Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 46,820
- 67,193
Hiki kinachoitwa kujiandikisha katika daftari la wapiga kura kwa raia wote waliokidhi vigezo na wanaohitaji kupiga kura ni aina fulani ya kituko na jambo lisilo na tija yoyote katika demokrasia zaidi ya kupunguza ushiriki wa raia katika uchaguzi kwa urasimu wa ajabu ajabu tu.
Pia ni upotezaji wa pesa za walipa kodi tu kwa gharama zisizo na mashiko yoyote.
Watanzania walio na vitambulisho kama NIDA, Passport na leseni ya udereva walitakiwa waweze kupiga kura kwa hivi vitambulisho vyao, hakuna haja ya kwenda kupanga mstari tena sijui kujiandikisha au kuboresha daftari la wapiga kura.