Kisingizio: Daftari la Wapiga Kura, vyombo vya dola. Sababu?

Unahoji viongozi wa CDM? Hujui kuwa watu hawa ni malaika hawafanyi makosa daima na ni mwiko kuwahoji
Hii ni kitu gani? hata sentesi inakusinda? 1+1=11

Out of 29 unaambulia matatu tu pamoja na Vuguvugu lote lile la M4C na udhaifu wote huo wa CCM?
safi sana 29-3=26, kaulize CCm wamna kata ngapi ndio uje!
Unajua maana ya VUGUVUGU!? ok kuna mabadilika ya siku moja? Rudi darasani ujue maana ya mabadiliko.

Hivi kwani waliojiandikisha kura ni wana CCM milele? Vipi majimbo mengine walioshida?
Unajua kuna Kadi ngapi feki zimekamatwa? Askari wametishia watu wangapi?

Daftari inaweza kuchangia kiasi fulani lakini not to that extent maana kama mwendo ndio huu then tusahau kabisa CDM kuchukua nchi 2015 ikiwa viongozi wote wapo free kukampeni kwenye chaguzi ndogo vipi wakijichimbia kwenye majimbo yao
unajigonga gonga tu...

Hapa kunatatizo kimsingi watu tunalewa na wingi wa watu kwenye mikutano na maandamano
pole na kulewa...
 
Kwa mtizamo mwepesi ni kuongea na keyboard, lakini kupeleka majeshi ardhini imekuwa tatizo. Swala kubwa hapa ni je wanachama na wapenzi wa CDM walifanya nini kufanikisha ushindi zaidi? Ieleweke ushindi ni pamoja na kuwa na washindani.

Kushinda ni pamoja na mambo mengi, ikiwa ni pamoja na kusiamamisha wagombea wanaokubalika, kuwa na wahamasishaji na njia nyingine zinazowafikishia ujumbe wanapiga kura, kwa uchache. Sina hakika kama tuko tayari kwa wingi kiasi hicho kugombea nafasi hizi au kushiriki kwa hali na mali vya kutosha kusaidia CDM ishinde. Labda kwa hofu kuwa wenye kazi zao wanaweza kubanwa katika njia moja au nyingine, ikiwa ni pamoja na hofu ya matokeo ya hivi karibuni. Kuna shida kubwa kuwa ni mara chache sana wasomi kujitoa katika mstari wa mbele ili wahesabiwe, na hili ndilo linalogharimu sana vyama vya upinzani.

Lakini ukweli utabaki kuwa pamoja na ushindi kutofikia viwango tulivyotegemea, kuna kazi ya kufanya na inapasa kukaa na kutafakari tabu ilikuwa wapi, na nini kifanyike ili palipoparuza panyooshwe.
 
MMK wewe na kundi lako ni zaidi kaswende kwenye harakati za ukombozi!!

Ila jamani tuoneeni huruma ndugu zenu maana wakati nyinyi mnasaza kwa pesa za ki-fisadi wenzenu hata mlo mmoja ni tabu!!

Hakika moto wa jehanamu upo na mtakuwa sehemu ya kwazi yake!! Tubuni muache kutumika!!
 
Tunachofanya ni kuwekeza, na matunda ya uwekezaji hayaji mara moja bali huanza taratibu mwaka hadi mwaka. Kwahiyo kupata kata tatu katikati ya kiwango cha juu cha rushwa mnayotoa kwa wananchi pamoja na majeruhi mengi kwa wananchama wetu ni jambo la heshima sana kwetu.

Hadi kufikia 2014 na 2015 bila shaka utakuwa unashuhudia mwenyewe kwa macho yako matunda ya uwekezaji tunaoufanya sasahivi.

Mkuu ni kazi sana kuwaelimisha hawa jamaa ni bora hata ya wanyama wanaweza kukuelewa, kampeni inaitwa vuguvugu la mabadiliko, M4C, wanataka tukiamuka tu, wakute mabadiliko!

Nadhani MMJ lengo alilitumwa anataka kulikamilisha...
 
Naamini kuna point ya msingi kwa CHADEMA, nayo ni kuwatumia na kuwaanda vizuri vijana wasomi na wenye maadili safi kitu ambacho kitaongeza mvuto wa kupigiwa kura siku zijazo,
 
Kama kweli wapo wana CDM (wanachama, wapenzi na mashabiki" wanaridhika na matokeo haya basi nina uhakika mwaka 2015 CDM itakaposhindwa kuchukua nchi watakuja na visingizio vingine ili kwanini wajiandae tena kwa 2020. Haiwezekani kukosekana sababu. Watu wanafikiria kuwa daftari la wapiga kura likiboreshwa basi wana CDM wengi ndio watajiandikisha. Hawadhanii kuwa wapo wana CCM wengi na mashabiki wa CCM ambao nao watajiandikisha.

Swali la msingi si daftari la wapiga kura kwanza ni wanachama. Kitila - CDM ina wanachama wangapi sasa na wameongezeka kwa kiasi gani kutoka 2010?
 
Last edited by a moderator:
Daftari la wapiga kura na vyombo vya dola vitabebeshwa lawama na labda vinastahili. Lakini katika hili CHADEMA inapaswa kutoa sababu zinazoeleweka zaidi ya visingizio.

Kila mtu (kiongozi ama mwanachama) ajiulize kwa nafasi yake. Nini mchango wake kwa chama? Tukiishia kupiga kelele ughaibuni haitasaidia. Sasa tunamlaumu nani ktk hili.

Hakuna kidogo kinachoshuka toka juu ambacho hatuwezi kushukuru au kupongeza. Tunapokuwa watu wakufikiria ushindi tu siku zote sijui tutakuwa tunakwenda wapi. Matatizo ya kufikiria juu ya ushindi bila kuwa na wazo la kushindwa itatupeleka pabaya.

Hii ni sawa na mume kumlaumu mke kwani nini hashiki mimba, kumbe tatizo analo yeye mume. Utadhani mke ni kiwanda cha kuzalisha mbegu. Unaona sasa: wa kulaumiwa ni mke. Kwa nini? Hatujifikirii wenyewe.

Kuna mambo mengi yanayosababisha kushindwa, nadhani tunajua sote. Pili, kwani hao CCM wanapenda kupoteza? Wakati CHADEMA wanaweka mikakati ya ushindi CCM wamelala? Hii ni ajabu kweli.
 
Siku zote mapenzi yasizidi ukweli. Ili tuwe na vyama imara vya kisiasa tofauti na miaka 50iliyopita lazima kuwena mabadiliko ya kufikiri na kutenda. CCM imefika hapa kwasababu kila wakionywa watu wanaambiwa hawana mapenzi na chama.Marehemu Kolimba alisema chama kimepoteza dira akaitwa Dodoma na bahati mbaya hakuishi kuona upotevu wa dira.

CDM lazima wakubali ukweli nakukabiliana nao. Ushabiki na mapenzi yasiyosimama katika ukweli yanakimaliza chama.
Naunga mkono hoja kuwa lazima kuwepo uwajibikaji kutokana na matokeo hayo.
Matokeo ni mabovu sana the least to say.

Kulalamika na kutafuta visingizio hakutatoa suluhu ya tatizo.
Tumewahi kusema na bahati mbaya kukaripiwa na wanachama,manazi na wapenzi wa CDM.
Tumesema kuwa chama hakijajiimarisha huko vijijini, tukaongeza kuwa baada ya mikutano kuna nini kinafuata ili kujua kuwa ujumbe umefika, mkakati umewekwa na vipingamizi vinaondolewa?

Tumesema kuwa dola haishikwi na umaarufu wa mtu mmoja bali chama as whole.
Tumesisitiza kuwa hivi huko mikoani na katika wilaya CDM haina uongozi kiasi kwamba kila jambo lazima limsubiri Dr Slaa, Mbowe, Mnyika au Lema?

Tumeeleza kuwa chama lazima kiwe taasisi inayojitegemea na si kundi la watu maarufu.
Tukasisitiza kuwa huu si muda wa migongano bali kujenga jama.
Tukaonya kuwa hakuna mtu anayeweza kuwa Rais wa Tanzania kwa kura za Lumumba au Kinondoni peke yake.

Tukauliza, je CDM walitafuta chanzo cha upigaji kura mdogo Mbeya, Iringa, Tarime n.k.?
Hakuna anayesikia wala kuchukua ushauri, sasa tunasikia lawama za daftari, tunaambiwa kesi nyingi mahakamani, watu wameumizwa n.k. Mbona haya hayakusemwa juzi na wiki mbili zilizopita yanajitokeza leo?

Lazima watu wawajibike kuanzia katika wilaya, mikoa na kitaifa ili kujenga chama chenye nidhamu.
Kinyume chake tutaendelea kusikia wagombea Urais ambao wataishia kukaribishwa katika ziara na dhifa za kitaifa si kukaa mbele ya bendera ya taifa.

Something is wrong, let us be honest.
 
Kuna wakati Saddam Hussein alishinda uchaguzi Iraq kwa 100% wengi tuliaminishwa kwamba anapendwa na watu wake, kumbe hila zake zilikuja kubainika baadaye kuwa kilikuwa ni kiini macho. ujanja ujanja huu wa CCM nao una mwisho wake.
 
Kama kweli wapo wana CDM (wanachama, wapenzi na mashabiki" wanaridhika na matokeo haya basi nina uhakika mwaka 2015 CDM itakaposhindwa kuchukua nchi watakuja na visingizio vingine ili kwanini wajiandae tena kwa 2020. Haiwezekani kukosekana sababu. Watu wanafikiria kuwa daftari la wapiga kura likiboreshwa basi wana CDM wengi ndio watajiandikisha. Hawadhanii kuwa wapo wana CCM wengi na mashabiki wa CCM ambao nao watajiandikisha.

Swali la msingi si daftari la wapiga kura kwanza ni wanachama. Kitila - CDM ina wanachama wangapi sasa na wameongezeka kwa kiasi gani kutoka 2010?
Haya ni mawazo yako sisi tuna Rais wetu Kijana ataingia Ikulu tu, kazi ya kujenga chama na kuandaa mazingira ya ushindi siyo kazi yetu, tuna jembe la ukweli!!"........
 
Dah! Watz ni watu wa kukata tamaa mapema sana! Kwa hali hii hatuwezi kuleta mabadiliko ya kweli, kumbuka black people in America under Martin Luther King jinsi walivyokuwa wavumilivu mpaka walipofikia goals zake za kuondoa Racism na exploitation in America,
Jaman kumbukeni wakina Steve Biko, Duo Bious, Malcom X na wengne wengi dunian walivyokuwa na strong with long determination ktk kutafuta mabadiliko, Leo hii CHADEMA mnajua kabisa sababu za kutokufanya vizuri sana ktk huo uchaguzi but mmekuwa vipofu namna hii na kuanza kujidharau.

Please guys hebu kuweni strong bhana ili muone matunda ya M4c kkwa kuanzia na uchaguzi wa ubunge sumbawanga mjini na Igunga then 2015 ikulu....!
Tuamini ktk Mbowe, Dr.slaa, Kabwe Zitto etc that CHADEMA kitakuwa salama.

Too long is not forever.
Peoples power!
Viva CHADEMA.
 
Siku zote mapenzi yasizidi ukweli. Ili tuwe na vyama imara vya kisiasa tofauti na miaka 50iliyopita lazima kuwena mabadiliko ya kufikiri na kutenda. CCM imefika hapa kwasababu kila wakionywa watu wanaambiwa hawana mapenzi na chama.Marehemu Kolimba alisema chama kimepoteza dira akaitwa Dodoma na bahati mbaya hakuishi kuona upotevu wa dira.

CDM lazima wakubali ukweli nakukabiliana nao. Ushabiki na mapenzi yasiyosimama katika ukweli yanakimaliza chama.
Naunga mkono hoja kuwa lazima kuwepo uwajibikaji kutokana na matokeo hayo.
Matokeo ni mabovu sana the least to say.

Kulalamika na kutafuta visingizio hakutatoa suluhu ya tatizo.
Tumewahi kusema na bahati mbaya kukaripiwa na wanachama,manazi na wapenzi wa CDM.
Tumesema kuwa chama hakijajiimarisha huko vijijini, tukaongeza kuwa baada ya mikutano kuna nini kinafuata ili kujua kuwa ujumbe umefika, mkakati umewekwa na vipingamizi vinaondolewa?

Tumesema kuwa dola haishikwi na umaarufu wa mtu mmoja bali chama as whole.
Tumesisitiza kuwa hivi huko mikoani na katika wilaya CDM haina uongozi kiasi kwamba kila jambo lazima limsubiri Dr Slaa, Mbowe, Mnyika au Lema?

Tumeeleza kuwa chama lazima kiwe taasisi inayojitegemea na si kundi la watu maarufu.
Tukasisitiza kuwa huu si muda wa migongano bali kujenga jama.
Tukaonya kuwa hakuna mtu anayeweza kuwa Rais wa Tanzania kwa kura za Lumumba au Kinondoni peke yake.

Tukauliza, je CDM walitafuta chanzo cha upigaji kura mdogo Mbeya, Iringa, Tarime n.k.?
Hakuna anayesikia wala kuchukua ushauri, sasa tunasikia lawama za daftari, tunaambiwa kesi nyingi mahakamani, watu wameumizwa n.k. Mbona haya hayakusemwa juzi na wiki mbili zilizopita yanajitokeza leo?

Lazima watu wawajibike kuanzia katika wilaya, mikoa na kitaifa ili kujenga chama chenye nidhamu.
Kinyume chake tutaendelea kusikia wagombea Urais ambao wataishia kukaribishwa katika ziara na dhifa za kitaifa si kukaa mbele ya bendera ya taifa.

Something is wrong, let us be honest.

Nguruvi, inaonekana mjadala huu umekuwa mrefu sana sasa jambo la msingi kwanza kama wanachama tushikamane na kusimamia hayo hapo kwenye RED mengine yatafuata.
 
Mimi sishangai, MM anashida na uongozi wa CHADEMA kwa muda mrefu sana, na hasa Mwenyekiti kamanda Freeman Mbowe. Ngoja tuone, ila wachache wenye moyo wa ukombozi, tuendelee kuwatia moyo viongozi wetu.
 
Kuna wakati Saddam Hussein alishinda uchaguzi Iraq kwa 100% wengi tuliaminishwa kwamba anapendwa na watu wake, kumbe hila zake zilikuja kubainika baadaye kuwa kilikuwa ni kiini macho. ujanja ujanja huu wa CCM nao una mwisho wake.

JF sio sehemu ya porojo wakati mwingine jifunze kutoka kwa members wengine kwanza hunajua Saddam Husein alichukuaje madaraka Iraq...ebu tuambie lini ulifanyika uchaguzi Iraq na Saddam akashinda uchaguzi kwa 100% usipende kuokota maneno mtaa unaleta JF kuna Great Thinkers.
 
Dah! Watz ni watu wa kukata tamaa mapema sana! Kwa hali hii hatuwezi kuleta mabadiliko ya kweli, kumbuka black people in America under Martin Luther King jinsi walivyokuwa wavumilivu mpaka walipofikia goals zake za kuondoa Racism na exploitation in America,
Jaman kumbukeni wakina Steve Biko, Duo Bious, Malcom X na wengne wengi dunian walivyokuwa na strong with long determination ktk kutafuta mabadiliko, Leo hii CHADEMA mnajua kabisa sababu za kutokufanya vizuri sana ktk huo uchaguzi but mmekuwa vipofu namna hii na kuanza kujidharau.

Please guys hebu kuweni strong bhana ili muone matunda ya M4c kkwa kuanzia na uchaguzi wa ubunge sumbawanga mjini na Igunga then 2015 ikulu....!
Tuamini ktk Mbowe, Dr.slaa, Kabwe Zitto etc that CHADEMA kitakuwa salama.Viva CHADEMA.
Mkuu, kukata tamaa ni pamoja na kukaa kimya. Ukiona watu wanasema hao hawajakata tamaa wana wasi wasi.

Hao uliowataja walianza harakati kuanzia ground zero ndiyo maana wengine kama akina Biko, Luther n.k hawakuishi kuona matunda ya ''M4C'' zao.

Chadema kimekuta system ipo tayari, huu ni mwaka wa 20 sasa mwendo ni wa kusua sua bado wanachama wao wanaambiwa wawe wavumilivu.

Chama kilicho na umaarufu na kukaribia kuchukua dola kinatakiwa kisimame toe to toe na chama tawala.
Leo miaka 20 ya chama bado watu wanaaminishwa kuwa kuchukua viti 5 kati ya 27 ni mafanikio makubwa! what? Tulitarajia ingechukua japo viti 14. In fact wameongeza viti 3.

Ukiangalia resources zilizotumika na hayo 'matunda ya M4C' ni sawa na kulima eka moja halafu ukavuna gunia moja na bado unasema umefanikiwa! gi me a break!

Tunaposema watu wawajibike hatuna maana uongozi wa kitaifa. Tuna maana kuanzia kwenye kata, wilaya, mkoa, sekretariati na hadi national level kama ikibidi.

Sisi wengine ni washauri tu hasa baada ya kuona kila dalili ya kuendelea kuishi na CCM kwa miongo mingine tukisubiri akina Steve Biko wazaliwe!

Kama hakuna kuwajibika ili kuleta nidhamu basi tusitarajie kipya hata wakiingia madarakani.
Huu utaratibu wa kulindana katika uzembe hautaishia katika kata, utaendelea tu kama ulivyo utamaduni wa CCM. Hatutaki kurudi huko.

Pamoja na kuwa siku hizi viongozi wa CDM wamekimbia jamvi wakisubiri matunda ya M4C, wasamaria wema tutabaki hapa kuwaambia ukweli.

Wajibishanane na si kufikiri kugombea Urasi, utakuwaje Rais ukiwa na kata 5 kati ya 27 kwa kufikiri tu.
Matokeo ni mabaya sana na mwanachama, shabiki au mpenzi wa CDM lazima awe na wasi wasi.
 
Ngonini mbona Bawacha ilishakufa siku nyingi tu? Chadema wana Bavicha tu.

Nafikiri ni kweli kuwa baraza la wanawake chadema halifanyi kazi vizuri.

Jamii ya wafanyakazi na wafanyabiashara ni waoga sana japo tunajua ndio wenye uelewa mkubwa kuhusu ubovu wa CCM. Wengi wa wagombea wa CDM ni watu wa hali ya chini sana. Wasomi wanaogopa kushughulikiwa na serikali.

Hivyo CDM waweke mikakati ya kuwavuta wasomi la sivyo tutakuwatunakwamishwa mara kwa mara.
 
Kumbe yuko Detroit, shabashi, nilifikiri naongea na mtu ambaye yupo hapa! Kumbe anafuatilia kampeni za Obama na Romney halafu anafikiri na tanzania tunaendeshe siasa hivyo! Atuambia wafuasi wangapi wa Republican au wa Democratic walipigwa ngeu kwenye kampeni zinazoendelea!

Wakuu, mwanakijiji is a snitch.
Yes, i said it. Ananijua,
Kama anafikiri simjui, aseme nimnyime tuhela twake twa vitabu....
 
Back
Top Bottom