilishwa na Wakili Jeremiah Mtobesya.

Upande wa Jamhuri umemleta Shahidi wao, Usama Mohammed ambaye ni Msimamizi wa Mauzo ya rejareja wa Oilcom (T) Ltd kwa ajili ya maswali kutoka kwa Wakili wa utetezi.

Wakili Kishenyi anasema kwa upande wake, yeye ameshamaliza examination na kusema kama upande wa Utetezi wana maswali wanaweza kuendelea.

Mheshimiwa Hakimu anamruhusu Wakili wa Utetezi, Jeremiah Mtobesya kuendelea na kuuliza maswali

*****

Wakili Mtobesya: Mhe mimi nina maswali matatu tu ila chochote kinaweza kitokea kutokana na majibu yake(Shahidi)

Swali la kwanza: Shahidi ielezee Mahakama Kampuni yako inaitwaje?

Shahidi: Olicom Tanzania Limited

Wakili Mtobesya: Kosa uliloenda kulilalamikia Polisi ilikuwa ni kosa gani?

Shahidi: Kuchafuliwa jina wa Kampuni yetu

Wakili Mtobesya: Unatambua Washitakiwa wanashitakiwa kwa kosa gani hapa ambalo wewe ndio umekuja kutolea ushahidi?

Shahidi: Kosa la kuzuia upelelezi

Wakili Mtobesya: Asante Mheshimiwa Hakimu, mimi nimemaliza maswali yangu

*****

Hakimu Simba: Kishenyi unahitaji re-examination?

Wakili Kishenyi: Hapana

Wakili Kishenyi anaongea na kusema “Mheshimiwa nilikuwa naomba tarehe nyingine ya kusikilizwa, nafahamu ilikuwa imepangwa tarehe 1/08 ila naomba iende tarehe 14/08"

Hakimu Simba anakubali ombi la Wakili Kishenyi, pia Wakili Mtobesya anakubali.

Kesi imeahirishwa mpaka tarehe 14/08/2018 saa 5 asubuhi ambapo dhamana inaendelea kwa washitakiwa.

===========

UPDATES
Kesi namba 456 (Jamhuri v Maxence Melo na mwenzake Micke William) ambapo kampuni ya OilCom iliandikwa katika mtandao wa JamiiForums ikidaiwa kukwepa kodi na kuchakachua mafuta bandarini Dar (iliyopo chini ya Hakimu Thomas Simba) imetajwa tena leo Agosti 14, 2018.

Katika shauri hili kwa siku ya leo, Upande wa Jamhuri unaongozwa na Wakili Mutalemwa Kishenyi huku upande wa Utetezi ukiwakilishwa na Wakili Peter Kibatala, Wakili Jeremiah Mtobesya na Wakili Mkungu

Upande wa Jamhuri umeomba nafasi ya kupewa siku nyingine kwa shauri hilo kusikilizwa kwa maana kwa siku hii hakuna shahidi waliyemleta.

Hakimu Simba anaridhia ombi lao na upande wa utetezi wanaridhia.

Wanajadiliana tarehe(Hakimu Simba, Upande wa Jamhuri na Upande wa Utetezi)

Hakimu Simba anasema shauri hili linaahirishwa tena hadi Septemba 4, 2018

=========

UPDATES

Kesi namba 456 (Jamhuri v Maxence Melo na mwenzake Micke William) ambapo kampuni ya OilCom iliandikwa katika mtandao wa JamiiForums ikidaiwa kukwepa kodi na kuchakachua mafuta bandarini Dar (iliyopo chini ya Hakimu Thomas Simba) imetajwa tena leo Septemba 04, 2018.

Katika shauri hili kwa siku ya leo, Upande wa Jamhuri unaongozwa na Wakili Mutalemwa Kishenyi huku upande wa Utetezi ukiwakilishwa na Wakili Jeremiah Mtobesya na Wakili Jebra Kambole.

Upande wa Jamhuri umeomba nafasi ya kupewa siku nyingine kwa shauri hilo kusikilizwa kwa maana kwa siku hii hakuna shahidi waliyemleta.

Hakimu Simba anasisitiza kuwa shauri hili linatakiwa kuisha mwezi huu wa tisa au likichelewa basi liishe mwezi wa kumi mwanzo kwa maana shauri hili ni la siku nyingi sana.

Aidha, anaridhia ombi lao na upande wa utetezi nao pia wanaridhia ombi hilo

Wanajadiliana tarehe(Hakimu Simba, Upande wa Jamhuri na Upande wa Utetezi)

Hakimu Simba anasema shauri hili linaahirishwa tena hadi Septemba 24, 2018

==========

UPDATES:
Kesi namba 456 (Jamhuri v Maxence Melo na mwenzake Micke William) kuhusu kampuni ya OilCom kuandikwa katika mtandao wa JamiiForums ikidaiwa kukwepa kodi na kuchakachua mafuta bandarini Dar (iliyopo chini ya Hakimu Thomas Simba) imetajwa tena leo Septemba 24, 2018

Katika shauri hili kwa siku ya leo, Upande wa Jamhuri unaongozwa na Wakili Mkuu wa Serikali Tumaini Kweka akishikirikiana na Wakili Mutalemwa Kishenyi huku upande wa Utetezi ukiwakilishwa na Wakili Peter Kibatala na Wakili Jebra Kambole

Upande wa Jamhuri umeomba nafasi ya kupewa hadi siku ya kesho Septemba 25 ili kuendelea kesi kutokana na kuwa na kesi nyingi kwa siku ya leo na kushindwa kuwa na shahidi.

Hakimu Simba anasisitiza kuwa shauri hili linatakiwa kuisha mwezi huu wa tisa au likichelewa basi liishe mwezi wa kumi kwa maana shauri hili ni la siku nyingi sana.

Hakimu Simba anasema shauri hili linaahirishwa tena hadi kesho Septemba 25, 2018.

========

UPDATES:
Shauri hili limeendelea tena leo Septemba 25, 2018 kama ilivyokubaliwa jana na upande wa Utetezi na Jamhuri mbele ya Hakimu Mkazi Thomas Simba.

Upande wa Jamhuri unaongozwa na Wakili Mkuu wa Serikali, Tumaini Kweka huku upande wa Utetezi ukiongozwa na Wakili Peter Kibatala akishirikiana na Wakili Jeremiah Mtobesya na Wakili Jebra Kambole.

Aidha kwa siku ya leo pia(kama ilivyokuwa jana) upande wa Jamhuri umeshindwa kuja na shahidi na kuomba kupangiwa siku nyingine huku wakisisitiza kuwa watakuwa na shahidi siku hiyo.

Shauri hili linaahirishwa mpaka Oktoba 11, 2018 ambapo litasikilizwa tena.

==========

UPDATES
Kesi namba 456 (Jamhuri v Maxence Melo na mwenzake Micke William) kuhusu kampuni ya OilCom kuandikwa katika mtandao wa JamiiForums ikidaiwa kukwepa kodi na kuchakachua mafuta bandarini Dar imetajwa tena leo Oktoba 11, 2018.

Kesi hiyo imetajwa mbele ya Hakimu Mkazi Thomas Simba huku upande wa Jamhuri ukiwakilishwa na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Patrick Mwita.

Upande wa Utetezi leo umewakilishwa na Wakili Jeremiah Mtobesya akisaidiana na Wakili Jebra Kambole.

Hata hivyo kesi hiyo imeshindwa kuendelea baada ya Upande wa Jamhuri kudai mbele ya Hakimu kuwa hawajaja na Shahidi yeyote.

Akiongea Wakili Mwandamizi, Patrick Mwita amesema "Mheshimiwa Hakimu, Shauri hili limekuja leo kwa ajili ya kusikilizwa lakini tunaomba tupangiwe tarehe nyingine ili tuje na shahidi kwa maana leo hatuna shahidi."

Hakimu Simba anakubaliana na ombi hilo huku Wakili Mtobesya akisema kama hakuna Shahidi inabidi kupangwa tarehe nyingine na ni sawa kuahirishwa kwa shauri hilo.

Upande wa Jamhuri na ule wa Utetezi wamekubaliana kuahirisha hadi tarehe 31 Oktoba 2018.

Hakimu Simba ameahirisha shauri hilo hadi Oktoba 31, 2018 kwa ajili ya kusikilizwa tena.

=====

UPDATES:
Kesi namba 456 (Jamhuri v Maxence Melo na mwenzake Micke William) kuhusu kampuni ya OilCom kuandikwa katika mtandao wa JamiiForums ikidaiwa kukwepa kodi na kuchakachua mafuta bandarini Dar imetajwa tena leo Oktoba 31, 2018.

Kesi hiyo imetajwa mbele ya Hakimu Mkazi Thomas Simba huku upande wa Jamhuri ukiwakilishwa na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Nassoro Katuga.

Upande wa Utetezi leo umewakilishwa na Wakili Jeremiah Mtobesya akisaidiana na Wakili Jebra Kambole.

Hata hivyo kesi hiyo imeshindwa kuendelea baada ya Upande wa Jamhuri kudai mbele ya Hakimu kuwa hawajaja na Shahidi yeyote.

Akiongea Wakili Mwandamizi, Nassoro Katuga amesema "Mheshimiwa Hakimu, Shauri hili limekuja leo kwaajili ya kusikilizwa lakini tunaomba tupangiwe tarehe nyingine ili tuje na shahidi kwa maana leo hatuna shahidi."

Hakimu anawauliza upande wa Utetezi kuwa wanasemaje. Wakili Mtobesya anasema "Mheshimiwa tunaomba wenzetu wachukulie hili suala kwa uzito na umuhimu kwa maana miaka miwili sasa na tumesikiliza mashahidi wanne tu."

Hakimu Simba anakubali hoja hiyo na kuuonya upande wa Jamhuri kuwa ahirisho la kutokana na kutokuwa na shahidi litakuwa la mwisho kwa maana kesi hii imechukua muda mrefu sana na haijafika popote.

Upande wa Jamhuri na ule wa Utetezi wamekubaliana kuahirisha hadi tarehe 15 Novemba 2018.

Hakimu Simba ameahirisha shauri hilo hadi Novemba 15, 2018 kwaajili ya kusikilizwa tena.
======

UPDATES:
Shauri hili limeendelea tena leo Novemba 15, 2018 katika Mahakama hii ya Hakimu Mkazi, Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Thomas Simba.

Upande wa Jamhuri unaongozwa na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Nassoro Katuga huku upande wa Utetezi ukiongozwa na Wakili Peter Kibatala akishirikiana na Wakili Jeremiah Mtobesya

Upande wa Jamhuri umesema umekosa shahidi na hivyo kuomba kupangiwa siku nyingine yakusikilizwa huku wakisisitiza kuwa watakuwa na shahidi siku hiyo

Shauri hili linaahirishwa mpaka Desemba 12, 2018 ambapo litasikilizwa tena
=======

UPDATE
Kesi namba 456 (Jamhuri v Maxence Melo na mwenzake Micke William) kuhusu kampuni ya OilCom kuandikwa katika mtandao wa JamiiForums ikidaiwa kukwepa kodi na kuchakachua mafuta bandarini Dar imetajwa tena leo Desemba 12, 2018.

Kesi hiyo imetajwa mbele ya Hakimu Mkazi Thomas Simba huku upande wa Jamhuri ukiwakilishwa na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Nassoro Katuga

Upande wa Utetezi leo umewakilishwa na Wakili Jeremiah Mtobesya akisaidiana na Wakili Jebra Kambole.

Hata hivyo kesi hiyo imeshindwa kuendelea baada ya Upande wa Jamhuri kudai mbele ya Hakimu kuwa hawajaja na Shahidi yeyote

Hakimu Simba anakubali hoja hiyo na kuuonya upande wa Jamhuri kuwa ahirisho la kutokana na kutokuwa na shahidi litakuwa la mwisho kwa maana kesi hii imechukua muda mrefu sana na haijafika popote

Upande wa Jamhuri na ule wa Utetezi wamekubaliana kuahirisha hadi tarehe 28 Januari 2019
 
Shahidi anasema alienda kulalamikia kosa la kuchafuliwa kampuni yao sasa anatoa ushahidi wa kesi ya kuzuia upelelezi, yeye mambo ya upelelezi yanamuhusu nini, hata mimi nisiyekuwa mwanasheria nimejua hii ni kesi ya kizushi
Saa zingine mtu unanyamaza ili uone mwisho ni upi!!!
Ila ikumbukwe siku zote haki hushinda na kweli hudhihiri hata kama itachukua muda
 
Saa zingine mtu unanyamaza ili uone mwisho ni upi!!!
Ila ikumbukwe siku zote haki hushinda na kweli hudhihiri hata kama itachukua muda

Lawyers wana msemo; JUSTICE DELAYED IS JUSTICE DENIED.
Hii ni Haki iliyo wazi lakni inayocheleweshwa maksudi!
Hapa kiukweli hakuna kesi! Jamhuri wamekwama kwa kukosa ushahidi na wanaona aibu kukiri kuwa wameshindwa!
WATASHINDANA SANA LAKINI HAWATASHINDA!!!!!
 
Lawyers wana msemo; JUSTICE DELAYED IS JUSTICE DENIED.
Hii ni Haki iliyo wazi lakni inayocheleweshwa maksudi!
Hapa kiukweli hakuna kesi! Jamhuri wamekwama kwa kukosa ushahidi na wanaona aibu kukiri kuwa wameshindwa!
WATASHINDANA SANA LAKINI HAWATASHINDA!!!!!
Ilisemwa "wanalipwa mshahara na serikali, mahakama ni za serikali wanashindwaje 'vyesi'?"
 
Back
Top Bottom