Kisingizio: Daftari la Wapiga Kura, vyombo vya dola. Sababu?

Sasa atafanya tafiti vipi wakati yeye yuko Detroit? anataka watu wawajibike wakati yeye anabofya keybord akiwa Mac Donald wakati wenzake wapo kwenye Battle Field.
 
Kwani hujui Mwanakijiji ni mmoja wa waasisi wa CCJ?

Thats why" hata siku moja hakuna mtu anaweza kunishawishi kuwa MM ana dhamira ya
dhati ya kuchangia mabadiliko kwenye hili taifa zaidi ya kutaka kuharibu pale ambapo
mabadiko yanachomoza kwenye hili taifa.
 

Chadema wamefanya kazi kubwa kuwajengea watanzania hamasa ya kushiriki mchakato wa kisiasa kwa miaka mingi hii nchi ilikuwa imefanywa kama shamba la bibi, mimi sikubaliani na mtanzamo wa mwanakijiji anaongea kama mtu asiyejua ulingo wa kisiasa wa kati chama tawala na CHADEMA, CCM imenunua vyama vingine na kuiacha CHADEMA in isolation, vyama vingine vyote vimeacha kupambana na CCM vinapambana na CHADEMA! Tunawashukuru sana watanzania wanaoendelea kuiunga mkono CHADEMA! Hata kwenye maeneo ambayo hatukusimamisha wagombea 2010 LAKINI TUMEPATA KURA NYINGI SANA, mimi nachukulia huko ni kukua kwa chadema na kuporomoka kwa umaarufu wa CCM! Mwanakiji uje na sababu sijui zipi kunishawishi! Nakusubiria!
 

Time will tell,ukombozi uko mlangoni,hauzuiliwi na propaganda za watu kama MM.


Kwani hujui Mwanakijiji ni mmoja wa waasisi wa CCJ?

Kama ndio hivyo? kwanini Tusimuone MMJ kuwa ni9 Janga la Taifa?
YES! I mean it, kama mtu kama yeye tulitegemea ataandika makala ndefu( kiama kawaida yake) kuponda huo mfumo anabaki kuwakatisha tama wanao pambana na huo mfumo?

Madharani: kumetokea fujo kila sehemu hakuna cha Tendwa, NEC wala IGP?

Kweli Mwanakijiji unazeeka vibaya!
 
Sasa atafanya tafiti vipi wakati yeye yuko Detroit? anataka watu wawajibike wakati yeye anabofya keybord akiwa Mac Donald wakati wenzake wapo kwenye Battle Field.

Kumbe yuko Detroit, shabashi, nilifikiri naongea na mtu ambaye yupo hapa! Kumbe anafuatilia kampeni za Obama na Romney halafu anafikiri na tanzania tunaendeshe siasa hivyo! Atuambia wafuasi wangapi wa Republican au wa Democratic walipigwa ngeu kwenye kampeni zinazoendelea!
 

Kiuhalisia daftari la wapiga kura na uwepo wa shahada za wapigakura ndiyo kwa miaka mingi vitandelea kuwa changamoto kubwa ya CDM na upinzani kwa ujumla.Haviwezi kupuuzwa hata kidogo. Vimebeba haki yote ya mwananchi kupiga kura na kama vikipokwa basi hakuna haki wala ushindi halali kwenye chaguzi.

Ni rahisi sana kwa chama tawala kuproject ushindi maana takwimu zipo mikononi, kinachofanywa ni kuandaa mapema utaratibu wa kununua/kupoka shahada za kupigia kura na kucheza na orodha iliyopo kwenye daftari hii ikiwa ni pamoja na kutokulihuisha. Mchezo huu umetumika sana kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 na umefanikiwa.

Hata hivyo, kitendo cha mwananchi kuuza au kukubali shahada yake ichukuliwe ili asipige kura ni tatizo linalotokana na kukosekana kwa elimu ya uraia. Yaani elimu ya uraia inayotolewa na CDM na wapinzani kwa ujumla haijatosha kiasi cha kuwafanya wananchi wafahamu umuhimu wa kupiga kura na kuleta mabadiliko katika maisha yao. Swali gumu ni Je chini ya mfumo wa ufukara uliojikita vijijini unawezaje kumshawishi mwananchi asiuze shahada yake? Akale wapi? Maana hata hiyo kesho yake hajui itakuaje.

Lakini pia ieleweke kwamba kutekeleza shughuli za kisiasa tena za upinzani katika nchi kama yetu ni kazi ngumu sana. Vifo ni vingi, mateso ni mengi, majonzi ni mengi na kwa hakika maumivu ni makubwa. Kwa viongozi wa CDM kupambana na hali kama hiyo na kuweza kufikisha vuguvugu hilo katika kiwango tunachokishuhudia kwenye matokeo haya ya udiwani na mengine mengi si kazi ndogo na ya kupuuza hata kidogo.

Tunaweza kutamani kuiona CDM kweli ikisukumwa na nguvu ya ushindi kuelekea 2015 lakini ni kwa maumivu hayo na watu kujitoa katika kukabili mateso yote hayo.Je ni akina nani wako tayari kupigwa risasi, kufunguliwa kesi zaidi ya nne mahakamani? Na tujitokeze sasa tutoke humu JF twende kwenye majukwaa. Maumivu ni makubwa kwa wachache,wengi wanasubili matunda baada ya wengi kuumia.

Uchaguzi huu mdogo wa madiwani matokeo yake ni mazuri kwa CDM, imeweza kutetea kata zake mbili na imeongeza tatu. CDM imegain na CCM imepoteza. Ni vema tukasubillil tathimini ya CDM ili tuweze kuanza kutoa lawama na hapo ndipo wanamageuzi wa kweli inabidi waanzie kujadili na kupanga mikakati ya kuutafuta ushindi mwaka 2015.
 

M4C ndio imezaa kata 3 jipangeni upya msitafute mchawi.
 
Chama Kinashinda MM anaona is nothing? maovu yanazidi bastora, mikuki na mapanga yeye anaona poa tu, hakuna kilichofanyika? kweli pesa mbaya sana MM kashanunuliwa, Tumsubiri Pasco, labda atakuwa na mawazo chanya...
na huwa nafurahia analysis za Mchambuzi, siyo huyo mameno mengi yanayosukumwa kwa posho!
 
Chadema sio chama cha kitaifa ni chama cha kikanda ndio maana umeona watanzania walivyokikataa kwenye chaguzi za udiwani, ni chama cha kikanda.
 
Hapana kusema kuwa kuongeza kata 3 tu kati ya 29 kwa chadema pamoja na popularity yote hii ni makosa , huo ni mwendo wa konokono kwa chama ambacho kinatarajia kushika dola hapo 2015! Ikumbukwe kuna M4C inatembea nchi nzima nilitarajia sana kuona reflection ya M4C kwenye hizi chaguzi ndogo za udiwani! Tusijipe moyo na hzi kata mbili tatu eti tumeongeza?? Viongozi wa juu waliopewa dhamana ya kuongoza chama lazima waje na majawabu haraka sana kuhusu haya:
1.Tathmini sahihi ya M4C je imeimarisha chama kwa kiasi gani na je iendelee au isimamishwe
2. Ni nini kimepelekea kupata kata chache hivo huku kukiwa na M4C na chadema kuungwa mkono na wananchi wengi kwa michango ya fedha na mawazo na kujitolea kwingi?
3.Mikakati madhubuti kwa ajili ya chaguzi ndogo za ubunge zijazo, kuna umuhimu wa kushiriki? kama ndio kwa nn? kama hapana kwa nn?
4.Mikakati madhubuti ya chaguzi za serikali za mitaa mwakani
5. Mbinu mikakati na malengo ya uchaguzi mkuu wa 2015
Tulio wengi tumevunjika moyo sana na matokeo hayo na tupo kusaidia kujua tatizo liko wapi ili lengo na azma yetu ya kushika dola na kutatua matatizo ya watanzania litimie hapo 2015!
 
M4C ndio imezaa kata 3 jipangeni upya msitafute mchawi.
Kuwa mstaarabu, tushindane kwa hoja, siyo vibwagizo Mkuu, Mfano M4c imezoa kata 3, ulitaka izoe ngapi, kwa nini?
ok niliuliza hivi Unaelewa mana ya VUGUVUGU la mabadiliko?

Mabadiliko huwa hayaji siku moja? Leo masikini kesho tajiri? ok Madhumuni ya M4C unayafahamu? twende kwa hoja,
 
Chadema sio chama cha kitaifa ni chama cha kikanda ndio maana umeona watanzania walivyokikataa kwenye chaguzi za udiwani, ni chama cha kikanda.
kaa kimya wewe gamba! kama huna mchango just keep quite!
 

Mwanakijijini na wenzake wameifanya kazi yao kw auamkini mkubwa sana.Na si wao tuu wapo pia wachambuzi wengine wa kisiasa ambao kazi yao ni kujenga kwanza jina huku wakipata msaada wa kukubalika na watu fulani,baada ya kujenga status ya usupa staa basi kinachofuatia ndio hii kuibuka na theories fulani huku wakienjoy status yao iliyokubalika kama great thinker.

Tutaona mengi zaidi.Kwa bahati mbaya nimesoma machapisho yake ya nyuma amabyo alikuwa kila akibanwa ana mwambia mtu akatafute,nilimbana aweze links, ingawa pia niliamua fuatilia.NIlichokuwa nikisoma nilipata mshtuko jinsi gani huyu jamaa amekuwa akipata adavantage hivyo,kuna maeneo mambo yapo wazi kabisa kuwa si agenta wa change.ila alijitahidi sana kutumia populism kuwa drag wengine ktk bandwagon.

Huyu jamaa amekuwa akimegewa vipande vidongo vya kueafanya watu wamwone kuwa naye ni mpambanaji wa ufisadi and the sort,kuwa na naye ni mshauri wa CDM na ushauri wake ilileta matokeo km alivyopredict.Ila mimi niliona vitu tofauti,alikwenda kama miangango ya CCM na CUF ilivyokwenda.Sishangai anachofanya hapa.
 
Pasco hana jipya ni karani wa Lowasa.
 
kata tatu kati ya 29 ni achievement lakini ni sawa na mwendo wa kobe au kinyonga kuelekea kushika dola hapo 2015 lazima tukubali matokeo haya yamekuwa beyond our expectation na viongozi watupe maelezo what actually happened na pia watoe dira kwa chaguzi zijazo ila ni upuuzi kushereekea kata 5 kati ya 29 hasa kwa chadema wangekuwa ADC au PONA au UDP au TADEA walipaswa kushangilia hata kwa miezi miwili lakini for chadema noooooo!!we have to look back and plan the future of our party
 
Sasa atafanya tafiti vipi wakati yeye yuko Detroit? anataka watu wawajibike wakati yeye anabofya keybord akiwa Mac Donald wakati wenzake wapo kwenye Battle Field.

Huyu jamaa anajitahidi sana ku derail kila kitu CDM wanachosimamia ili kuwafanya invalid before 2015.Sasa katoka katika ,viongozi wa kitaifa kuingia ktk kampeni, ka downpaly ufisadi, kaingia katika daftari la wapiga kura sasa.Bado atazidi sana kuandika" irresponsibly".

Ila we hatupo hapa kushuhudia watu wakijitahidi tudanganya just beause wapo kwenye mission na wapo so naive kuthibitisha kuwa wamekuja na "great idea" na theory ya kuendesha siasa za Tanzania.
 
Kuna wakati sijui hujisahau au hukusudia ktk kuwapa ushauri na tahadhari CDM huwa anatumia "tu___,sisi,..." etc kama vile anataka jiweka ktk kundi.
 

Nadhani wengine wana divided mind (stagering faith) kwamba hivi kweli CCM itasalimika ama ama hivi kweli CDM itashinda? Yaani hawako katika perseverance na persistence ya ku persuade kuleta ushindi bali wanatamani kufikia ushindi kama vile unapewa zawadi expensive ambayo hukutolea jasho kuilipia.

Kwa mtu yeyote mwenye dhamira njema, mapenzi mema na mwenye kujali wenzake kulaumu makamanda walioko field ni kuwa provoke pasipo lazima na kuwakatisha tamaa..Watu wame uawa wengine wamevunjwa viungo vyao wamedhalilishwa, wameacha ku-enjoy na family zao kila siku wako barabarani then badala hata ya kupongeza huo ujasiri tunathubutu kuwalaumu? By the way kama na sisi tulishiriki ni vipi tulishindwa kuleta hiyo expectation tunayowabebesha wenzetu?

Ninakasirika na sitaki tena kusikia haya wheather tunashinda ama tunashindwa we can never give inn never give up tutaendelea na mapambano come 2015 come not; we will still continue maana dhamira yetu ni kuleta haki usawa na maendeleo na tunafanya kwa nguvu akili na uwezo wetu wote.....Shujaa wa kweli haogopi mapambano na wala hajilaumu bali anajifunza kwakadri anayopata nafasi ya kufanya hivyo....
 

Kwa hayo yote MM anajifanya amefumba macho hayaoni,ningemuona ana dhamira ya dhati ya kutetea
mabadiliko kama angeanzisha topic ya kukemea vurugu na vitisho vya ccm na polisi kwenye kampeni na
hata kwenye uchaguzi.Lakini anachokimbilia haraka ni kuanzisha uzi wa kulaumu viongozi wa CDM,MM
umeshindwa kufanya kazi yako vizuri umetufanya tujue kuwa wewe ni kati ya Tiss wa Tz waliopo kwa ajili
ya maslihi yao.Umeshindwa kujificha sawa na ushauri kwenye Sign ya Invisible.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…