Daftari la wapiga kura na vyombo vya dola vitabebeshwa lawama na labda vinastahili. Lakini katika hili CHADEMA inapaswa kutoa sababu zinazoeleweka zaidi ya visingizio.
Wanachama, wapenzi, na mashabiki wa CHADEMA wanapaswa kuwa wakali kidogo (au sana) ili chama kiweze kutoa maelezo yanayoeleweka ya kwanini matokeo haya hayakuwa mazuri kama watu walivyokuwa wanaaminishwa au kutarajia. Kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015 CHADEMA ilitakiwa iwe inasukumwa na upepo wa ushindi lakini hali sivyo ilivyo.
Kama majibu ya kueleweka hayapo ipo haja ya haraka ya kuanza kudai watu wawajibike au wawajibishwe.
To be continued....
Ulitaka nani abebeshwe lawama? MM hivi kweli kuwa na mfumo unaowanyima watu kutumia haki yao ya kidemokrasia ya kuwapigia kura watu wanaowataka eti kwa sababu tu hawako kwenye daftari kwa nini utaratibu huo usilalamikiwe kwa matokeo ya aina yoyote ile.
The police will not escape blame as they have not exercised prudence in excuting their responsibilities. Hivi MM unawezaje kusema hoja hizi ni visingizio, watu wanachomwa mikuki, rushwa kedekede, umafya nk?
Najua haya ni maoni yako na una uhuru nayo, lakini maoni ambayo yanawaghafilisha wasomi wako si yako tena ni ya wote tafadhali jitahidi kama ambavyo umekuwa ukifanya huko nyuma kutuletea a well cooked ideas