Mkome kuchagua wapiga vidufu kuingia ikulu
Kigogo,
Unaikebehi "dufu," kwa kuwa huijui historia ya uhuru wa Tanganyika.
Nakuwekea hapa kitu kidogo utafakari tulikotoka:
"Nyerere aliporudi Lindi mwaka 1959, TANU ilikuwa ina nguvu sana na ilikuwa imekumba kila mtu. Wale watumishi wa serikali wengi wao wakiwa Wakristo, walio kuwa wakiibeza TANU mwaka 1955 kwa sababu ilikuwa ikiongozwa na Waislam wasiokuwa na elimu, ukweli ulikuwa umewadhihirikia na sasa walikuwa wakionyesha heshima kwa chama. Hawakuwa na khiyari na ilibidi waonyeshe heshima kwa sababu bwana mwenyewe, yaani serikali ya kikoloni, ilikuwa na heshima kwa TANU. Serikali ilikuwa imetambua kuwa dhamiri ya watu ya kukataa kutawaliwa haiwezi tena kupuuzwa.
Nyerere alikuwa amelihutubia Baraza la Udhamini la Umoja wa Mataifa mara mbili, mara ya pili ikiwa mwaka 1957. Ujumbe wa TANU ulikuwa wazi, watu wa Tanganyika walikuwa tayari kujitawala. Kila siku zilivyopita ndivyo TANU ilivyopata nguvu.
Rashidi Salum Mpunga, dereva wa lori, aliweza kumshawishi na akafanikiwa kumuingiza TANU mmoja wa masheikh wenye kuheshimiwa sana mjini Lindi na mshairi maarufu,
Sheikh Mohamed bin Yusuf Badi.
Sheikh Badi alipoingia TANU kwa ajili ya heshima yake na kukubalika na watu, idadi kubwa ya Waislam walimfuata na kukata kadi za TANU.
Nyerere alipokuja Lindi kujadili tatizo la kura tatu na uongozi wa Jimbo la Kusini,
Sheikh Yusufu Badi alimpokea
Nyerere na madras yake, wanafunzi wakimwimbia
Nyerere kasda na kumpigia
dufu. Kuanzia hapo sasa kila mtu alijiunga na TANU. Si
Mponda wala
Kanisa lilikuwa na uwezo wa kupambana na TANU kwa wakati ule. Polepole lakini na kwa uhakika, TANU ilingia ndani ya maeneo ya Kikristo huko Songea, Masasi, Tunduru na Newala, nyumbani kwa
Yustino Mponda."
(Kutoka: "Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) Historia Iliyofichwa Kuhusu Harakati za Waislam Dhidi ya Ukoloni wa Waingereza Katika Tanganyika," Phoenix Publishers, Nairobi 2002).